Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 4/8 uku. 30
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Hazina za Waroma Zapatikana Uingereza
  • Tetemeko Baya Sana la India
  • Matatizo ya Kusoma na Kuandika Nchini Kanada na United States
  • Sifa ya Makasisi Yapungua
  • Wanyama wa Pori wa India Wamo Hatarini
  • Ripoti ya Afya Ulimwenguni
  • Vifo Vihusikavyo na Kuvuta Sigareti Katika United States Vyapungua
  • Mtamauko na Moyo
  • Bado Hakuna Mwisho
  • Magonjwa ya Kuambukiza Katika Karne ya 20
    Amkeni!—1997
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1992
  • Magonjwa Je! Kuna Siku Yatakapokwisha?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Hali ya Afya Ulimwenguni—Mwanya Unaozidi Kukua
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 4/8 uku. 30

Kuutazama Ulimwengu

Hazina za Waroma Zapatikana Uingereza

Akiba ya sarafu 14,780 za dhahabu, fedha, na shaba nyeusi, na vilevile mkufu wa dhahabu wenye urefu wa sentimeta 90, bangili 15 za dhahabu, karibu vijiko 100 vya fedha, vimepatikana kwenye shamba moja katika Suffolk, Uingereza. Hazina hiyo iligunduliwa na mtunza-bustani aliyestaafu ambaye alikuwa akitumia kitafuta-chuma katika kutafuta nyundo yake iliyopotea. Mstadi mmoja amekadiria thamani ya hazina hiyo kuwa angalau dola milioni 15. Baraza la mahakama iliamua kwamba hazina hiyo ni mali ya Serikali ya Uingereza, jambo linalomaanisha kwamba Eric Lawes mwenye miaka 70, aliyepata hazina hiyo, atapewa malipo ya hisani ya fedha zinazotoshana na thamani ya hazina hiyo katika soko. Hazina hiyo imewekwa katika wonyesho wa umma katika Chumba cha Hifadhi ya Vitu vya Kale cha Uingereza, laripoti Guardian Weekly.

Tetemeko Baya Sana la India

“Akiwa na kichwa cha ndovu na mwili wa mtu mwenye kitambi, Bwana Ganesha ni mojapo miungu wa Wahindu inayopendwa sana, akiwa mungu wa vyanzo vipya na bahati nzuri,” lasema gazeti Time. Lakini saa chache tu baada ya kumalizika kwa sherehe ya siku kumi kwa heshima ya mungu huyu wa bahati nzuri, eneo la kusini-magharibi mwa India lilitikiswa na tetemeko la ardhi lililoangusha nyumba nyingi katika vijiji na miji zaidi ya 50. Kijiji cha Killari, kilichokuwa karibu zaidi na kitovu cha tetemeko hilo lililokuwa kwa kiwango cha 6.4 kwenye kipimio cha Rikta, kiliharibiwa kabisa kwa asimilia 90. Makadirio fulani yaonyesha kulikuwa na vifo zaidi 20,000, likifanya tetemeko hilo la ardhi kuwa tetemeko baya zaidi kupata kutokea katika bara hilo la India kwa miaka 58. Vifo vingi vilitokana na ujenzi mbaya wa nyumba, ambazo zilijengwa kwa matope, zilizoanguka na kuzika wakaaji wazo bali havikutokana hasa na tetemeko lenyewe. Kwa kielelezo, lile tetemeko la ardhi la San Francisco lililotukia miaka michache iliyopita lilikuwa kwenye kiwango cha 6.9 katika kipimio cha Rikta. Lakini, inaripotiwa kwamba watu 67 pekee walikufa, kutia ndani na vifo vilivyotokana na maradhi ya moyo.

Matatizo ya Kusoma na Kuandika Nchini Kanada na United States

Uchunguzi wa serikali wa miaka minne juu ya kujua kusoma na kuandika katika United States umeonyesha kwamba “karibu nusu ya wakazi ambao ni watu wazima milioni 191 hawajui Kiingereza vizuri vya kutosha kuandika barua ya kulalamikia makosa ya hesabu au kutambua umbali wa safari ya basi kutoka katika ratiba iliyochapishwa,” laripoti The New York Times. Jambo hilo lamaanisha kwamba wanapata ugumu kwa mambo ya kila siku, kama kupokea habari kwa usahihi kutoka kwa gazeti, kujaza fomu za akiba ya benki, kusoma ratiba za basi, au kujua kutokana na kibandiko kiasi kifaacho cha dawa za kumpa mtoto. Uchunguzi mwingine rasmi uliofanana na huo nchini Kanada ulitaja kwamba “uwezo wa kusoma wa asilimia 16 ya watu wazima wa Kanada ni mdogo mno kuweza kuwasaidia kushughulikia habari nyingi zinazoandikwa zinazopatikana katika maisha ya kila siku” na kwamba asilimia nyingine 22 waweza kusoma tu maandishi yanayosema waziwazi jambo fulani rahisi na ambayo yamo kwa muktadha wanayoelewa, hayo ni kulingana na The Globe and Mail. Kutojua kusoma na kuandika kumefanya biashara nyingi zipoteze mabilioni ya dola kwa kukosa mazao, kupata makosa, na kwa aksidenti.

Sifa ya Makasisi Yapungua

“Mahoji ya Gallup yaonyesha kwamba kila mwaka tangu 1988 watu wengi zaidi wanaamini kwamba dini inapoteza uvutano wao kwa watu kuliko wale wanaoamini kwamba dini inaongeza uvutano wao kwa watu,” lasema Los Angeles Times. Sababu moja ni kwamba kazi ya ukasisi inapoteza sifa mbele ya umma. Miaka minane iliyopita kilele cha asilimia 67 ya Waamerika waliwaona makasisi kuwa wa hali ya “juu” au hata “juu zaidi” kwa unyoofu na adili. Uchunguzi wa 1993 ulionyesha upungufu wa asilimia 53. Kwa nini? Kashfa zinazohusu tabia mbaya za kingono za waeneza evanjeli wa televisheni, mapasta wa Kiprotestanti, na makasisi wa Katoliki zimeshusha hadhi ya makasisi, jinsi ambavyo mizozo ya ukusanyaji fedha imefanya pia. Kufikia 1988, wauzaji dawa walikuwa wameondoa makasisi kuwa wa kwanza katika kuheshimiwa na umma. Uchunguzi mwingine hata ulionyesha kwamba biashara zenye kujitegemea, pamoja na kompyuta na tekinolojia, zilishinda makanisa katika kuwa na uvutano mzuri kwa watu. Lakini umma ungali unaona kwamba makasisi ni wanyoofu kuliko wanasiasa na waandishi wa habari.

Wanyama wa Pori wa India Wamo Hatarini

Maofisa wa Wizara ya Muungano wa Mazingira walikuwa tayari mwaka uliopita kutangaza matimizo yao katika kuokoa simba-milia wa India walipogundua jambo tofauti kabisa: Simba-milia wanaelekea kutoweka. Simba-milia wapatao 1,500 kati ya wale 4,500 walio porini wameuawa na wawindaji-haramu tangu 1988. Karibu kila sehemu ya simba-milia hao wanaouawa—ngozi, mifupa, damu, na hata viungo vya uzazi—huuzwa kimagendo kwa fedha nyingi sana. Magendo pia inafanya wanyama wengine wa India waelekee kutoweka. Idadi ya vifaru wanaouawa kwa ajili ya pembe zao imeongezeka. Ndovu wa kiume wanauawa tena kwa ajili ya pembe zao. Aina zote za chui wanauawa kwa ajili ya ngozi zao, dia-muski wanachinjwa kwa ajili ya mifuko ya manukato iliyoko chini ya tumbo zao, na dubu-mweusi wanachinjwa kwa ajili ya nyongo zao. Na zaidi, nyoka na kenge wanauawa kwa ajili ya ngozi zao, na nguchiro kwa sababu ya manyoya yao magumu, yanayotumiwa kutengeneza brashi. Wanyama wengine, kama vile kobe na kozi, husafirishwa nje kimagendo katika biashara haramu ya wanyama wa kufugwa. Walinzi wa misitu wanahofia uhai wao kwa sababu ya wawindaji-haramu wenye silaha kali zaidi.

Ripoti ya Afya Ulimwenguni

Likionyesha wakati ujao usio na tumaini katika pigano dhidi ya maradhi, Shirika la Afya Ulimwenguni, katika ripoti yalo ripoti ya nane ya hali ya afya ulimwenguni, lasema hivi: “Yaonekana maradhi ya kitropiki yameongezeka sana, huku kipindupindu kikienea hadi mabara ya Amerika kwa mara ya kwanza katika karne hii, homa ya manjano na kidinga-popo zikiambukiza watu wengi hata zaidi, na hali ya kukabili malaria inadhoofika . . . Pigo la Ukimwi laendelea kupanuka ulimwenguni pote . . . kifua-kikuu kinaongezeka . . . Hesabu ya visa vya kansa katika nchi zinazositawi kwa mara ya kwanza imepita hesabu ya visa vya kansa katika nchi zilizositawi. Kisukari kinaongezeka kila mahali.” Ripoti hiyo ikishughulikia kipindi cha kati ya 1985 na 1990, ilionyesha kwamba vifo milioni 46.5 kati ya vifo milioni 50 vinavyotokea kila mwaka hutokana na magonjwa na maradhi na kwamba karibu watoto milioni 4 kati ya wale milioni 140 wanaozaliwa kila mwaka hufa kwa muda wa saa kadhaa au siku kadhaa baada ya kuzaliwa. Visa vipya milioni 7 vya kansa hutokea kila mwaka, na zaidi ya watu milioni moja huambukizwa ile virusi HIV isababishayo UKIMWI. Kwa upande mzuri, maradhi mengine ya utoto, kama vile surua na kifaduro, yanapungua, na tazamio la urefu wa maisha limeongezeka kwa kati ya mwaka mmoja na miaka miwili. Wastani wa dunia nzima ni miaka 65.

Vifo Vihusikavyo na Kuvuta Sigareti Katika United States Vyapungua

Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Maradhi vya U.S. (CDC) vimetangaza kwamba vifo vitokanavyo na uvutaji wa sigareti vimepungua—kwa mara ya kwanza tangu rekodi ianze kuwekwa tokea 1985. Idadi ya Waamerika wanaokufa kutokana na kuvuta sigareti ilipungua kwa 15,000, ikifikia 419,000 katika 1990, hasa kwa sababu ya kupungua kwa maradhi ya moyo yanayotokezwa na uvutaji wa sigareti. Asilimia ipatayo 42.4 ya Waamerika walikuwa wakivuta sigareti katika 1965. Kufikia 1990 ilikuwa imekuwa asilimia 25.5. Hata hivyo, uvutaji wa sigareti ungali kisababishi kikubwa zaidi cha maradhi yanayoweza kuzuilika na cha vifo nao unaongeza gharama za afya kwa karibu dola bilioni 20 kwa mwaka. Ingawa serikali hutumia karibu dola milioni 1 kila mwaka katika kutoa matangazo dhidi ya uvutaji wa sigareti, biashara ya tumbako hutumia dola bilioni 4 kwa matangazo ya biashara ili kuongeza uvutaji wa sigareti. Uvutaji wa sigareti hufanya mvutaji apoteze wastani wa miaka mitano ya muda wa kuishi, laripoti CDC.

Mtamauko na Moyo

“Mtamauko wenye kuendelea bila kukoma na maumivu ya kihisia-moyo huongeza sana uwezekano wa mtu kupata maradhi ya moyo na kufa kutokana nayo,” lasema Science News. “Mtamauko na huzuni unaoendelea kwa miaka mingi, na ambazo hasa haziwi ‘mshuko mkubwa wa moyo,’ zaweza kudhoofisha kazi ya moyo,” watafiti wasema hivyo. Wachunguzi walichunguza watu wazima 2,832, wenye umri wa miaka kati ya 45 hadi 77, kwa wastani wa miaka 12. Kwanza wote hawakuwa na maradhi ya moyo na magonjwa mengine ya kudumu. Uchunguzi huo ulionyesha kwamba vifo kutokana na maradhi ya moyo vilikuwa mara nne zaidi miongoni mwa watu walioripoti kutamauka sana kuliko wale ambao waliripoti kutotamauka na kwamba wale ambao walikuwa wameshuka moyo walielekea zaidi kuwa na maradhi ya moyo yasiyotokeza vifo. Kiwango cha vifo kutokana na maradhi ya moyo kilikuwa cha juu sana hata miongoni mwa watu walioshuka moyo kidogo na kutamauka kidogo kikilinganishwa na wale walioripoti kutotamauka.

Bado Hakuna Mwisho

Katika 1989, Craig Shergold, mvulana mmoja Mwingereza mwenye umri wa miaka saba, alikuwa akiugua uvimbe wa ubongo na hakutazamiwa kuishi. Tamaa yake ilikuwa ni kuvunja rekodi ya ulimwengu ya kupata kadi nyingi zaidi za kumtakia mema. Jambo hilo likitangazwa kwa vyombo vya habari pamoja na Shirika la Kimataifa la Tamaa za Watoto lenye makao makuu katika Atlanta, rekodi hiyo ilivunjwa baada ya miezi michache. Kadi zaidi ya milioni 16 za kumsalimu zilipokewa katika mwaka wa kwanza, na milioni 33 kufikia 1992. Zingali zinapokewa kwa kiwango cha kadi 300,000 kwa juma ingawa ombi lilitolewa miaka miwili iliyopita kwamba zisipelekwe tena. Jumla yote ilikuja kuwa milioni 60. “Tuna bohari yenye ukubwa wa meta za mraba 900 iliyojazwa kufikia dari kadi ambazo hazijafunguliwa,” asema Arthur Stein, msimamizi wa shirika hilo. Kupitia msaada wa mfadhili fulani, Craig alifanyiwa upasuaji mapema katika 1991, na asilimia 90 ya uvimbe huo uliondolewa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki