Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 6/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kucheza Kamari Ni Zaidi ya Fedha
  • Kudhoofisha Biblia
  • Uvuvi Wahatarishwa
  • Gharama Zinazopanda za Supu ya Viota vya Ndege
  • Polisi Wachukua Hatua juu ya Mifuko Mizito ya Shule
  • Upongezaji Hushinda Mkazo
  • Watoto Watorokaji
  • Upungufu Mkubwa wa Maji
  • Uchafuzi wa Makelele
  • Viwango vya Jela Vyaongezeka
  • Watoto Ambao Husoma na Kuandika Vizuri Mno
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1992
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1997
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1993
  • Utafutaji wa Elimu Nzuri
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 6/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Kucheza Kamari Ni Zaidi ya Fedha

Kulingana na gazeti la habari The Sydney Morning Herald la Australia, kukiwa na ufunguzi wa kasino mpya, serikali inakabiliana na tatizo isilokuwa ikitazamia: “wazazi wawaachao watoto wao ili kucheza kamari.” Watoto kadhaa wamepatikana wakiwa wamefungiwa garini huku wazazi wakitumia saa nyingi kwenye meza za kamari. Kisa kimoja kilicho kibaya sana kilikuwa kile cha mvulana mwenye umri wa miaka mitano na dada yake mwenye umri wa miezi 18 waliofungiwa garini kwa muda wa saa tano hadi walipofunguliwa na polisi saa moja asubuhi. Ishara zilizo dhahiri katika lugha kadhaa sasa zimewekwa nje ya kasino moja zikionya wazazi kwamba wanakabili faini ya dola 5,000 na uwezekano wa kutiwa mbaroni kwa kuwaacha watoto wao katika hali hii. Kulingana na The Herald, mfanyakazi mmoja wa kijamii aliona kwamba uraibu wa kucheza kamari pia umeongoza kwenye “mivunjiko ya ndoa, uhalifu, kupoteza kazi na ujiuaji.”

Kudhoofisha Biblia

Oxford University Press imetayarisha fasiri mpya ya Biblia yenye mabadiliko chungu nzima. Katika jaribio la ‘kutoudhi kikundi chochote cha watu,’ hiyo fasiri yaepuka taarifa ambazo zingeweza kufafanuliwa isivyofaa kuwa za kingono, ujamii, ama zenye waa la kupinga Wayahudi. Kwa kielelezo, hiyo fasiri mpya yamrejezea Mungu kuwa “Baba-Mama.” Yesu atakuwa si “Mwana wa mwanadamu” bali, “Aliye Binadamu.” Hiyo fasiri haina rejezo lolote kwa Wayahudi kuwa walimuua Yesu Kristo. Hata kupotolewa kusikofaa dhidi ya watu wa mkono-kushoto kutaondolewa wakati “mkono wa kulia” wa Mungu unapokuwa ‘mkono wake wenye nguvu’ lasema The Sunday Times.

Uvuvi Wahatarishwa

Misafara ya uvuvi ya mataifa tofauti-tofauti itetapo juu ya utamalaki wa eneo la uvuvi na haki za uvuvi, ripoti fulani ya Worldwatch Institute yaonya kwamba vuno la samaki ulimwenguni limefikia upeo walo na kwa hakika sasa lapungua katika maeneo mengi duniani. Huku ikikubali kwamba uchafuzi wa kimazingira umekuwa kisababishi katika upungufu wa tufeni kuhusu uhai wa baharini, hiyo ripoti yasema kwamba kuvua kupita kiasi na biashara kubwa za uvuvi ni sababu ya msingi ya idadi inayopungua ya samaki wanaovuliwa katika bahari kuu za Atlantiki na Pasifiki pamoja na bahari Nyeusi na Mediterania. Idhaa ya habari ya Agence France-Presse yasema kwamba kulingana na ripoti ya Worldwatch, uvuaji umepungua kwa asilimia nyingi kufikia 30 katika maeneo fulani na kwamba ikiwa huko kusimamia kwa sasa kusikofaa kwa rasilimali za bahari kuu kutaendelea, kwa uhalisi mamilioni ya wavuvi karibuni watabaki bila kazi.

Gharama Zinazopanda za Supu ya Viota vya Ndege

Katika mikahawa ya Hong Kong na majiji mengine ya Kiasia, mlo unaopendwa na wengi ni kiota cha ndege kiwezacho kulika, ambacho mara nyingi hupikwa ili kupakuliwa kikiwa supu. Kulingana na International Herald Tribune, Wachina wengi huviona viota vilivyopikwa si kama tu kinywaji kitamu bali pia chenye afya mwilini. Vikundi vya uhifadhi vyakadiria kwamba Hong Kong peke yake ilitumia karibu viota milioni 17 vya ndege mbayuwayu katika 1992. Hata hivyo, kuvivuna kupita kiasi kumepandisha gharama za uuzaji-jumla wa viota kuwa dola 500 kwa kilo, na viota vilivyoyakinishwa kuwa bora vyaweza kufikia mara nane kiasi hicho. Gharama kwa mbayuwayu anayetokeza hivyo viota ni ya juu sana. Uharibifu wa mayai na vifaranga wakati viota vinapovunwa umetokeza upungufu wa idadi fulani wa mbayuwayu na kutoweka kwa wengine.

Polisi Wachukua Hatua juu ya Mifuko Mizito ya Shule

“Uzani wa mifuko ya shule hauwezi kuzidi asilimia 15 ya uzani wa mwili [wa mwanafunzi],” asema meya wa Cantù, mji fulani katika mkoa wa Como, kaskazini mwa Italia. Huyo meya ana wasiwasi kuhusu hatari ya kujipinda kwa uti wa mgongo. Wazazi wa watoto wanaokiuka hiyo kanuni waweza kukabili faini ya lira 400,000 [dola 250 za Marekani] na kifungo cha miezi mingi kufikia sita gerezani. Ili kuonyesha kwamba alimaanisha alilosema, huyo meya alipeleka polisi wa jiji, wakiwa na mizani za kupima, ili kuweka vituo vya kuchunguzia nje ya shule mbalimbali, laripoti Corriere della Sera. Ni watoto wawili tu waliosimamishwa wakati wa huo uchunguzi waliokuwa na uzani uliohitajiwa. Kwa kweli, mvulana mmoja aliyekuwa na uzani wa kilo 34 alibeba mfuko wenye uzani wa kilo 12. Wanashule wenzake waliungana ili kumtetea, wakilalamika kwamba vitabu vya sanaa na hesabu peke yavyo vilikuwa na uzani wa kilo tano, na walihitaji kubeba vitabu vya masomo manne kila siku. Huyo meya alilaumu mashirika ya kibiashara ya uchapaji, ambayo mapendezi yayo ni “katika kuuza vitabu vizito na ghali zaidi.” Alidokeza kwamba yachapishe vitabu kwa sehemu-sehemu.

Upongezaji Hushinda Mkazo

Kila mwaka mashambulio ya moyo huzoa uhai wa watu 200,000 katika Ujerumani. Kisababishi kikuu ni nini? “Mkazo,” laripoti gazeti la habari Süddeutsche Zeitung, kwani kufanya kazi katika Ujerumani huhitaji “ujitoaji kamili, na mkazo wa daima.” Mkazo kazini hutokeza viwango vya juu vya kutokuwa kazini kutokana na ugonjwa na waweza kuongoza kwenye kuungua nishati. Kila sekunde muuguzi huugua kutokana na dalili za mkazo, na mwalimu 1 kwa 3 hustaafu mapema, wengi kwa sababu ya “mkazo wa hisi.” Makampuni ya bima ya afya yachunguza jinsi ya kupunguza mkazo kazini. Uchunguzi mmoja, uliofanywa katika mamia kadhaa ya mashirika ya wastani, waonyesha kihususa kile kinachoonekana kuwa kisababishi kinachochangia: Kati ya wafanyakazi waliochunguzwa, asilimia 44 hawakupewa kamwe pongezi yoyote kazini.

Watoto Watorokaji

Kila mwaka watoto 98,000 katika Uingereza hutoroka kutoka nyumbani, laonelea gazeti la habari The Independent. Wengi huondoka ili kutoroka ujeuri katika familia. Zaidi ya 10,000 hutoroka angalau mara kumi kabla ya kufikia umri wa miaka 16. Wakiwa wachanga mno kupata faida za utunzi, wengi wa watorokaji hawa hugeukia uhalifu na ukahaba. Tukipuuza hilo tatizo, aonya Ian Sparks, mfanyakazi mkubwa wa Children’s Society, nao vijana hawa watakua kuwa “watu wazima wasio na makao waliokwanyuliwa kutoka jamii.” Ikiwa “jamii kwa ujumla” iliweka mkazo zaidi juu ya kutegemeza na kusaidia hao wazazi, alionelea, basi “matatizo mengi hayangetukia tangu mwanzoni.”

Upungufu Mkubwa wa Maji

“Afrika Kusini inakabili janga la maji la viwango vikubwa,” laripoti gazeti la habari The Star. Vyanzo vya badala vya maji visipovumbuliwa, vyanzo vya sasa vya maji vitakwisha “kwa muda upatao miaka 15 ijayo.” Kisababishi kimoja ni ongezeko la haraka la idadi ya watu. Mvua kidogo, karibu nusu ya wastani wa ulimwengu, ni kisababishi kingine. Kiwango cha uvukizaji cha juu isivyo kawaida huzidisha hilo tatizo. Bwawa la kuhifadhia maji lililo kubwa kupita yote nchini hupoteza galoni 130,000,000 kila mwaka kwa wastani kupitia uvukizaji. Ubora wa maji yaliyoko wadidimia pia kama tokeo la uchafuzi. The Star lataarifu hivi: “Sasa kuna watu milioni 12 wasio na maji safi ya kunywa na zaidi ya milioni 20 wasio na mfumo (wa maji) wa kutosha wa usafi.”

Uchafuzi wa Makelele

Angalau asilimia 10 ya idadi ya watu ulimwenguni huugua kiasi fulani cha ukosefu wa kusikia. Gazeti la Brazili Globo Ciência laeleza kwamba “sikio la binadamu halikufanywa ili kustahimili makelele yafanywayo na jamii ya siku ya kisasa.” Kuwapo mahali penye viwango vya makelele yenye kudhuru kila siku kwaweza pia kuchangia umakinifu usiofaa, utokezaji wa chini, ukali, na aksidenti kazini.

Viwango vya Jela Vyaongezeka

Kadiri uhalifu unavyozidi kuongezeka ulimwenguni pote, ndivyo na kiwango cha kifungo kinavyozidi. Urusi sasa ina kiwango cha kifungo cha watu 558 kwa kila 100,000, ikifuatiwa na Marekani ikiwa na 519 kwa 100,000. Kisha yaja Afrika Kusini ikiwa na 368, Singapore ikiwa na 229, na Kanada ikiwa na 116. Tangu msambaratiko wa ule uliokuwa Muungano wa Sovieti, mauaji ya kimakusudi na uhalifu mwingine mbalimbali umeongezeka sana katika Urusi, na kiwango cha kufungwa jela kimepanda kupita Marekani, kiongozi wa awali. Kwa nini mataifa ya Ulaya hufunga watu jela viwango ambavyo ni sudusi moja ya kile cha Marekani? “Elezo moja ni kwamba ingawa viwango vya uhalifu wote hutofautiana kidogo kuvuka mipaka, jeuri imeenea sana katika Marekani, Urusi na Afrika Kusini,” lasema U.S.News & World Report. “Sababu ziwazo zote, mwanya wa kifungo cha jela waelekea kukua.”

Watoto Ambao Husoma na Kuandika Vizuri Mno

“Kusomea vijana vitabu hukuza stadi za kuandika,” laripoti gazeti la habari Globe and Mail la Kanada. Kulingana na matokeo ya majaribio ya majuzi yaliyofanywa na Wizara ya Elimu ya Ontario, Kanada, wanafunzi waliosema kwamba mara nyingi walisomewa hadithi walipokuwa wakikua walifanya vizuri katika mitihani kuliko wale waliosomewa kwa nadra ama hawakusomewa vitabu kamwe. Globe liliongezea kwamba “wanafunzi waliofanya vema katika kusoma pia walifanya vema katika kuandika” na kwamba “wanafunzi waliosoma mambo yasiyo ya shule walifanya vema sana katika kusoma na kuandika.” Kulingana na msimamizi wa Ontario Teachers Federation, matokeo ya majaribio yalifunua kwamba “wanafunzi ambao hawasomi ama hawana zoea la kusomewa vitabu kufikia umri wa miaka 14 hawatasoma baada ya hapo.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki