Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 2/22 kur. 3-4
  • Kutojua Kusoma na Kuandika—Tatizo la Ulimwenguni Pote

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutojua Kusoma na Kuandika—Tatizo la Ulimwenguni Pote
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kujua Kusoma na Kuandika Miongoni mwa Watu wa Mungu
    Amkeni!—1994
  • Mama na Baba Hawakusoma Naweza Kuwastahi Namna Gani?
    Amkeni!—1990
  • Kusaidia Watu Kujua Kusoma
    Amkeni!—1994
  • Jinsi Wakristo wa Mapema Walivyoandika Maandishi Matakatifu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 2/22 kur. 3-4

Kutojua Kusoma na Kuandika—Tatizo la Ulimwenguni Pote

Na mleta habari za Amkeni! katika Naijeria

ALMAZ aishi nchini Ethiopia. Binti yake alipokuwa mgonjwa, daktari alimwaandikia jinsi ya kutumia dawa fulani ya chupa. Lakini Almaz hakujua kusoma kiasi cha dawa kilichotakiwa kitumiwe—angempatia dawa kiasi gani, na wakati gani? Kwa uzuri, jirani yake alijua kusoma agizo la daktari. Yule mtoto alipewa dawa ifaavyo akapona.

Ramu ni mkulima katika India. Wakati ulipofika wa binti yake kuolewa, aliamua kuweka shamba lake rahani ili akopeshe fedha kutoka kwa mkopeshaji-fedha wa kwao. Kwa sababu hakujua kusoma wala kuandika, alitumia kidole gumba kutia sahihi hati ambayo yeye hakuelewa. Miezi kadhaa baadaye Ramu aligundua kwamba kumbe ile hati ilikuwa ni mkataba wa kuuza shamba—sasa shamba lake lilikuwa la mtu mwingine.

Michael alikuwa akifanya kazi katika shamba fulani kubwa katika United States. Msimamizi wake alimwambia apatie ng’ombe chakula cha nyongeza. Michael alipata mifuko miwili yenye maandishi katika kibanda, lakini hakujua kusoma maandishi yaliyokuwa kwenye magunia hayo. Akachagua gunia baya. Ng’ombe wakafa siku kadhaa baadaye. Kumbe Michael alikuwa amewapa sumu. Alifutwa kazi mara moja.

Kutojua kusoma na kuandika kulifanya Michael apoteze kazi yake. Kulimgharimu mwajiri wake kundi la ng’ombe wa kufugwa kwa ajili ya nyama. Kulimgharimu Ramu shamba lake. Kungelimgharimu Almaz mtoto wake.[1]

Kulingana na UNESCO (Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Tamaduni), zaidi ya robo ya idadi ya watu wazima ulimwenguni—wanaume na wanawake zaidi ya milioni 960—hawajui kusoma na kuandika.[2]a Katika nchi zinazoendelea, mtu mzima 1 kati ya kila watu 3 hajui kusoma na kuandika.[3] Kama ilivyo na Almaz, Ramu, na Michael, mamilioni hao hawawezi kusoma ishara za barabara, gazeti, au fungu fulani la Biblia. Hawawezi kusoma zile habari nyingi zipatikanazo katika magazeti na vitabu. Hawawezi kuandika barua wala kujaza fomu iliyo rahisi kujaza. Wengi hata hawawezi kuandika majina yao. Kwa sababu hawawezi kupata kazi zinazohitaji kujua kusoma na kuandika mambo ya msingi, wengi hukosa kazi, huku vipawa vyao vikibaki bila kutumiwa, uwezo wao ukikosa kukuzwa.

Tarakimu hizo hazitii ndani idadi kubwa ya watu wazima ambao hawajui kusoma na kuandika vizuri—wawezao kusoma na kuandika mambo ya msingi lakini ambao hawawezi kusoma na kuandika mambo magumu zaidi ya maisha ya kila siku.[5] Katika United States pekee, watu wazima wasiojua kusoma na kuandika vizuri ni milioni 27.[6]

Na vipi juu ya watoto? Ingawa tarakimu hazijakamilishwa, kwa sababu uchunguzi haujafanywa katika nchi zote, Shirika la Hazina ya Watoto la Umoja wa Mataifa lakadiria kwamba watoto wapatao milioni 100 ulimwenguni pote wenye umri wa kwenda shule hawataenda shule kamwe.[7] Milioni wengine 100 hata hawatamaliza masomo ya msingi.[8] Kwa kweli, Idara ya Habari ya UM yadai kwamba katika sehemu za mashambani za nchi zinazoendelea, ni nusu tu ya watoto hupokea masomo ya shule ya msingi kwa zaidi ya miaka minne.[9] Na katika nchi nyingine zenye utajiri, watoto wengi hutumia wakati wao mwingi kutazama televisheni kuliko wakati wanaotumia shuleni.[10]

Watoto wasiojua kusoma na kuandika kwa kawaida hukua na kuwa watu wazima wasiojua kusoma na kuandika. Ni jambo gani linalotokeza tatizo hilo la ulimwenguni pote? Ni jambo gani liwezalo kufanywa ili kusaidia mtu mzima asiyejua kusoma au kuandika? Maswali hayo yatazungumzwa katika makala ifuatayo.

[Maelezo ya Chini]

a Mtu asiyejua kusoma na kuandika, kulingana na ufafanuzi wa shirika la UNESCO, ni mtu mwenye umri wa miaka 15 au mkubwa zaidi ambaye hawezi kusoma wala kuandika kwa kuelewa taarifa fupi, iliyo rahisi juu ya maisha yake.[4]

[Picha katika ukurasa wa 3]

Zaidi ya robo ya idadi ya watu wazima ulimwenguni hawajui kusoma na kuandika

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki