Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 7/22 uku. 31
  • Pornografia Imo Vyuoni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pornografia Imo Vyuoni
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kuendelea Kuwa na Maoni ya Mungu Juu ya Ngono
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Jilinde Usinaswe na Mtego Huu wa Shetani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
  • Je, Ponografia Ni Raha Isiyodhuru?
    Amkeni!—2002
  • Kwa Nini Pornografia Ni Hatari
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 7/22 uku. 31

Pornografia Imo Vyuoni

“RIPOTI ya Matier na Ross” katika gazeti la San Francisco Chronicle, la Novemba 1, 1993, ilikazia juu ya somo linapopingwa linalofunzwa katika Chuo Kikuu cha Jimbo cha San Francisco. Profesa John DeCecco ndiye mwalimu wa somo hilo juu ya utendaji wa ngono wa kibinadamu. Matier na Ross watoa maelezo juu ya somo hilo kama ifuatavyo: [1]

“Ni somo lenye kuvutia wee! Ikiwa wataka kupata kiwango cha juu cha maksi tatu zinazotamanika ili upate digrii ya SFSU, chunguza tu habari zinazoleta uchu (na nyakati nyingine zilizo sahihi kisiasa) zilizoorodheshwa katika muhtasari wa somo.”

Halafu ripoti hiyo yaorodhesha kupiga punyeto, kuvaa mavazi ya watu wa jinsia tofauti, ugoni-jinsia-kiume, ugoni-jinsia-kike, kufanya ngono na wanyama, kupata raha ya kingono kwa kujiumiza au kuumiza wengine, na mambo mengine. Mihadhara juu ya baadhi ya matendo hayo yatia ndani maonyesho ya vidio.

Matendo kama hayo yaweza kulinganishwa na ‘desturi zenye kukirihisha’ ambazo Yehova huchukia, kama vile inavyoonyeshwa katika sheria ya Musa kwenye Mambo ya Walawi sura ya 18. Baada ya kushutumu matendo ya ulawiti, uzinzi, na upotovu mwingine wa kingono, mistari 22 na 23 yasema: “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo. Wala usilale na mnyama ye yote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni uchafuko [“ni kinyume cha yaliyo ya asili,” NW].”

Kuzoea mambo hayo ambayo Yehova hukirihi huleta shutumu hili lake: “Msijitie unajisi katika mambo hayo hata mojawapo; kwa maana hizo taifa nitakazozitoa mbele zenu zimekuwa najisi kwa mambo hayo yote; na hiyo nchi imekuwa najisi; kwa ajili ya hayo naipatiliza uovu wake juu yake, na hiyo nchi yatapika wenyeji wake na kuwatoa. Kwani mtu awaye yote atakayefanya machukizo hayo mojawapo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao.”—Mambo ya Walawi 18:24, 25, 29.

Mwanafunzi mmoja anayefanya mtaala huo wa SFSU alimsifu DeCecco kwa “kuondolea mbali maoni mabaya kuhusu watu wasio na adili na kuonyesha kwamba wao ni kama mtu mwingine yeyote.” Wao ni kama mtu mwingine yeyote? Kwa kweli watu walio wengi hawajiingizi katika upotovu wa kingono wa ugoni-jinsia-kiume, ugoni-jinsia-kike, na kupata raha ya kingono kwa kujiumiza au kuumiza wengine, wala hawafanyi ngono na wanyama. Ni kweli, leo katika jamii kuna mvunjiko mkubwa wa kiadili wenye kusikitisha, lakini matendo hayo yaliyoonyeshwa katika somo hilo la chuo kikuu ni pornografia ya waziwazi ikifanywa chini ya kibandiko cha usomi na utafiti.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki