Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 8/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2004
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 8/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Wazazi Wazee-Wazee Baba-mkwe wangu hawezi kutoka kitandani naye ahitaji kufanyiwa kila kitu. Kwa kuwa nimechoka kiakili na kimwili, nyakati nyingine nimepoteza saburi yangu na kusema mambo ambayo baadaye nilisikitikia. Kwa hiyo niliposoma makala hizo juu ya “Tatizo la Kutunza Wazazi Wazee-Wazee,” (Februari 8, 1994), nilihisi kana kwamba ningepasuka moyo kwa sababu ya hisia! Nawashukuru sana kwa kutayarisha habari hiyo. Makala hizo zitanitegemeza ninapoendelea kutekeleza wajibu wangu.

T. H., Japani

Nina umri wa miaka 16, na nyanya yangu sasa ahitaji utunzi wa muda wa saa 24. Yeye aishi umbali wa karibu kilometa 160. Kwa hiyo, kumekuwa na mkazo mkubwa katika familia yetu. Kwa hiyo ninataka kuwashukuru kwa ajili ya makala hizo. Zilikuwa zenye kujenga sana.

M. R., Marekani

Ninafanya kazi kwa shirika la kijamii linalosaidia wale wanaotunza wazazi wazee-wazee. Kwa kawaida, wafanyakazi wenzangu hukataa fasihi zenye msingi wa Biblia ninazowapa. Hata hivyo, kwenye mkutano wa wafanyakazi, nilimpa kila mtu nakala ya toleo hilo. Kila mmoja wao alikubali! Nalipata mfanyakazi mmoja akiisoma katika deski yake.

B. H., Marekani

Mlipendekeza kuomba moja kwa moja ndugu na dada wa kimwili wa mtu wasaidie katika kutoa utunzaji. Nilikuwa nikiamini kwamba hakuna mtu awezaye kukataa aulizwapo. Naam, sasa ninawaeleza kwamba nimewatunza wazazi wangu zaidi ya miaka kumi, na nilipowauliza ndugu zangu wanisaidie, wao walikataa. Twaishi katika ulimwengu usiojali kabisa. Afadhali watu wangeamka na kutambua kwamba kutunza wazazi wako si kazi—bali ni pendeleo!

M. D., Marekani

Maandiko yasema kwamba kutunza washiriki wa familia ni wajibu kwa Wakristo. “Mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani.” (1 Timotheo 5:8)—Mhariri.

Nilithamini sana lile shauri la kutafuta wakati kwa ajili ya mwenzi wako na kwa ajili yako mwenyewe. Nimeshindwa kufanya hivyo wakati uliopita, nikihisi kwamba utunzi wa wazazi wetu ulikuwa wa maana kuliko wakati wa kuwa na mume wangu—au wakati kwa ajili yangu mwenyewe. Hata hivyo, naona hekima ya shauri hilo, nami nitajaribu kuwa mwenye usawaziko zaidi katika hali hiyo.

M. O., Marekani

Kuhama Nina umri wa miaka 14 na ningependa kuwashukuru kwa ajili ya makala ya “Vijana Huuliza . . . Kwa Nini Ni Lazima Tuhame?” (Februari 22, 1994) Nilipokuwa na miaka tisa, baba yangu, ambaye ni mzee wa kutaniko, aliombwa ahamie kutaniko jirani. Sasa tumekuwa hapo kwa zaidi ya miaka minne na nimekuja kupenda kutaniko hilo sana. Lakini sasa baba yangu ameombwa ahamie kutaniko jingine tena. Siku tuliyoombwa tuhame, tulipokea gazeti hilo. Lilitusaidia mimi na ndugu yangu kukabiliana na hali vizuri zaidi. Ni pendeleo kuombwa kuhama, lakini ni vigumu sana kuwaaga wale wote tuwapendao.

L. B., Uingereza

Ubaguzi wa Rangi Sasa hivi nimepata fursa nzuri ya kusoma toleo lenu la Agosti 22, 1993, lenye mfululizo “Je! Jamii Zote Zitapata Kuungana Wakati Wowote?” Nilishangazwa na kuvutiwa na uelewevu wenu usiopendelea na ulio wa ndani wa tatizo hilo gumu. Hivi majuzi nilimaliza mtaala wa chuo wa somo la historia. Lakini kwa kurasa tisa pekee, gazeti lenu lilitoa historia fupi, maelezo mafupi, na suluhisho! Lilipita muhula mzima wa chuo wenye masomo ya vitabu na mafundisho.

R. J., Marekani

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki