Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 11/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Shida Kubwa ya Maji
  • Je, Ni Pokeo Linalokufa la Kijapani?
  • Tahadhari Kuhusu Michezo ya Kupumua Kasi
  • Sababu ya Magari Kuwa Machache Sana Katika China
  • Kamera Zafanyiza Tofauti
  • Kile Kizazi cha 1914
  • Okoeni Wadudu Hao
  • Lugha Zinazokufa
  • Ulimi wa Nyoka Ulio Kama Uma
  • Kusumbuliwa Kingono na Wagonjwa
  • Kuchoma Konea
  • Uhalifu Katika Nyua za Shule
  • Kusumbuliwa Kingono—Tatizo la Duniani Pote
    Amkeni!—1996
  • Naweza Kupambanaje na Kusumbuliwa Kingono?
    Amkeni!—2000
  • Kusumbuliwa Kingono—Jinsi Unavyoweza Kujikinga
    Amkeni!—1996
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 11/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Shida Kubwa ya Maji

Ripoti ya karibuni zaidi iliyotolewa na FAO (Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa) yasema kwamba nchi zipatazo 30 kuzunguka dunia zitakuwa zikikabili mapunguko mazito ya maji kufikia mwaka 2000. Kulingana na FAO, kukiwa na ushindaniaji wenye kuongezeka daima wa maji machache, mamia ya mamilioni ya watu hawatapokea kile kiasi kidogo cha maji kihitajiwacho ili kuhifadhi uhai wao. Watu walio katika hatari kubwa zaidi ni wale walio katika Afrika ya kaskazini na ya chini ya Sahara, katika Mashariki ya Karibu, na Hungaria. Ripoti hiyo, iliyotokea katika gazeti Le Monde la Paris, yasema kwamba ukulima hutumia yapata asilimia 70 (asilimia 90 katika nchi zinazositawi) ya ugavi wa maji matamu ya dunia kwa unyunyizaji. FAO lakadiria kwamba kufikia asilimia 60 ya maji haya hutapanywa kwa sababu ya njia za unyunyizaji zisizo na matokeo.

Je, Ni Pokeo Linalokufa la Kijapani?

Kicho kingi ambacho watu Wajapani wamewaonyesha wazee wao kimapokeo chaonekana kuwa kikizorota. Kutenda wazee-wazee vibaya kimwili na kisaikolojia kunaongezeka. Mainichi Daily News laeleza kwamba kulingana na mstadi mmoja, familia nyingi za kisasa hujikuta zikitunza wazee wa ukoo wao bila hiari na haziwezi kukabiliana na mkazo wa kufanya hivyo. Hizo hugeukia mara nyingi kuwatenda jeuri na kuwapuuza. Kulingana na Mainichi Daily News, katika kisa kimoja mwanamume mmoja aliingilia “tabia ya kumcharaza baba yake wa miaka 75 kama ngoma wakati wowote alipokataa kumpa fedha zake za malipo ya uzee.” Vielelezo vingine halisi vyatia ndani kufunga mikono na miguu ya mzazi mkongwe kisha kumfungia katika chumba na kushindilia matambara katika kinywa cha mwanamke mzee.

Tahadhari Kuhusu Michezo ya Kupumua Kasi

The Times la London laripoti kwamba “ufuatiaji mwingi mno wa michezo ya kupumua kasi sana” waweza kutokeza madhara ya sikio la ndani. Yaonekana kwamba vipindi vingi mno vya kuruka kisulubu vyaweza kudhuru daima vile vijipande vyepesi vya sikio la ndani. Nyingine za dalili za kawaida ni kizunguzungu, kukosa usawaziko, ugonjwa wa miendo, na mlio katika masikio. Uchunguzi wa hivi karibuni kwa wanawake waliofundisha madarasa ya michezo ya kupumua kasi mara mbili kwa siku ulifunua kwamba asilimia 83 walikuwa na matatizo ya kusikia mivumo ya kiwango cha juu. Kisababishi kingine cha kuhangaisha ni kwamba wanawake fulani huelekea kusitawisha “uchu wa mazoezi,” ambao ni uraibu wa mazoezi yenye sulubu nyingi mno. Wenye uraibu huo “hujikuta wamenyong’onyea mwishowe, wakiwa na misuli iliyokazika, mivunjiko isababishwayo na mkazo na, ikiwa wao huenda madarasa ya kujizoeza miendo ya haraka, hupatwa na matatizo ya usawaziko,” lasema The Times.

Sababu ya Magari Kuwa Machache Sana Katika China

Ikiwa na idadi ya watu zaidi ya bilioni moja, China ina magari 50,000 tu yaliyo mali ya watu binafsi. Na bado, kulingana na China Today, tarakimu hii yaonyesha “ongezeko kubwa ajabu.” Katika 1983 kulikuwa na magari 60 tu ya watu binafsi katika nchi hiyo! Idadi ya wenye magari yatarajiwa kuongezeka hivi karibuni. Hata hivyo, ni lazima atazamiwaye kuwa mnunuzi ahesabu gharama. Katika China kuna zaidi ya namna 40 tofauti za kodi ambazo hupandisha gharama ya gari. Kwa kielelezo, “gari lingeweza kuuzika kwa yuan 300,000 (karibu dola 37,000 za Marekani) katika China, lakini lisigharimu zaidi ya dola 10,000 za Marekani katika nchi nyinginezo.” Namna gani gharama ya kujifunza kuendesha? Shule moja ya uendeshaji hutoza “mara mbili za mapato ya mwaka ya mchuma-mshahara wa wastani,” lasema China Today.

Kamera Zafanyiza Tofauti

Idara ya Usafirishaji katika London, Uingereza, yaripoti punguo la kutazamisha katika hesabu ya visa vya kuvunja sheria za kwenda kasi katika maeneo ambako kamera zimewekwa kupiga picha vibati vyenye nambari za magari yanayoenda kasi. Kamera hizi huandalia wenye mamlaka picha zitumiwazo kushtaki madereva wanaoenda kasi. Zaweza pia kutokeza ithibati yenye kushtaki dhidi ya wale wapitao taa nyekundu za barabarani. Gazeti New Scientist laripoti kwamba tangu kamera hizo ziwekwe, “idadi ya watu waliopata madhara makubwa katika barabara zilizochaguliwa kwa mradi huo imepungua kwa theluthi moja.” Mara kamera hizo zilipoanza kazi, hesabu ya wastani wa magari yaendayo kasi kwa kuuzidi mpaka halali uliowekwa kwa kilometa 32 kwa saa ilipungua kutoka magari 1,000 hadi 30 kwa siku. “Kumekuwa na punguo la asilimia 40 katika idadi ya madereva wanaoziruka taa na punguzo la asilimia 60 katika hesabu ya aksidenti kwenye barabara-panda,” lasema New Scientist.

Kile Kizazi cha 1914

Ni watu 272,000 tu kati ya wanaume na wanawake 4,743,826 wa Marekani walioshiriki katika Vita ya Ulimwengu 1 waliokuwa hai katika 1984. (Amkeni!, Aprili 8, 1988, la Kiingereza) Leo idadi hiyo, kulingana na Idara ya Mambo ya Wazee-wa-Kazi, imeshuka kuwa ikadiriwayo 30,000, na umri wao wa wastani ni 95. Hata hivyo, ulimwenguni pote katika 1992 kulikuwa kungali na watu 61,486,000 wakiwa hai kutokana na kile kizazi kilichozaliwa katika 1914 au kabla ya mwaka huo.

Okoeni Wadudu Hao

Bila wadudu na viumbe wengine wasio na uti wa mgongo, “mfumo-mazingira wa duniani ungeangamia, wanadamu na viumbe wengine wenye uti wa mgongo labda wangeendelea kwa miezi michache tu, na sayari ingemilikiwa sana-sana na mwani na kuvu,” lasema The New York Times. Kwa msingi wa uchunguzi mmoja wa majuzi, makala ya Times yaonya kwamba yale mahangaiko ya watu wengi juu ya kuwaokoa nyangumi, simba-milia, na spishi nyingine zilizohatarishwa yapasa kupanuliwa yatie ndani viumbe wasio na uti wa mgongo. Viumbe wadogo hawa ndio husababisha taratibu kadhaa za maana katika mazingira, kutia na kula uoza, kuchavua mimea, kutawanya mbegu, na kuondoa takataka. Katika Marekani pekee, wanadamu hutokeza karibu tani milioni 130 za kinyesi kila mwaka, na mifugo tani zaidi ya bilioni 12. Kulingana na mstadi mmoja, asilimia 99 ya takataka hii “hufikiriwa kuwa huozeshwa na viumbe wasio na uti wa mgongo.”

Lugha Zinazokufa

Lugha kadhaa zimo katika hatari ya kutokomea katika ile nchi ya Papua New Guinea yenye unamnamna wa lugha. Tayari lugha tano zimekufa muda wa miaka 40 iliyopita. Hiyo “yaiacha nchi na lugha 867 tu,” kulingana na Post-Courier la Papua New Guinea. “Unamnanamna wa lugha [za nchi hiyo] waelezwa ni kutokana na kutengeka kijiografia kwa makabila mengi katika eneo lenye milima na misitu la kitovu cha nchi,” laeleza Post-Courier. Gazeti hilo laongeza kwamba kuna “lugha 22 zenye wasemaji wachache kuliko 100, lugha saba zikiwa na wasemaji wachache kuliko 20 na lugha 10 zenye wasemaji wachache kuliko 10.” Mojapo lugha zilizohatarishwa ni Uruava, isemwayo na watu watano. Bina na Yoba husemwa na watu wawili tu kila moja.

Ulimi wa Nyoka Ulio Kama Uma

Ulimi wa nyoka ulio kama uma una faida gani kwake? Kulingana na ripoti moja katika International Herald Tribune, ulimi huo humsaidia nyoka kufuata njia yenye manukato kwa njia kama ileile ambayo masikio yetu mawili hufanya kazi pamoja kugundua upande ambao mvumo umetoka. Awapo njiani kutafuta windo lake au mwenzi wake, nyoka huuchezesha-chezesha nje ulimi wake, akitanua ncha zao kwa kadiri iwezekanavyo. Kwa njia hii, nyoka hupima nguvu ya ile harufu kwenye ncha mbili, hiyo ikimwezesha kujua upande ambao mnyama amtafutaye yuko.

Kusumbuliwa Kingono na Wagonjwa

Uchunguzi mmoja wa majuzi wafunua kwamba kusumbuliwa kingono kazini ni tatizo zito kwa matabibu wengi wa kike. Katika uchunguzi huo, asilimia 77 ya waliokubali kutoa maoni “waliripoti namna fulani ya kusumbuliwa kingono na wagonjwa,” laeleza The Medical Post. Wengi waamini kwamba utatuzi wa tatizo hili wategemea madaktari wenyewe. Wao watiwa moyo kujichukua kwa hadhi ya kikazi na kitaalamu, wavae koti la maabara, na kuvaa pete ya arusi wanapotibu wagonjwa. Hata hivyo, wengine wahisi kwamba hakuna liwezalo kufanywa kuepuka kusumbuliwa kingono kwa madaktari wa kike. Post latoa maoni haya isemapo kwamba “madaktari wanawake ni sehemu ya jamii ambapo kusumbuliwa kingono na hofu ya kutendwa hivyo ni sehemu asili iambatanayo na kuwa mwanamke.”

Kuchoma Konea

Jarida moja la kitiba liliripoti majuzi kwamba wanawake vijana wengi wanachoma konea zao kiaksidenti kwa kuingiza ghafula vyuma vya kukunja nywele ndani ya macho wakati wanapopamba nywele zao. Kulingana na Dakt. Dean Ouano wa Chuo Kikuu cha Taasisi ya Macho ya Scheie ya Pennsylvania, hili “labda ndilo jeraha la moto lipatalo konea mara nyingi zaidi.” Uchunguzi mmoja waonyesha kwamba katika visa vilivyo vingi hakuna madhara ya muda mrefu kwa jicho, na katika visa vingi jicho lililochomwa hupona mnamo siku tatu. Hata hivyo, Dakt. Albert Cheskes wa Taasisi ya Macho ya Bochner katika Toronto aieleza namna hii ya aksidenti kuwa moja iwezayo kuwa “hatari sana.” Aongezea kwamba hiyo hutokea “kwa sababu kuna vyuma vingi zaidi na zaidi vya kukunja nywele vinavyotumiwa, na wanawake wanafanya haraka haraka.”

Uhalifu Katika Nyua za Shule

“Jeuri ya shuleni yachukiza, imeenea sana na inazidi haraka kuwa suala linalokabili waelimishaji na wanasiasa,” ladai The Toronto Star. Hesabu ya vitendo vya jeuri inaongezeka kadiri kila mwaka unavyopita. Katika 1993, uhalifu katika nyua za shule katika eneo la Toronto ulitia ndani mashambulizi 810, mashambulizi 131 ya kingono, na visa 7 vya kutiliwa sumu na pia mashtaka 141 ya kutumia silaha hatari. Polisi ‘wamekamata rundo kubwa kama bohari la bunduki, visu, vijiti, marungu na silaha nyinginezo kutoka kwa wanafunzi,’ laongezea Star. Wazazi wenye kuhangaika sana waziona shule kuwa mahali hatari pa kupeleka watoto wao. Shule zilikuwa kituo salama cha mafunzo zamani, “lakini sasa huko kuna magenge, vitisho kutoka kwa marika, silaha,” laripoti Star.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki