Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 11/22 kur. 13-15
  • Mitindo—Ina Uvutio Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mitindo—Ina Uvutio Gani?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Vijana na Mitindo Yao ya Mavazi
  • Tekinolojia ya Hali ya Juu Fashoni ya Hali ya Juu
  • Mitindo—Ya Kiajabu-Ajabu Tena Hatari
  • Mitindo—Ni Nini Kinachoitegemeza?
  • Mitindo—Je, Nifuate Halaiki?
    Amkeni!—1994
  • Usijiache Unaswe na Mitindo na Tafrija
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Madhara ya Sura Yenye Kuvutia
    Amkeni!—2003
  • Vijana—Kinzeni Roho ya Ulimwengu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 11/22 kur. 13-15

Vijana Huuliza...

Mitindo—Ina Uvutio Gani?

AVERY mchanga ni mmoja wa yale maelfu—labda mamilioni—ya vijana ambao wameathiriwa sana na ule mtindo upendwao sana wa kuvalia T-shati zenye maneno ya shime. Ni kweli, T-shati zenye maneno ya shime zimekuwapo kwa muda mrefu; hata huenda wazazi wako walizivalia wakiwa vijana. Hata hivyo, kulingana na gazeti Newsweek, kuna namna mpya katika mtindo huu. Baadhi ya vijana sasa “wanashaua T-shati zinazoonyesha maneno yaliyotolewa moja kwa moja kutoka hali ya utovu wa adabu.”

Shati mpya hizo hubeba maneno ambayo, mengi yayo kwa wazi hayapigiki chapa. Yaanza kwenye mitwezo ya kitaifa hadi maelezo yenye utovu wa adabu kuhusu wanawake. Wafuatao mtindo huu huelekea kutofikiria sana jinsi wengine—kutia ndani wazazi wao—wanavyohisi kuhusiana na hayo maneno machafu. Wakati Andrea mwenye miaka 18 alipomuuliza kijana mmoja kwa nini alivalia hasa shati yenye kuchukiza, “yeye hakujua la kusema, alitoa tu visababu kama, ‘Hii ni shwari’ na ‘Kila mtu huivalia.’”

Kwa miongo iliyopita, mamia ya mitindo imeteka uangalifu wa vijana. Mmoja wa mitindo ipendwayo na wengi zaidi ya yote—na yenye kuleta faida—ulikuwa Hula-Hoop uliopendwa sana katika Marekani huko nyuma katika miaka ya 1950. Rudi nyuma miaka michache mapema, na kumeza samaki-dhahabu akiwa hai na kuona ni watu wangapi wangetoshea katika kibanda cha simu yalipendwa na wengi. Katika miaka ya karibuni, kucheza breki-dansi, dangarizi zilizochujuka, mbao za kutelezea barafuni, na kukimbia-kimbia uchi hadharani yamepata muda wayo wa kupendwa na wengi. Mwandikaji mmoja wa Biblia alionelea hivi: “Tamasha ya ulimwengu huu inabadilika.” (1 Wakorintho 7:31, New World Translation) Leo, dazani za mitindo—kuanzia ya kipuuzi hadi iliyo hatari—imeenea miongoni mwa vijana.

Vijana na Mitindo Yao ya Mavazi

Kwa kielelezo, fikiria mavazi. Kulingana na gazeti Time, muziki wa rapu (uitwao hipu-hopu mara nyingi) “yawezekana ndiyo bidhaa ya Kimarekani yenye mafanikio zaidi sasa tangu kuvumbuliwa kwa kibanzi-elektroni au mikrochipu, ukienea, ukielekea kutawala, tamaduni za vijana ulimwenguni pote.” Lakini, kama ujuavyo vizuri, rapu ni zaidi ya muziki. Laongeza Time: “Rapu pia ni kifaa cha mtindo ulimwenguni pote. Tofauti ndogo-ndogo za mavazi katika mitaa ya Kimarekani—suruali zilizofura kama mifuko mikubwa, snika za bei, fulana zenye kifuniko cha kichwa, vito shaufu—yaonekana kila mahali.” Kuchochea kunakopita kiasi kwa vikundi vya kimuziki vipendwavyo na wengi—na kwa vidio za muziki—kumeongezea kutakwa sana kwa staili za hipu-hopu.

Mavazi hayo yaliyofura kama mifuko mikubwa si ya bei rahisi—vile viatu vifikavyo kwenye vifundo vya miguu mara nyingi hugharimu sana! Lakini vijana wengi wanahisi vyastahiki bei. Kulingana na kijana mmoja aitwaye Marcus, “ikiwa huvalii nguo kubwa-kubwa, wewe hauelewi hipu-hopu.”

Hiyo ni sawa tu kwa vijana ambao upendezi wao hauegemei kuelekea sura ya “kizembe” inayopendwa na wengi. Dangarizi zilizotatuka-tatuka na shati pana nene zinazoainisha mvalio huu wa kichaa ulienezwa kwa wengi na bendi za kichini-chini za Kimarekani za muziki wa roki. Mwandikaji mmoja aliita kivao hicho cha “uzembe” “umaskini uliosingiziwa.” Uliosingiziwa, kwelikweli. Vao hilo la kizembe si la gharama ndogo. Halafu kuna ile “staili ya kizamani.” Kulingana na gazeti la Kanada Maclean’s, hizi ni “staili zinazoamsha mitindo kutoka miaka ya mwisho-mwisho ya 1960 na ya mapema 1970.” Watu wazima hukodoa macho kwa mshangao wakati vijana wanalipa bei za juu kwa ajili ya mivalio—kama vile viatu vyenye soli nene na suruali zilizo pana sehemu ya chini—ambazo yaonekana zilikwisha kuwa za kizamani kama muziki wa disko.

Tekinolojia ya Hali ya Juu Fashoni ya Hali ya Juu

Vilia-bipu vya mfukoni vya kielektroni, ni kielelezo kingine cha jinsi vijana walio na mawazo mengi wanavyoelekea kugeuza chochote kile kuwa fashoni ya karibuni au ya hali ya juu. Vikitumiwa mwanzoni na madaktari na wenye ufundi wengine wanaohitajika daima, vifaa hivi vilikuja kupendwa na wachuuzi wa mijini wa dawa za kulevya. Vilia-bipu hivi vilifanya iwe rahisi kwa wauza madawa kupanga mikutano na wale ambao wangeweza kuwa wanunuzi. Kulingana na The New York Times, “matumizi yavyo yalikuwa na mweneo mkubwa sana hivi kwamba viliaji vya mfukoni vilikuja kuwa alama ya utamaduni wa dawa za kulevya.” Basi, si ajabu kwamba mabaraza ya shule taifani pote yalianza kupiga marufuku vifaa hivyo vidogo mno kutoka shuleni!Kwa faida ndogo, hata hivyo. Vilia-bipu vimekuwa vyenye kupendwa mno miongoni mwa vijana wa mijini. Baadhi yao huvitumia kwa makusudi yaliyonuiwa, kama vifaa vya uwasilianaji, vikiwezesha wazazi wao kufahamu walipo au kuwasiliana nao wakati wa dharura. Lakini kwa vijana wengine, kifaa hicho ni kiongezeo cha fashoni tu. Kulingana na Times, “matineja wanaweka vilia-bipu katika shanta, mifuko ya koti na mishipini. Kuna saa za mkononi ziliazo bipu, tai ziliazo bipu, kalamu ziliazo bipu, vilia-bipu vya samawati, vyekundu-vyeupe na vyekundu, na vilia-bipu vyeusi na vya kahawia vilivyo vikukuu na bila mapambo.” Ingawa watu wazima fulani bado wanahusianisha vilia-bipu na dawa za kulevya moja kwa moja, ofisa mmoja wa polisi wa New York City asema: “Ni kitu kiuzwacho sana. Wachache wa watoto walio navyo wanatumia dawa za kulevya, lakini wengi hawafanyi hivyo. Ni mtindo tu.”

Mitindo—Ya Kiajabu-Ajabu Tena Hatari

Ingawa huenda mitindo ya mavazi ikafikia kiasi cha kuvumilika au kiasi cha kuudhi, mitindo fulani ipendwayo na wengi huelekea kuvunja sheria zote za uamuzi timamu. Ili kupata umbo la wembamba la violezo fulani wapendwao na wengi, wasichana wengi wachanga hujiingiza katika ulaji wa kimtindo—pasipo kufikiria kwa uzito matokeo kwa afya na hali njema yao. “Kupunguza ulaji ni tamaa ya kitaifa isiyotulizika,” aandika Alvin Rosenbaum. “Ebu soma kwa uangalifu orodha ya vitabu 10 viuzwavyo kwa wingi zaidi na kwa kawaida utapata kitabu cha ulaji kimeorodheshwa.” Rosenbaum anataja kwamba vingi vya vitabu hivi vipendwavyo na wengi hutangaza ulaji usio na matokeo hakika. Wastadi wengi wanalaumu kile kichaa cha kuwa mwembamba kwa kupanda kunakoudhi kwa matatizo ya kula—kama vile anorexia nervosa—miongoni mwa matineja.a

Namna nyingine za kimtindo za kurembesha sura ya kibinafsi zaweza kuwa hatari—na vilevile za kiajabu. Kulingana na makala moja katika Newsweek, “kuchanja chale, ufundi wa wakale na waharamishwa kumekuwa kukisogea kikawaida kukawa fashoni kubwa.” Wakichochewa na mifano ya wacheza sinema maarufu na wanamuziki wa roki yenye mdundo mzito, vijana fulani hutamani chanjo zenye madoido zibandikwe daima katika viwiliwili vyao wenyewe. Maonyo ya madaktari kuhusu hatari za matokeo ya mchochota wa ini na ya kimizio kwa wino wa kuchanja chale yaonekana hayawatii wasiwasi wowote.

Au vipi ule mtindo wenye kuogofya uitwao utoboaji mwili? Ingawaje masikio yaliyotobolewa yaweza kuwa desturi kwa wanawake katika tamaduni fulani, wengine wamepita kiasi na kuruhusu ndimi na vitovu vyao vitobolewe na hivyo waning’inize vito vya kujionyesha. Kwa kijana yeyote aliyejitolea mhanga kuchukiza wazazi wake, kitu cha kuudhi zaidi kingekuwa pete kubwa ya puani.

Mitindo—Ni Nini Kinachoitegemeza?

Kitabu Adolescents and Youth hufasili mtindo kuwa “fashoni ya kipindi kifupi inayotokea mara kwa mara iliyo kama kufuata kidhehebu. Mitindo kwa ufasiri ni ya muda na isiyoelezeka kimbele, na huenea hasa miongoni mwa matineja.” Lakini ni nini hasa kinachofanya mamilioni ya vijana ghafula wavalie dangarizi zilizofura kama mifuko mikubwa au wabebe vilia-bipu? Wabuni na watangazaji bidhaa wangefurahia sana kupata jibu la kisayansi kwa swali hilo. Makala moja katika gazeti la Uingereza The Economist ilivyokiri: “Mitindo na fashoni yaonekana zinaasi kufikiri kwenye busara.”

Hata hivyo, kitabu Adolescents and Youth kinathubutu kutoa maelezo, kikisema: “Visababishi tofauti-tofauti vyaweza kueleza kwa nini mitindo inapendwa na wengi: ile tamaa ya kuvuta uangalifu; ule msukumo wa kukubaliana na yale vikundi vya marika huthamini; ule uhitaji wa watu kutambuliwa mmoja-mmoja na kama marika; na kule kusisimukia mambo yasiyo ya kawaida.” Tineja mmoja aliisahilisha hivi: “Shule ya sekondari ni wakati mzuri wa kutenda kama kichaa na kutosheleza tamaa hiyo ya ukichaa ili ikuondoke.”

Biblia hailaumu mwenendo wa ujana. Kwa kweli, hiyo husema: “Vijana, furahieni ujana wenu. Iweni na furaha mngali wachanga. Fanyeni mtakalo kufanya, na mfuate tamaa ya moyo wenu.” Hata hivyo, Biblia yafuatia shauri hilo kwa tahadhari hii: “Lakini ukumbuke kwamba Mungu atakuja kukuhukumu kwa lolote unalofanya.” (Mhubiri 11:9, Today’s English Version) Kulingana na shauri hili lenye busara, kijana Mkristo anapaswa kuitikiaje mitindo ya karibuni zaidi? Je! unapaswa kuwa wa kwanza kujiingiza katika mitindo ya halaiki? Makala yetu inayofuata katika mfululizo huu itatoa mashauri yenye msaada kuhusiana na mambo haya.

[Maelezo ya Chini]

a Kwa habari kuhusu matatizo ya kula, ona Amkeni! la Kiingereza la Desemba 22, 1990. Ona pia makala “Vijana Huuliza . . .” za Aprili 22 na Mei 8, 1994 kwa habari iliyosawazika juu ya kupunguza uzito.

[Blabu katika ukurasa wa 14]

“Shati hizi . . . Kila mtu anazivalia.” Avery mwenye miaka 17

[Picha katika ukurasa wa 15]

Utoboaji mwili na kuchanja chale kumekuja kupendwa na wengi sanay

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki