Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 12/22 kur. 10-11
  • Jinsi Angahewa Letu Litakavyookolewa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jinsi Angahewa Letu Litakavyookolewa
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Maandalizi ya Kulidumisha
  • Dunia Iliyosafishwa I Karibu
  • Angahewa Letu Linapoharibiwa
    Amkeni!—1994
  • Angahewa Letu Lenye Thamani
    Amkeni!—1994
  • Ngao za Dunia Zenye Nguvu
    Amkeni!—2009
  • Ah, Angalau Hewa Safi!
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 12/22 kur. 10-11

Jinsi Angahewa Letu Litakavyookolewa

JE, WANADAMU kwa hiari wataacha kujaza anga letu kwa uchafu? Je, angahewa letu litaokolewa kwa jinsi hii?

Katu. Kuokoa angahewa letu lenye thamani hakutegemei juu ya utii wa kibinadamu wa matakwa ya kupinga uchafuzi. Badala yake, mwingilio wa Mmoja yule anayemiliki mamlaka kuu ndio utakaoleta si angahewa lililosafishwa tu bali pia dunia iliyosafishwa.

Kwamba Muumba anajali dunia yetu, sawasawa na uhai uliopo juu yayo huonyeshwa na njia ya ajabu aliyoibuni. Aliifanya idumu kwa wakati usio dhahiri, hata milele.—Zaburi 104:5, 24.

Maandalizi ya Kulidumisha

Kwa kielelezo, lile angahewa, liliumbwa kwa njia ya kwamba laweza kujifanya upya na kujisafisha. Fikiria ile ozoni katika angahewa la juu. Ile ngao ya ozoni ilifanywa kiasili ili kwamba ifyonze mnururisho wa kiukaurujuani ambao ungekuwa hatari kwa wanadamu duniani. Wakati uleule, yakiruhusu mwangaza usio na madhara uhitajikao na uhai wa kidunia upite.

Mapema kidogo tulijifunza kwamba ngao ya ozoni inaharibiwa vibaya sana na klorofluorokaboni zilizotengenezwa na mwanadamu, ambazo hupaa kwenye angahewa la juu. Ngao linzi ya ozoni itarudishwaje upya? Kwa kustaajabisha, Muumba aliibuni ili kwamba ijirekebishe yenyewe upya. Naam, ozoni inaendelea kufanywa katika angahewa la juu—hakika, ozoni hujichuja kwa miali hiyohiyo hatari! Hivyo wakati uleule uchafuzi wa mwanadamu unapoiharibu ozoni kwa haraka, ozoni fulani inarekebishwa upya.

Hali inafanana katika angahewa la chini, ambapo nyingi zaidi ya zile tani kwadrilioni 5 za hewa yapatikana. Mfumo wa kiasili mara huisafisha hewa hii ya vichafuzi kwa njia yenye kupendeza. The World Book Encyclopedia yaeleza hivi: “Upepo hutapanya vichafuzi, na mvua na theluji huzisafisha hadi kwenye ardhi.”

Kwa wazi, basi, ikiwa wanadamu wangeacha kuchafua hewa, ama kupunguza uchafuaji kwa kiasi kikubwa, upesi hewa kila mahali ingekuwa safi na yenye kupendeza. Hata hivyo rejezeo lililo juu laonyesha tatizo, likieleza hivi: “Katika maeneo mengi, vichafuzi hutupwa hewani upesi sana kuliko vile hali za hewa ziwezavyo kuvibwaga.”

Basi, uchafuzi wenye ubinafsi wa mwanadamu wa angahewa utasimamishwaje?

Dunia Iliyosafishwa I Karibu

Uchafuzi utakomeshwa na Mungu mwenyewe tu, wakati atakapoingilia. Biblia hutabiri kwamba ‘atawaharibu hao waiharibuo dunia.’ (Ufunuo 11:18) Hataruhusu watu wenye pupa waendelee kuichafua dunia hii yenye urembo na angahewa lake lenye kuendeleza uhai. Aahidi hivi: “Watenda mabaya wataharibiwa, bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.”—Zaburi 37:9.

Waovu wote watafikiaje mwisho? Itakuwa kupitia serikali ya kimbingu ya Mungu, Ufalme wake, utakaochukua mahali pa serikali zilizopungukiwa za wanadamu. Biblia yaahidi hivi: “Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, . . . [nao ufalme wenyewe] utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.” (Danieli 2:44) Serikali hii ya Ufalme wa Mungu ndiyo ile ambayo Yesu alifunza wafuasi wake kuomba: “Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”—Mathayo 6:9, 10.

Mapenzi ya Mungu kwa dunia yetu ni kwamba wanadamu wapaswa kutawalwa na Ufalme wake na hivyo basi kufurahia maisha katika mazingira yasiyochafuliwa. Hiyo ndiyo sababu Mungu ameazimia “kuwaangamiza wale wanaoangamiza dunia.” (Ufunuo 11:18, Habari Njema kwa Watu Wote) Lo! huo utakuwa uokozi ulioje!

Wazia kuishi katika dunia isiyo na uchafuzi wote ambao wanadamu wenye ubinafsi wameirundikisha! Wakati huo angahewa letu lenye thamani litarudishwa katika hali yenye afya. Hili litatukia wakati ule unabii wa Biblia utakapotimizwa: “Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”—Ufunuo 21:3, 4; 2 Petro 3:13.

Ni lazima tufanye nini ili tuokoke tuingie katika ulimwengu mpya mwadilifu ambao Mungu aahidi? Wahitaji kujifunza kuhusu na kufuata mafundisho ya yule mmoja ambaye Mungu alimtuma duniani akiwa mwakilishi Wake. (Yohana 3:16; 7:29) Mmoja huyu, Yesu Kristo, alisema katika sala kwa Mungu: “Hii yamaanisha uhai udumuo milele, wao kuendelea kutwaa ujuzi juu yako wewe, Mungu pekee wa kweli, na juu ya yule uliyemtuma, Yesu Kristo.”—Yohana 17:3, New World Translation.

[Picha katika ukurasa wa 10]

Dunia-paradiso iliyo safi, isiyochafuliwa i karibu

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki