Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 1/8 uku. 25
  • Je, Si Sehemu ya Ulimwengu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Si Sehemu ya Ulimwengu?
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Dini Ilivyookoka Mashambulizi
    Amkeni!—2001
  • Kwa Nini Kanisa Linapoteza Uvutano?
    Amkeni!—1996
  • Ulaya Mashariki—Kufufuka Kidini?
    Amkeni!—1992
  • Kanisa La Kweli na Msingi Wake
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 1/8 uku. 25

Je, Si Sehemu ya Ulimwengu?

NA MLETA-HABARI ZA AMKENI! KATIKA UJERUMANI

“WAO si sehemu ya ulimwengu, kama vile mimi si sehemu ya ulimwengu.” (Yohana 17:16, NW) Kwa maneno haya Yesu alieleza kutokuwamo kamili kwa wafuasi wake kuelekea mambo ya kisiasa. Je, wadaio kuwa Wakristo leo hutimiza kiwango hiki?

Fikiria maelezo yanayofuata ya magazeti kuhusiana na mhusiko wa Jumuiya ya Wakristo katika ile iliyokuwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Ujerumani (GDR), ambayo hadi wakati wa kuvunjwa kwayo katika 1990 ilikuwa imesimamiwa na utawala wa Kikomunisti.

• “Kwa kuwa sasa Kanisa la Kilutheri katika GDR limeona fahari ya muda mfupi ya kuwa mwanzilishi wa yale mapinduzi yenye amani, heshima yalo mbele ya umma yaonekana ikididimia haraka sana. Kwa wengi laonekana limekuwa hasa nguzo ya kutegemeza utawala huo na kuwa uwanja wa kuendeshea Stasi (Huduma ya Usalama wa Serikali).”—Die Zeit, Novemba 1991.

• “Makanisa mbalimbali ya Kilutheri ya majimbo . . . yameeleza kuwa yametatanishwa fikira na mhusiko wa wafanyakazi na washiriki wa kanisa pamoja na Stas.”—Evangelische Kommentare, Januari 1991.

• “Viongozi wa Kanisa [wa Kilutheri] husikia malalamiko kwamba mapadri hawawatunzi tena watu wao kama walivyokuwa wakifanya zamani, kwa kuwa ni watendaji katika siasa.”—Süddeutsche Zeitung, Februari 1990.

• “Weizsäcker [aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Serikali ya Ujerumani] alisema kwamba Kanisa [la Kilutheri] lilikuwa sikuzote limeshiriki kusaidia katika uhusiano wa kisiasa wa zile Serikali mbili za Ujerumani.”—Wetterauer Zeitung, Februari 1992.

Mwingilio wa kisiasa kwa vyovyote haukufanywa na Kanisa la Kilutheri tu. “Karibu kila kikundi cha kanisa [la Kiprotestanti] kilipenywa na mawakili wa Stasi,” likaripoti The European. Manfred Stolpe, ambaye The European lamweleza kuwa “ndiye mshauriani mkuu wa kanisa la kiprotestanti pamoja na wenye mamlaka wakomunisti,” alisema hivi kwa kujitetea: “Kama jambo hilo lingaliendeleza lengo letu, ningalisalimiana na Ibilisi kwa mikono.”

Guardian la London liliripoti juu ya uhusiano wa karibu ulio kati ya makasisi na Mafia katika Italia. Lilitaarifu hivi: “Kanisa na Cosa Nostra wameingiliana kwa amani kwa muda mrefu sana hivi kwamba kanisa hushtakiwa mara nyingi juu ya kukubaliana nao.”

Toronto Star lilikuwa na makala juu ya ushirikiano wa mapadri fulani wa Orthodoksi ya Kirusi pamoja na ile iliyokuwa KGB (Halmashauri ya Usalama wa Serikali). Ripoti hiyo yataarifu hivi: “Mafunuo juu ya ushirikiano wa kanisa pamoja na utawala huo wa kikomunisti ndilo pigo lililo kali zaidi. . . . Habari za kutoka hifadhi za KGB . . . zadokeza kuwa si kwamba tu maofisa wakuu wa kanisa walisaliti kanuni zao wenyewe bali pia walikuwa tayari kuridhiana msimamo wa viongozi wa kidini kotekote.”

Ingawa makanisa ya Jumuiya ya Wakristo yaendelea kuingilia siasa, Ukristo wa kweli washikamana na agizo la Yesu la kutokuwa sehemu ya ulimwengu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki