Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 1/8 kur. 6-8
  • Ulaya Mashariki—Kufufuka Kidini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ulaya Mashariki—Kufufuka Kidini?
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Mambo Yamebadilika!
  • Mabadiliko Katika Albania
  • Mashahidi wa Yehova Katika Ulaya Mashariki
    Amkeni!—1992
  • Dini Yajiunga
    Amkeni!—1994
  • Kanisa Othodoksi la Kigiriki—Dini Iliyogawanyika
    Amkeni!—1996
  • ‘Na Ukuta Ukaanguka kwa Kishindo’
    Amkeni!—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 1/8 kur. 6-8

Ulaya Mashariki—Kufufuka Kidini?

KUZUIWA kwa uhuru wa usemi katika muda wa miongo mingi ya miaka iliyopita katika nchi za Ulaya Mashariki kumetia ndani vizuizi vizito kwa dini. Kutoamini juu ya kuwapo kwa Mungu kulihubiriwa kwa bidii, na makathidro na makanisa kadhaa yakageuzwa kuwa majumba ya maonyesho ya kutokuamini juu ya kuwapo kwa Mungu, kama lile linalotembelewa na watalii wengi katika Leningrad. Makasisi wowote wa wakati huo wakawa wasaidizi wa serikali iliyokuwa ikitawala wakati huo. Sehemu zote za ibada, kama vile nyumba za watawa, makanisa, na misikiti, zilifungwa kirasmi katika 1967, Albania hata ikitangazwa na Radio ya Tirana kuwa “Taifa la kwanza ulimwenguni ambalo haliamini kuwapo kwa Mungu.”

Sasa, huku uhuru ukichanuka kama maua ya wakati wa masika kila mahali katika Ulaya Mashariki, ni nini kinatukia kuhusu dini? Kama vile mwandikaji Mfaransa Jean-François Kahn alivyoandika: “Dini inayozuiwa yaweza kuungana mikono na taifa linalodhulumiwa. Ilitukia hivyo jana katika Iran. Inatukia hivyo leo katika sehemu ya Azerbaijan ya urusi. Kesho yaweza kuenea kotekote katika Urusi kama moto wa msitu.” Hata sasa baadhi ya dini zinajipatanisha na mawazo ya kitaifa na jitihada za uhuru na ndizo hasa zinazotoa malalamiko ya kisiasa, zikitakasa malalamiko hayo kwa kuwapo kwa mapadri wa Kikatoliki na wa Orthodoksi pamoja na mapasta wa Kilutheri.

Kwa hiyo uhuru wa kidini ukoje katika hali hiyo mpya ya kidemokrasi?

Jinsi Mambo Yamebadilika!

Dini zilizo kubwa katika Ulaya Mashariki, hasa Kanisa Katoliki, zimechukua hatua ya mara moja ili kupata utambulisho wa kisheria kutoka kwa serikali hizi mpya. Kwa mfano, L’Osservatore Romano liliripoti kwamba “mnamo Februari 9 [1990], mapatano yalifanywa kati ya Holy See (Mamlaka ya Papa) na Jamhuri ya Hungari.” Kwa mapatano hayo sehemu hizi mbili zilikubaliana kuanzisha upya mahusiano ya kibalozi. (Vatikani huonwa kama taifa lenye mamlaka lililo peke yake.)

Ripoti nyingine kutoka Vatikani yasema kwamba Kanisa Katoliki la Madhehebu ya Kiukrainia, lililokandamizwa katika 1946, limeuliza liweze kutambuliwa kisheria na limeingia katika mazungumzo “pamoja na Serikali na Kanisa la Urusi la Orthodoksi juu ya maswali yafaayo kuhusu maisha ya Kanisa katika Ukraine.”

Katika Aprili 1990 papa alizuru Chekoslovakia na alisalimiwa katika uwanja wa ndege wa Prague” na wakuu wa Kanisa na wa Taifa, kutia ndani. . . Bw. Vaclav Havel, Rais wa Jamhuri.” (L’Osservatore Romano) Hali mpya ya kidini inajitokeza huko pia.

Kanisa Katoliki limekuwa kila mara nguvu ipasayo kufikiriwa kwa uzito katika Polandi. Sasa, likiwa na uhuru mpya uliopatikana, linajikaza sana na kufanya kampeni ili kuanzisha mafunzo ya kidini shuleni. Padri mmoja alisema: “Shule ni mali ya taifa. Taifa la Polandi lina Wakatoliki zaidi ya asilimia 90. . . . Kukiwa na staha kwa dini nyinginezo, maagizo ya kidini shuleni yatarudisha mamlaka ya walimu, na . . . wenye mamlaka kwa sababu ndiyo yashughulikayo na msingi wa tabia njema za binadamu.”

Ripoti moja kutoka Romania juu ya Kanisa Orthodoksi lililo huko yasema: “Askofu Mkuu pamoja na baadhi ya maaskofu ambao walishirikiana na utawala wa [Ceauşescu] walilazimishwa kujiuzulu. Kamati ilianzishwa ili kulihuisha Kanisa. Wengi ambao hapo kwanza walikuwa wasioamini sasa wanageukia dini na kuyajaza makanisa ya kwao. . . Kanisa Katoliki la Byzantine Romania, lililolazimika kuvunjwa miaka 40 iliyopita, sasa limeruhusiwa kujitengeneza upya.”—Orthodox Unity, Julai 1990.

Mabadiliko Katika Albania

Kulingana na ripoti zilizochapishwa kwenye magazeti, mabadiliko ya kushangaza yanatukia pole kwa pole katika Albania, nchi ndogo yenye milima-milima ya wenyeji milioni tatu na robo, iliyobanwa katika Pwani ya Adriatiki kati ya Yugoslavia na Ugiriki. Gazeti la Ujerumani Die Welt liliripoti: “Katika Albania, ngome ya mwisho ya ukomunisti wa kizamani katika Ulaya, watu wameanza kupiga kura kwa miguu yao” kwa kutafuta kimbilio katika majumba ya kibalozi ya nchi za Magharibi, ambako baadaye waliruhusiwa kuondoka kuelekea Italia, Ujerumani, na nchi nyinginezo.

Ripoti hiyo yaendelea kusema: “Katika Mei 1990 Waalbania waliahidiwa pasipoti na pia kuondolewa kwa sheria zinazopiga marufuku kufuatilia mambo ya kidini.” (Imenukuliwa kutoka The German Tribune, Julai 15, 1990) Kama vile profesa wa historia Denis R. Janz alivyoandika: “Jitihada ya muda mrefu na ya jasho ya kutenga mambo ya kidini kwa ukamili yaonekana kuwa imewekwa kando.” Hata hivyo, yeye aongezea: “Kuna ushuhuda . . .kwamba dini imepigwa dharuba kali katika jamii hii.”

Katika hali hii Mashahidi wa Yehova wanadumisha kutokuwamo kwao kwa kawaida tena kwenye kushikiliwa sana. Kwa msingi wa kanuni za Biblia, wao hawajihusishi katika migawanyiko ya kisiasa au kitaifa. Wao wanamtumaini Mungu kuwapa hali za amani ambazo katika hizo wanaweza kutimiza agizo lao la kuhubiri duniani pote juu ya Ufalme wa Mungu.—Mathayo 22:21; 1 Timotheo 2:1, 2; 1 Petro 2:13-15.

Kwa hiyo, namna gani juu ya Mashahidi wa Yehova katika Ulaya Mashariki? Je, wamesitawi chini ya marufuku? Je, kuna uhuru wa kidini kwao?

[Picha katika ukurasa wa 7]

Je, watu watarudia makanisa ya Ulaya Mashariki?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki