Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 1/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Miezi Zaidi ya Sarateni Yavumbuliwa
  • Kuomba Radhi—Baada ya Miaka 50
  • Kanisa la Mormon Halikukinza Wanazi
  • Watoto Wasiotunzwa
  • “Kupata Lepe Ili Kupata Nguvu”
  • Kemikali za Shamba—Ni Tisho?
  • Mchwa Wenye Kumudu Joto Jingi
  • Komesheni Hiyo Kelele
  • Kupambana na Unyweaji wa Mifupa
  • Hangaiko Kuhusu Maradhi Yasababishwayo na Damu
  • Utiaji-damu Mishipani—Ni Salama Kadiri Gani?
    Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?
  • Je, Ni “Kana Kwamba Ilibuniwa”?
    Amkeni!—2005
  • Wadudu Wanaoondoa Takataka kwa Ustadi
    Amkeni!—2002
  • Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
    Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 1/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Miezi Zaidi ya Sarateni Yavumbuliwa

Picha zilizochukuliwa na Darubiniupeo ya Angani ya Hubble zimefunua angalau miezi miwili ikizunguka Sarateni ambayo haikujulikana hapo awali. Hizo picha zilichukuliwa wakati wa “Mpitano wa mizingo ya Sarateni na Dunia,” pindi ambayo ni adimu mno wakati Dunia inapokuwa na mwono wa kiupembe wa mizingo ya Sarateni. Chini ya hali hizi mwangaza mwangavu uwakiswao na hiyo mizingo huwa umepungua na hiyo miezi inaweza kuonekana kwa urahisi zaidi. Waastronomia wakadiria hiyo miezi kuwa na kipenyo cha kati ya kilometa 10 na kilometa 60. Miezi mipya iliyovumbuliwa huzunguka Sarateni kwenye umbali wa kilometa 140,000 hadi 150,000 kutoka kwenye kitovu cha hiyo sayari. Hii ni karibu mno kuliko zile kilometa 400,000 baina ya Dunia na mwezi wayo. Sarateni iko kilometa bilioni moja unusu hivi kutoka Dunia.

Kuomba Radhi—Baada ya Miaka 50

“Sisi hapa twaungama, zaidi ya yote mbele za Mungu, ile dhambi ya [Chuo Kikuu cha] Meiji Gakuin kwa kushiriki katika vita vya wakati uliopita na kwa wakati uleule kuomba radhi kwa watu wa nchi za kigeni, hasa wale wa Korea na China,” akasema mkuu wa chuo kikuu, Hiromasa Nakayama, katika mhadhara wake kwenye kanisa la hicho chuo kikuu katika Tokyo Juni uliopita. Chuo Kikuu cha Meiji Gakuin ni shule ya misheni ya “Kikristo.” Kulingana na gazeti la habari Asahi Shimbun, ilikuwa mara ya kwanza huyo mwakilishi wa shule kukiri hadharani kwamba shule ilishiriki katika harakati za vita. Wakati wa vita mwenyekiti wa baraza la wakurugenzi la chuo kikuu lilipanga United Church of Christ katika Japani ili kuunganisha makanisa kwa ajili ya jitihada za vita. United Church lilichangisha fedha ili kutokeza ndege za kivita na lilihimiza Wakristo kujitolea kwa hiari kwa nchi yao, Nakayama alisema.

Kanisa la Mormon Halikukinza Wanazi

Likikabili ripoti za jeuri kuelekea Wayahudi katika Ujerumani ya Nazi, “Kanisa la Mormon yaelekea halikufanya chochote,” lasema The Salt Lake Tribune. Baadhi ya Wamormon, pamoja na washiriki wa makanisa mengine, “walichukuliwa na Hitler na ujumbe wake wa usafi wa kijamii, na kuna wale ambao walifikiri kwamba walikuwa wakitii mafundisho yao ya kanisa ya kuheshimu viongozi wa serikali.” Wakati wa Teketezo la Umati kikundi cha Kijerumani cha Wamormon “kilifanya vile makanisa mengi yalivyofanya; viongozi hawakupinga,” akasema Profesa Franklin Littell wa Chuo Kikuu cha Temple, Philadelphia. Douglas Tobler, profesa wa historia kwenye Chuo Kikuu cha Brigham Young, ataka kuchunguza “kushindwa kwa makanisa kuchukua msimamo dhidi ya Unazi yakiwa makundi,” hilo gazeti likasema. Kwa kupendeza, Tribune lilionelea kwamba mwanahistoria John S. Conway, wa Chuo Kikuu cha British Columbia, Kanada, alisema kwamba tengenezo la kidini peke yalo ambalo lilikataa katakata kufuata Wanazi lilikuwa Mashahidi wa Yehova. Aliongezea kwamba kwa sababu ya msimamo huu zaidi ya nusu walipelekwa kwenye kambi za mateso.

Watoto Wasiotunzwa

Uchunguzi fulani wa kitaifa wa Australia ulifunua kwamba watoto walio wachanga kufikia miaka sita wanaachwa nyumbani peke yao huku wazazi wao wawili wakiwa kazini ama wakiwa nje na marafiki, laripoti The Canberra Times. Kulingana na Wendy Reid, msemaji mwanamke wa Boys Town National Community Projects, “zaidi ya nusu ya watoto walisema walikuwa wapweke na walikosa uandamani wa wazazi wao, huku asilimia kubwa ya wale wenye umri wa chini ya miaka 12 waliogopa—giza, radi, wajidukizaji, au kutekwa nyara.” Kwa kuongezea, Reid alisema kwamba “asilimia 71 ya [hao] watoto hawakuwa na mkakati wowote wa kufuatilia iwapo taabu ingezuka na kwamba nusu ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 12 hawakujua hata njia ya kuwasiliana na wazazi wao,” Times likaripoti.

“Kupata Lepe Ili Kupata Nguvu”

“Kupata lepe kwaweza kuboresha tabia-moyo, umakinifu na kufanya kazi,” laripoti The Wall Street Journal. Yale matokeo ya kupata nguvu upya kutokana na kupata lepe yamechochea baadhi ya viwanda kutafuta njia za kuingiza lepe katika siku ya kawaida ya kazi. Hili hasa ni kweli mahali ambapo ufikirio wa usalama huhusianishwa na umakinifu wa waajiriwa—kama vile waendesha-malori, marubani wa ndege, na waelekezi wa mitambo ya nyukilia. “Tumepata kwamba unapata tena umakinifu mwingi—wa kudumu saa nyingi—kutokana na lepe la dakika 15,” asema mtafiti wa usingizi Claudio Stampi. Lakini, kupata kibali cha waajiri kuhusu kupata lepe kazini kungali kuna mwendo mrefu. Journal lasema kwamba ili “kufanya kulala kazini kuwe kwenye kukubalika zaidi, wapendekezaji sasa wakurejezea kuwa ‘kupata lepe ili kupata nguvu.’”

Kemikali za Shamba—Ni Tisho?

Kemikali za kunyunyizia uga na bustani huenda zinahatarisha afya ya watoto wako, laripoti gazeti la maumbile ya asili Terre Sauvage, la Kifaransa. Hilo laonya kwamba “watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na minne wanaoishi katika makao ambapo bustani hupuliziwa viuamagugu au viuavisumbufu huwa katika hatari mara nne zaidi ya kuambukizwa na sarcoma, aina fulani ya kansa,” kuliko watoto ambao hawako mahali ambapo kuna kemikali kama hizo. Hiyo ripoti yaongezea kwamba utumizi wa viuawadudu katika mazingira ya mtoto huongeza hatari ya kupatwa na leukemia kwa mara moja unusu hadi mara tatu. Kwa kuwa zaidi ya nusu ya nyumba zote za Kifaransa hutumia kemikali za bustani, wengi huenda bila kujua wanafanyiza mazingira yenye sumu zaidi kwa watoto wao kuliko yale ya majiji makubwa ambayo yamechafuliwa.

Mchwa Wenye Kumudu Joto Jingi

Watafiti wawili katika Uswisi wamevumbua ni sababu gani mchwa fulani katika Jangwa la Sahara waweza kustahimili halijoto zenye kuchoma mno za digrii 60 Selsiasi. Rüdiger Wehner wa Taasisi ya Kizuolojia ya Chuo Kikuu cha Zurich na mtaalamu wa tabia za urithi Walter Gehring wa Chuo Kikuu cha Basel wamepata kwamba mchwa hufanyiza “dutu ziitwazo heat shock proteins (HSP), ambazo husaidia kulinda protini za mwili dhidi ya kuharibiwa na joto,” laripoti gazeti la Science. Wanapokuwa chini ya viwango vya halijoto vyenye kupita kiasi, “wanyama wote hutengeneza HSP baada ya uharibifu kuanza [kutokana na michomo ya joto],” hilo gazeti lasema, lakini “mchwa hujitengenezea hizo kimbele ili kujilinda.” Katika njia gani? Watafiti walipata kwamba mchwa huigiza michomo ya joto na kufanyiza HSP hata kabla ya kuacha makao yao. Aongezea Gehring: “Sisi hatukuwa werevu vya kutosha kufikiria hili, lakini mchwa walikuwa.” Au je, Muumba wao aliyekuwa mwerevu?

Komesheni Hiyo Kelele

“Tafadhali Komesheni Kelele Hiyo,” kikasihi kichwa kikuu katika gazeti la habari The Toronto Star. Kelele zisizoisha za jijini kutokana na vinyoashamba, vikusanya majani, vichimba mawe, honi na alamu za gari, kaseti plea zenye kuvuma, mbwa wenye kubweka, watoto wanaolia, na sherehe zenye kuchelewa mno usiku zimefanya vikundi vya kupinga kelele kufanya kampeini ya kupata amani na utulivu. Kuwa mahali penye kelele kama hizo kwa muda mrefu “kwaweza kuzidisha uchovu na wasiwasi,” lasema Star. Hilo laongezea hivi: “Utafiti wa kitiba huonyesha msongo wa damu waweza kupanda, kima cha moyo chaweza kubadilika na mwili hutokeza adrenalini na homoni nyinginezo ambazo huathiri mishipa ya damu.” Kulingana na mamlaka za afya, kuwa mahali penye sauti yoyote inayozidi decibels 85, kama vile kinyoashamba chenye kelele au pikipiki, kwa zaidi ya muda wa saa nane ni hatari kwa uwezo wako wa kusikia.

Kupambana na Unyweaji wa Mifupa

Utendaji wa kimwili waweza kuregesha uzito wa mifupa uliopotezwa kwa unyweaji wa mifupa, lasema gazeti la habari Jornal do Brasil. Wataalamu kwenye Kliniki ya Cotrauma katika Rio de Janeiro hutoa matibabu ya mazoezi lakini pia hufunza wagonjwa jinsi ya “kutembea vizuri na kuhodhi mkao sahihi.” Baada ya miaka miwili ya kufanya kazi pamoja na kikundi cha wanawake wenye umri wa kutoka miaka 45 hadi 77, asilimia 80 ya hicho kikundi kilikuwa kimeongeza sana uzito wa mifupa. Wakati huo wanawake walikuwa na maumivu kidogo zaidi ya mgongo kutokana na baridi yabisi, na hakuna yeyote aliyepatwa na mvunjiko wa mfupa. Dakt. Theo Cohen, mkurugenzi wa hiyo kliniki, apendekeza pia chakula ambacho kina kalsiamu nyingi na shahamu kidogo. Isitoshe, yeye huhimiza kutafuta kusudi maishani. “Hatutaki kuwaona walio wazee-wazee wakiwa wameketi na kufuma,” aonelea Dakt. Cohen. “Kutoka nje ili kutembea kidogo ni muhimu kama vile kufanya mchezo wa kujaza mafumbo ya maneno ili kuzoeza chembe za ubongo.”

Hangaiko Kuhusu Maradhi Yasababishwayo na Damu

Mbinu salama zaidi zinahitajiwa ili kulinda ugavi wa damu, kulingana na ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Matibabu ya U.S. National Academy of Sciences. Kama uthibitisho, hiyo ripoti yaonyesha ueneaji wa HIV (Human Immunodeficiency Virus) kupitia kwa utiaji-damu mishipani katika miaka ya mapema ya kipuku cha UKIMWI. Likipitia hiyo ripoti, The New York Times lilitaarifu: “Zaidi ya nusu ya watu 16,000 ambao hawatungami damu katika Marekani na wagonjwa zaidi ya 12,000 waliotiwa damu na vifanyizwa vya damu mishipani waliambukizwa H.I.V.” Ripoti ya taasisi yadhihirisha hangaiko kwamba viambukizaji hatari visivyojulikana kama vile HIV vingeweza tena kukumba mfumo wa afya wa kitaifa bila habari. Hiyo ilipendekeza kuweka mfumo fulani ili “kuchungua, kusimamia, na kutoa onyo kuhusu kuathiriwa vibaya kwa wapokezi wa damu na vifanyizwa vya damu.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki