Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 10/22 kur. 16-17
  • Akee—Chakula cha Kitaifa cha Jamaika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Akee—Chakula cha Kitaifa cha Jamaika
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mti Wenye Kuthaminiwa
  • Inapokuwa Hatari
  • Inazidi Kupendwa
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Chewa-Ulaya Wote Hao Walienda Wapi?
    Amkeni!—1997
  • ‘Fulizeni Kuzaa Matunda Mengi’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Habari Za Kitheokrasi
    Huduma Yetu ya Ufalme—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 10/22 kur. 16-17

Akee—Chakula cha Kitaifa cha Jamaika

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA JAMAIKA

NI ASUBUHI ya Jumapili katika kisiwa cha Jamaika katika Karibea. “Tunaandaa kiamsha-kinywa,” akatangaza mwenyeji mchangamfu kwa mgeni wake kutoka nchi ya kigeni.

“Naona kiamsha-kinywa kitakuwa mayai yaliyovurugwa,” mgeni akasema.

“La, hasha,” akajibu huyo mke-nyumbani, “hiyo ni akee na samaki aliyetiwa chumvi. Onja.”

“Ni tamu,” mgeni wake akajibu. “Lakini hakika inaonekana kama mayai yaliyovurugwa! Akee ni nini? Je, ni tunda au ni mboga?”

“Hilo ni swali ambalo huulizwa,” akajibu huyo mke-nyumbani. “Kibotania, akee huonwa kuwa tunda, lakini kama imepikwa, wengi huiona kuwa mboga.”

Ebu tukueleze mengi zaidi kuhusu akee.

Mti Wenye Kuthaminiwa

Mti wa akee ulitoka Afrika Magharibi. Kulingana na kitabu A-Z of Jamaican Heritage, cha Olive Senior, mimea ya kwanza ilifika Jamaika iliponunuliwa na nahodha mmoja wa meli ya watumwa katika karne ya 18. Wengine huamini kwamba jina akee limetokana na neno ankye la lugha ya Kitwi ya Ghana.

Miti ya akee ni mikubwa, ikifikia kimo cha meta 15 hivi. Miti hiyo inaweza kupatikana kotekote katika Jamaika, na matunda yayo huliwa na watu wa matabaka yote. Chakula kinachopikwa kwa akee huitwa kwa uchangamfu chakula cha kitaifa cha Jamaika. Mara nyingi akee huchanganywa na samaki chewa-ulaya, kutoka nchi za nje, katika mchuzi wa vitunguu, pilipili, na vikolezo vingine. Chewa-ulaya waliotiwa chumvi wasipopatikana, akee huliwa na samaki wengine au nyama au huliwa kavu.

Tunda bichi la mti wa akee ni lenye rangi ya kijani-kibichi, lakini linapoendelea kuwa bivu hilo hugeuka rangi na kuwa jekundu-jangavu. Linapokuwa bivu kabisa, tunda hupasuka na kuwa tayari kuchunwa. Tunda hilo lijifunguapo, vitu vitatu hujitokeza, kila kimoja kikiwa na mbegu nyeusi kwenye ncha yacho ya juu. Vitu hivyo vitatu vyenye rangi ya mtindi ndivyo sehemu ambazo huliwa baada ya mbegu nyeusi na kitu fulani chekundu kilichopo katikati ya vitu hivyo kutolewa.

Inapokuwa Hatari

Pindi kwa pindi kumekuwa na visa vya kudhuriwa—hasa kwa watoto—kwa sababu ya kula akee. Uchunguzi umetaja kisababishi kuwa kula tunda bichi. Utafiti umethibitisha kwamba kabla ya tunda kupasuka, hilo huwa na hypoglycin, ambayo ni aina ya amino asidi.

Wanabiokemia wamegundua kwamba hypoglycin huvuruga mmeng’enyo wa asidi za mafuta. Hilo laweza kusababisha kujaa kwa asidi nyingi za kikaboni katika damu, na kutokeza kizunguzungu na kuzirai. Hiyo hypoglycin pia huzuia kutengenezwa kwa glukosi ya damu, ambayo ni muhimu sana kwa mmeng’enyo wa chakula.

Uchunguzi waonyesha kwamba hypoglycin katika akee huyeyuka matunda yasiyopasuka yanapopikwa. Hivyo, maji ambamo akee imepikiwa yapaswa kumwagwa na hayapaswi kutumiwa kupika chakula kinginecho. Maonyo juu ya hatari ya kula au kupika akee mbichi yametolewa pindi kwa pindi na Idara ya Afya ya Umma.

Wapenzi wengi wa akee husema kwamba wao wameila maisha zao zote na hawajapata kudhuriwa nayo. Hivyo, wengine waweza kukana kwamba akee inaweza kuwa hatari.

Inazidi Kupendwa

Japo ripoti za mara kwa mara juu ya kudhuriwa na akee, akee na samaki waliotiwa chumvi inazidi kupendwa kikiwa chakula cha Jamaika. Lakini, desturi ya kula akee na samaki waliotiwa chumvi huenda ikaisha, kwa kuwa bei ya chewa-ulaya kutoka nchi za nje imeongezeka sana katika miaka ya majuzi. Lakini akee inaweza kupikwa na samaki wa aina nyinginezo na nyama, kwa hiyo wengi wa watu labda hawataacha kula chakula hiki cha kitaifa cha Jamaika.

Ikiwa upendezi wako kwa akee umechochewa, si lazima uzuru Jamaika ili uionje kwa sababu hiyo imekuwa chakula chenye kupelekwa sana nchi za nje. Ndiyo, akee huwekwa kwenye mikebe na kusafirishwa nchi nyinginezo, hasa nchi ambazo zina idadi kubwa za Wajamaika waliohamia huko. Basi, ukiona akee ya mikebe katika nchi yenu au ukizuru Jamaika, jaribu kula akee na samaki waliotiwa chumvi. Ni nani ajuaye? Huenda wewe pia ukapenda ladha yayo ya kipekee!

[Picha katika ukurasa wa 17

Tunda la mti wa “akee”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki