Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 11/8 uku. 31
  • Usidanganywe na Sura ya Nje

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Usidanganywe na Sura ya Nje
  • Amkeni!—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Wakati Ndege Wanapogonga Majengo
    Amkeni!—2009
  • Cock-of-the-Rock—Mrembo wa Msitu wa Amazon
    Amkeni!—1998
  • Fahamiana na Ndege Mwenye Kope
    Amkeni!—1998
  • Shomoro Aliyejeruhiwa Apata Makao Mapya
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 11/8 uku. 31

Usidanganywe na Sura ya Nje

TULIKUWA tunakaa katika nyumba yenye ustarehe ya rafiki iliyoko msituni, nasi tulilala katika orofa ya chini ya nyumba ambayo sehemu yake imejengwa chini ya ardhi. Hivyo, kwa ndani madirisha yalikuwa usawa wa macho na kwa nje usawa wa ardhi. Asubuhi ya kwanza, karibu saa 12, niliamshwa na sauti ya ajabu iliyokuwa ikipiga mara mbili-mbili ambayo ilielekea kutokea sehemu tofauti-tofauti za nyumba hiyo. Nikishangaa, nilisimama na kwenda jikoni ili kuona ikiwa friji au kipasha joto kilikuwa kinafanya kelele. Hamna chochote kati ya hivyo kilichofanya kelele. Nikiwa nimetatanishwa, kwa ghafula nilisikia sauti ikitokea chumba cha kupumzikia. Niliingia kwa ukimya, na kwa mshangao wangu, nje nilimwona ndege mwekundu sana, cardinal, akishambulia vioo vya dirisha! Aliruka haraka-haraka kutoka dirisha moja kwenda jingine kuzunguka nyumba—chumba cha kulala, chumba cha kuoga, chumba cha televisheni—popote ambapo kulikuwa na dirisha lililo usawa wa ardhi. Niliduwaa.

Niliposogelea karibu zaidi na dirisha, niligundua sababu ya fumbo hilo—kulikuwa na cardinal jike nje, umbali wa inchi chache tu, akiuma-uma mbegu kwa utulivu. Lakini kwa nini wa kiume alikuwa anashambulia vioo? Yaonekana, aliendelea kujiona kwenye kioo na kudhani ni cardinal mwingine mshindani naye alikuwa anajaribu kumtisha ili akimbie! Alidanganywa na sura ya nje.

Baadaye nilithibitisha kwamba hili lilikuwa kusudi la tabia ya ajabu ya ndege huyo. Katika kitabu chake The Cardinal, June Osborne aeleza kwamba cardinal wa kiume “hufanya jambo lolote liwezekanalo kuhakikisha kwamba eneo lake ni salama kutokana na wengine wa kiume wa spishi yake. . . . Yeye hawafukuzi tu wavamizi hao, bali amejulikana kupiga akisisho lake katika habu za magari, vioo vya magari, au vioo vikubwa vya madirisha na milango inayojongea ya vioo.” Kisha aongeza elezo fulani ambalo tulilikubali: “Hili laweza kuvuruga sana maisha ya amani ya mwenye nyumba.” Hilo tulijionea wenyewe, kila siku asubuhi.

Kitu gani kinaweza kufanywa kumzuia huyo wa kiume asiyejidhibiti? Mwandikaji Osborne ashauri: “Mara nyingine huwa lazima kufunika sehemu zenye kung’ara ili kurudisha amani na ukimya . . . , kwa kuongezea, hili litasaidia ndege huyo asijiumize mwenyewe katika mashambulio haya yanayokaribia kujiua.”—Imechangwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki