Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa 22. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Ni kupitia njia gani Mungu alimaliza uumbaji wa ulimwengu mzima wenye kuonekana? (Mwanzo 1:2)
2. Kupitia vimulikaji katika anga la mbingu, Yehova aliweka msingi wa nini? (Ona Mwanzo 1:14.)
3. Watumishi wa Senakeribu walitumaini kutimiza nini kwa kuongea kwa sauti kuu na katika lugha ya Wayahudi wenyewe kwenye ukuta wa Yerusalemu? (2 Mambo ya Nyakati 32:18)
4. Ni zana gani ya kilimo ambayo ilitumiwa katika nyakati za kale katika kuondoa magugu katika bara? (Isaya 7:25)
5. Kifuko kitakatifu ambacho kilikuwa kimetariziwa, chenye Urimu na Thumimu, ambacho kuhani mkuu alivaa juu ya moyo wake alipoingia Patakatifu kiliitwaje? (Kutoka 28:29, 30)
6. Kulingana na sheria ya Mungu, ni angalau mashahidi wangapi wanaotakikana ili kuthibitisha jambo? (Waebrania 10:28)
7. Mpiganaji Mwisraeli aliyemuua Lahmi, nduguye Goliathi, aliitwaje? (1 Mambo ya Nyakati 20:5)
8. Ni kuhani mkuu yupi aliyetoa amri ya kuuawa kwa Malkia mwovu Athalia? (2 Wafalme 11:15, 16)
9. Biblia yasema mtu apaswa kufanya nini na uso wa Yehova aombapo huruma yake? (Kutoka 32:11, NW)
10. Ni mwana yupi wa Yakobo mwenye jina linalomaanisha “Bahati Njema,” akiitwa hivyo kutokana na mshangao wa Lea wakati wa kuzaliwa kwake? (Mwanzo 30:11)
11. Ule mwinuko wa mwamba ambao juu yao Sulemani alijenga hekalu la Yehova unaitwaje? (2 Mambo ya Nyakati 3:1)
12. Jina la cheo cha Yesu, “Kristo,” lamaanisha nini? (Matendo 4:26, NW)
13. Yesu alisema ni lazima kufanya nini ili “kuingia katika mlango ulio mwembamba”? (Luka 13:24)
14. Kazi ya mwisho ya Mungu ya uumbaji wa kidunia inayoripotiwa katika Biblia inaitwaje? (Mwanzo 3:20)
15. Awali, Mungu alichanganuaje mioyo ya wanadamu? (Mwanzo 8:21)
16. Ni binti wa mfalme yupi wa Midiani aliyeuawa na Finehasi, ikimaliza pigo la Mungu juu ya Israeli? (Hesabu 25:15)
17. Ni kwa kutumia nini Mikali mke wa Daudi aliwahadaa watumishi ambao Sauli aliwatuma ili kumuua Daudi? (1 Samweli 19:11-16)
18. Malaika wa saba amwaga bakuli la hasira ya Mungu juu ya nini? (Ufunuo 16:17)
19. Ni jina gani linalotumiwa katika Biblia kutaja watu ambao si Waisraeli wa asili? (Ezra 10:2)
20. Ni mtu yupi wa ukoo wa Yuda, asiye na mwana, aliyetoa binti yake kwa mtumishi wake Yarha ili kuendeleza mstari wa ukoo wake? (1 Mambo ya Nyakati 2:34, 35)
21. Wakati wa kusafirisha sanduku la agano, ni kitu gani ambacho kilimsukuma Uza kunyoosha mkono na kulishika? (1 Mambo ya Nyakati 13:9, 10)
22. Ni simulizi gani la pekee la Biblia linaloshughulika kipekee na utume wa nabii fulani wa kutangaza ujumbe wa maangamizi kwa mji wa wasio-Waisraeli?
23. Ni jambo gani ambalo Mungu hawezi kufanya? (Waebrania 6:18)
24. Yehova atoapo baraka, ni kitu gani hachanganyi nayo? (Mithali 10:22)
25. Ni vitu gani ambavyo Daudi alivichukua kando ya kichwa cha Sauli alipokuwa analala, kuthibitisha kwamba asingemdhuru? (1 Samweli 26:12)
26. Yesu alifanya nini ili kuepuka kupigwa mawe? (Yohana 8:59)
Majibu ya Maswali
1. Kani yake ya utendaji
2. Kalenda
3. Kuwaogofisha na kuwafadhaisha
4. Jembe
5. Kifuko cha kifuani
6. Wawili
7. Elhanani
8. Yehoyada
9. Kuupoza
10. Gadi
11. Mlima Moria
12. Mtiwa Mafuta
13. ‘Kujitahidi’
14. Hawa
15. ‘Ni mbaya tangu ujana wake’
16. Suri
17. Kinyago na mto wa singa za mbuzi
18. Juu ya anga
19. Wageni
20. Sheshani
21. Ng’ombe walikunguwaa
22. Kitabu cha Yona
23. Kusema uwongo
24. Huzuni
25. Fumo na gudulia la maji
26. Alijificha