Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 9/22 uku. 11
  • Kulinda Afya ya Watoto

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kulinda Afya ya Watoto
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Jitihada Inayoendelea ya Kutafuta Suluhisho
    Amkeni!—2000
  • Jitihada za Kuwaokoa Watoto
    Amkeni!—1994
  • Uthibitisho wa Mafaa ya Maziwa ya Mama
    Amkeni!—1993
  • Kinachoamua Afya Yako—Lile Uwezalo Kufanya
    Amkeni!—1995
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 9/22 uku. 11

Kulinda Afya ya Watoto

RIPOTI moja ya juzijuzi iliyotolewa na Hazina ya Watoto ya Umoja wa Mataifa (UNICEF), The Progress of Nations, yaonyesha maendeleo makubwa katika hali za afya ya watoto wengi katika nchi nyingi. Kupitia juhudi za pamoja za serikali na mashirika ya kimataifa, idadi ya vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano imepungua katika nchi kadhaa. Hata hivyo, The Progress of Nations pia yaonyesha kuwa kila mwaka mamilioni zaidi ya uhai wa wachanga ungeokolewa kwa njia rahisi na zisizo ghali, hasa katika nchi zinazoendelea. Wazazi katika nchi hizi na kwingineko waweza kuona mapendekezo yafuatayo katika ripoti hiyo kuwa yenye msaada.

Kunyonyesha maziwa ya mama. “Kunyonyesha maziwa ya mama ndiko chanzo bora zaidi kwa afya na lishe bora,” ripoti hiyo yashauri. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), “uhai wa vitoto vichanga zaidi ya milioni 1 ungeweza kuokolewa kwa mwaka mmoja ikiwa watoto wote wachanga wangenyonyeshwa maziwa ya mama kikamili kwa angalau miezi sita ya kwanza.” Kwa kuwa hospitali na vituo vya uzazi huweka kielelezo chenye nguvu, UNICEF na WHO yanaendeleza “hali ya hospitali ya kushughulikia hali-njema ya mtoto.” Lengo lao ni kuchochea hospitali ziwape akina mama wa watoto waliotoka tu kuzaliwa utegemezo na mashauri mazuri kuhusu kunyonyesha maziwa ya mama.

Usafi wa kiafya na maji safi. “Wingi wa maradhi ungeweza kupunguzwa sana kwa kutumia maji safi, kwa kutumia vyoo, kwa kunawa mikono kabla ya kushika chakula, na kwa kutayarisha na kuweka chakula mahali salama,” ripoti hiyo yataarifu. Ingawa katika jamii nyingi ni vigumu kupata ya kutosha, maji safi ni ya lazima kwa afya ya mtoto na ya familia pia.

Lishe. Nyongeza ya vitamini-A yaweza kuzuia vifo vya watoto milioni tatu hivi kila mwaka, kulingana na ripoti hiyo. Suluhisho kwa tatizo hilo lipo na laweza kugharimikiwa, yasema, na yaweza kutimizwa kwa kuboresha milo, kuongezea ubora wa vyakula, au kugawanya vidonge vya vitamini-A. Kugawanya vidonge vya vitamini-A vya senti mbili za Marekani kila baada ya muda kwa watoto wachanga tayari kwatokeza matokeo mazuri katika nchi ambazo upungufu wa vitamini-A ni wa kawaida. Pia vyakula kama vile papai, maembe, karoti, mboga zenye majani ya kijani kibichi, na mayai, vilipendekezwa.

Tiba ya “Oral Rehydration.” Shirika la UNICEF lasema kuwa nusu ya vifo vya watoto kwa mwaka vinavyosababishwa na kuhara vingeweza kuzuiwa kwa msaada wa michanganyiko isiyo ghali na iliyo rahisi kutengenezwa ya maji safi, chumvi, na sukari au ungaunga wa mchele.a Wazazi pia wapaswa kuendelea kumpa mtoto chakula. Tayari, uhai upatao milioni moja unaokolewa kwa njia hii.

[Maelezo ya Chini]

a Kwa habari zaidi kuhusu kulinda afya ya watoto wako, tafadhali ona Amkeni!, Aprili 8, 1995, ukurasa wa 3-14.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 11]

WHO

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki