Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g02 12/8 uku. 31
  • Suluhisho la kelele nyingi mno

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Suluhisho la kelele nyingi mno
  • Amkeni!—2002
  • Habari Zinazolingana
  • Ninaweza Kuwa na Usawaziko Jinsi Gani Kuhusu Muziki?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Jihadhari na Muziki Unaovunja Heshima!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Ninaweza Kuwekaje Muziki Mahali Pao Panapofaa?
    Amkeni!—1993
  • Je, ni Muhimu Kuchunguza Aina ya Muziki Ninaosikiliza?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2002
g02 12/8 uku. 31

Suluhisho la kelele nyingi mno

“Ninafanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza vitu vya kuchezea vya watoto. Kwa kuwa tunafanya kazi ileile siku nenda siku rudi, wafanyakazi wanaruhusiwa kusikiliza muziki. Mmoja wa wafanyakazi wenzangu ambaye ana- fanya kazi karibu nami, hupenda kusikiliza muziki usiofaa. Wafanyakazi wengine wawili katika idara yetu hupenda muziki wa aina hiyo pia. Lakini kwa upande wangu, niliona ni mateso kusikiliza muziki huo kwa muda wa saa nane kila siku.

“Nilifikiria faida za kuendelea na kazi hiyo. Jambo moja ni kwamba msimamizi wangu sikuzote aliniruhusu kupata wakati wa kuhudhuria makusanyiko na mikutano ya pekee ya Mashahidi wa Yehova wanaofanya huduma ya wakati wote. Pia kazini si mbali, na kazi hiyo inaniwezesha kupata wakati wa kuhubiri.

“Niliongea na wafanyakazi wenzangu nikawauliza kwa upole kama wanaweza kubadili muziki wao au kupunguza sauti. Walienda kumlalamikia msimamizi. Msimamizi akaniita ofisini mwake. Akasema: ‘Sharon, huwezi kubadili kiwanda hiki kiwe dini yako. Wafanyakazi wetu wanaweza kusikiliza muziki wowote wanaotaka.’

“Kisha nikaomba kama naweza kuleta tepu-rekoda yangu mwenyewe na vifaa vya masikio. Akakubali. Nilileta kaseti za Mnara wa Mlinzi. Hiyo imenisaidia kuepuka kusikia muziki usiofaa. Kusikiliza kaseti hizo pia kumefanya niwe imara kiroho.”—Imesimuliwa na Sharon Quan.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki