Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g20 Na. 3 kur. 4-5
  • Pata Habari Sahihi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pata Habari Sahihi
  • Amkeni!—2020
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Tatizo
  • Kanuni ya Biblia
  • Kujua Ukweli Kunaweza Kutusaidiaje?
  • Mambo Unayoweza Kufanya
  • Ubaguzi—Je, Umekuathiri?
    Amkeni!—2020
  • Je, Wewe ni Mhasiriwa wa Ubaguzi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Ubaguzi Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Ubaguzi Utakwisha Lini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2020
g20 Na. 3 kur. 4-5
Wanaume wawili wakimhoji mwanamke anayetafuta kazi katika kiwanda cha kutengeneza magari. Mwanamke huyo anaonekana ana mkazo.

Pata Habari Sahihi

Tatizo

Mara nyingi watu huwabagua wengine kwa sababu ya kutokuwa na habari sahihi. Fikiria mifano ifuatayo:

  • Baadhi ya waajiri hufikiri kimakosa kwamba wanawake hawawezi kufanya kazi zinazohusiana na mambo ya kisayansi au teknolojia.

  • Huenda wageni wanaohamia nchi fulani wakabaguliwa kwa kudhaniwa watachukua kazi za wenyeji wa nchi hiyo.

  • Watu wengi huamini kimakosa kwamba kila mtu mwenye ulemavu ana huzuni au hasira.

Watu wanaoamini mambo hayo wanaweza kutafuta mifano au uthibitisho usiotegemeka ili kuunga mkono maoni yao. Na wanafikiri kwamba mtu yeyote anayepinga maoni hayo ni mjinga.

Kanuni ya Biblia

“Mtu asiye na ujuzi si mtu mzuri.”​—METHALI 19:2.

Kanuni hii inamaanisha nini? Tusipokuwa na habari sahihi tunaweza kufanya maamuzi yasiyofaa. Ikiwa tutaamini tu mambo ambayo wengine wanasema bila kujua ukweli, tutakuwa na maoni yasiyofaa kuhusu watu wengine.

Je, Biblia Inaunga Mkono Ubaguzi?

Baadhi ya watu wanadai kwamba Biblia inaunga mkono ubaguzi. Lakini Biblia inafundisha nini?

  • Wanadamu wote ni ndugu: Mungu “alifanyiza kila taifa la watu kutoka kwa mtu mmoja.”​—Matendo 17:26.

  • Mungu hana ubaguzi: “Mungu hana ubaguzi, lakini katika kila taifa mtu anayemwogopa na kutenda uadilifu anakubaliwa naye.”​—Matendo 10:34, 35.

  • Mungu huchunguza moyo wa mtu, si jinsi alivyo kwa nje: “Mwanadamu huona kinachoonekana kwa macho, lakini Yehova huona ndani ya moyo.”​—1 Samweli 16:7.a

a Yehova ni jina la Mungu kama linavyoonyeshwa katika Biblia.

Kujua Ukweli Kunaweza Kutusaidiaje?

Ikiwa tutakuwa na habari sahihi kuhusu watu fulani, inaelekea hatutaamini mambo ya uwongo yanayosemwa kuwahusu. Na tukijua kwamba habari tulizopata kuhusiana na watu fulani ni za uwongo, inaelekea tutafikiria kwa makini na kufanya utafiti kuhusu habari nyingine zozote ambazo tumesikia.

Simulizi: Jovica (Ulaya)

Jovica aliyenukuliwa kwenye makala iliyopita, alilelewa kwenye eneo ambalo vyombo vya habari vilieneza taarifa zisizofaa kuhusu watu wa jamii fulani. Alisema hivi: “Niliwabagua na hata kuwachukia watu hao. Nilihisi nina haki ya kufanya hivyo.

“Hata hivyo, nilipojiunga na jeshi, nililazimika kuishi na kufanya kazi na wanajeshi wenzangu kutoka kwenye jamii hiyo. Baada ya muda, nilijua mambo mengi kuwahusu. Hata nilianza kujifunza lugha yao na kusikiliza nyimbo zao za asili. Nilisitawisha uhusiano mzuri pamoja nao na maoni yangu kuwahusu yakaanza kubadilika. Lakini ninajua hisia za ubaguzi zinaweza kurudi tena. Hivyo, ninaepuka kusikiliza habari zozote mbaya kuhusu watu hao. Pia, ninaepuka kutazama filamu au vichekesho vinavyokusudiwa kuwakejeli. Ninajua kwamba hisia za ubaguzi zinaweza kusababisha hasira na chuki.”

Mambo Unayoweza Kufanya

  • Huenda wengine wakasema kwamba watu wa jamii fulani wana sifa mbaya, lakini kumbuka si wote katika jamii hiyo wana sifa mbaya.

  • Kumbuka kwamba huenda usiwe na habari kamili.

  • Jaribu kutafuta habari sahihi kutoka katika chanzo kinachoaminika.

Walishinda chuki

Collage: 1. Two men walk and talk to each other. 2. One of the men smiles in the company of friends.

Ni nini kilichomsaidia Mwarabu na Myahudi kushinda ubaguzi?

Tazama video Wakati Ambapo Upendo Mshikamanifu Utashinda Chuki. Tafuta video hiyo kwenye tovuti ya jw.org/sw.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki