Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g23 Na. 1 kur. 6-8
  • Bahari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Bahari
  • Amkeni!—2023
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kwa Nini Tunahitaji Kulinda Bahari Zetu
  • Dunia Yetu Imeumbwa Ikiwa na Uwezo wa Kuokoka
  • Hatua Zinazochukuliwa Sasa
  • Sababu za Kuwa na Tumaini—Biblia Inasema Nini
  • “Mali Nyingi ya Bahari”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2023
  • Ni Nini Kiwezacho Kufanywa ili Kuokoa Miamba ya Matumbawe?
    Amkeni!—1996
  • Binadamu Anaifanya Dunia Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2023
g23 Na. 1 kur. 6-8
Mzamiaji akiogelea baharini huku akiwa amezungukwa na samaki wenye rangi mbalimbali, matumbawe, na mimea ya baharini.

Georgette Douwma/​Stone via Getty Images

JE, DUNIA YETU ITAOKOKA?

BAHARI

BAHARI hutokeza chakula tunachokula na vitu tunavyohitaji ili kutengeneza dawa. Bahari zetu huzalisha zaidi ya nusu ya oksijeni iliyo duniani, na hufyonza gesi ya kaboni inayotokana na shughuli za wanadamu. Kwa kuongezea, bahari hudhibiti hali ya hewa.

Kwa Nini Tunahitaji Kulinda Bahari Zetu

Mabadiliko ya hali ya hewa huathiri matumbawe, samaki gamba, na viumbe wengine baharini. Wanasayansi wanatabiri kwamba karibu matumbawe yote—yanayotegemeza angalau robo ya viumbe wote wanaojulikana kuwa baharini—yako katika hatari ya kutoweka ndani ya miaka 30 ijayo.

Wataalamu wanakadiria kwamba karibu asilimia 90 ya ndege wanaopata chakula chao kutoka baharini, wamekula plastiki, na inasemekana kwamba kiwango cha plastiki kilicho baharini huua mamilioni ya viumbe baharini kila mwaka.

Katika mwaka wa 2022, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alisema hivi: “Tumeacha kuithamini bahari na leo tunakabili kile ambacho ninaweza kukiita kuwa ‘Hali ya Dharura Katika Bahari.’”

Dunia Yetu Imeumbwa Ikiwa na Uwezo wa Kuokoka

Bahari isipochafuliwa na wanadamu, ina uwezo wa kujisafisha na kudumisha uhai wa viumbe walio ndani yake. Kitabu Regeneration: Ending the Climate Crisis in One Generation kinasema kwamba bahari isipochafuliwa na viwanda vya wanadamu, “ina uwezo wa asili wa kujisafisha yenyewe.” Fikiria mifano michache:

  • Miani humeng’enya na kuhifadhi kaboni dioksidi—hewa inayoaminiwa kusababisha kuongezeka kwa joto duniani. Miani pekee huhifadhi kiwango cha kaboni dioksidi kinachokaribia kile kinachohifadhiwa na miti, majani, na mimea mingine inayopatikana duniani.

  • Bakteria hula samaki waliokufa ambao huenda wangeichafua bahari. Kisha bakteria hao huliwa na viumbe wengine wa baharini. Kulingana na Smithsonian Institution Ocean Portal, utaratibu huo “hudumisha bahari ikiwa safi na maridadi.”

  • Viumbe wengi wa baharini hutumia mifumo yao ya kumeng’enya ili kubadili maji ya bahari yenye asidi—yanayoathiri matumbawe, samaki gamba, na viumbe wengine —na kuwa maji ya chumvi yanayofaa.

    JE, WAJUA?

    Nyasi za Baharini Zinaendeleza Uhai

    Mchoro unaoonyesha mawimbi yanayokaribia ufuo. Sakafu, nyasi, na viumbe wa baharini wanaonekana. Mawimbi yanapokaribia ufuoni, nyasi hupunguza ukubwa na mwendo wa mawimbi na huondoa takataka katika maji. Samaki na viumbe wengine wa baharini huishi katika nyasi. Maji yanayofika ufuoni ni safi, na mawimbi yametulia zaidi.

    Nyasi zilizo ndani ya bahari hunasa mchanga na hivyo kuimarisha sakafu ya bahari. Hudumisha afya ya matumbawe na kulinda ufuo wa bahari kwa kupunguza ukubwa wa mawimbi na kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Hatua Zinazochukuliwa Sasa

Picha: 1. Mwanamume akitoa vitu alivyonunua kutoka kwenye mfuko anaoweza kutumia tena. 2. Mwanamke akijaza maji katika chupa anayoweza kutumia tena.

Tukitumia mifuko na chupa za maji tunazoweza kutumia zaidi ya mara moja, tunaweza kupunguza kiasi cha takataka za plastiki baharini

Takataka zisizoingia baharini hazihitaji kusafishwa. Hivyo, wataalamu wanawashauri watu kutumia tena mifuko, vifaa, na vyombo badala ya kutumia vifaa vya plastiki mara moja na kuvitupa.

Lakini jitihada zinahitajika. Hivi karibuni, kwa kipindi cha mwaka mmoja, shirika moja linaloshughulika na kutunza mazingira lilikusanya tani 9,200 za takataka zilizotupwa kwenye fuo za bahari katika nchi 112. Hata hivyo, hiyo ni asilimia ndogo sana ikilinganishwa na takataka zote zinazoingia baharini kila mwaka.

Gazeti la National Geographic liliripoti kwamba “kuongezeka kwa asidi [katika bahari] kulikotokea kufikia sasa huenda kusiweze kurekebishwa.” Linaendelea kusema, “wanadamu wanatumia mafuta mengi sana hivi kwamba viumbe wa baharini hawawezi kudumisha bahari zikiwa safi kama walivyofanya zamani.”

Sababu za Kuwa na Tumaini—Biblia Inasema Nini

“Dunia imejaa vitu ulivyoumba. Kisha kuna bahari, ni kubwa sana na pana, imejaa viumbe walio hai wasio na idadi, wadogo kwa wakubwa.” —Zaburi 104:​24, 25.

Muumba wetu ameumba bahari na uwezo wake wa kujisafisha. Fikiria hili: Ikiwa anajua mambo yote kuhusu bahari na viumbe walio ndani yake, bila shaka anaweza kurekebisha madhara yanayosababishwa na wanadamu. Ona makala yenye kichwa “Mungu Anaahidi Kwamba Dunia Yetu Itaokoka,” katika ukurasa wa 15.

JIFUNZE MENGI ZAIDI

Nyangumi wanaoitwa Pilot wakiogelea baharini.

Blue Planet Archive/​Doug Perrine

Wanasayansi wamejifunza kutoka kwa samaki jinsi ya kusafisha chaza wadogo kutoka kwenye meli kubwa bila kutumia kemikali zenye sumu. Soma makala “Uwezo wa Kujisafisha wa Ngozi ya Nyangumi Anayeitwa Pilot” katika jw.org/sw.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki