Ukristo Waenea Katika Nchi Nyingine
AKIWA katika Mlima wa Mizeituni karibu na Bethania, Yesu aliagiza kazi ya kuhubiri ifanywe. Kazi hiyo ingebadili historia ya ulimwengu. Ingeanzia Yerusalemu, eneo lililokuwa karibu kilometa tatu magharibi ya mlima huo. Ujumbe huo ungeenezwa hadi Yudea na Samaria, maeneo yaliyokuwa karibu na Yerusalemu, na hatimaye kufikia “sehemu ya mbali zaidi ya dunia.”—Mdo 1:4, 8, 12.
Muda mfupi baada ya Yesu kusema maneno hayo, Wayahudi na wageuzwa-imani kutoka sehemu mbalimbali za Milki ya Roma ambazo zimeonyeshwa katika ramani iliyo hapa chini, walikusanyika kwa ajili ya Sikukuu ya Pentekoste. Mahubiri ya mtume Petro siku hiyo yalifanya Ukristo uenee haraka.—Mdo 2:9-11.
Punde si punde, mnyanyaso uliotokea Yerusalemu uliwatawanya wafuasi wa Kristo. Petro na Yohana waliwasaidia Wasamaria kusikia na kukubali habari njema. (Mdo 8:1, 4, 14-16) Baada ya Filipo kumhubiria Mwethiopia kwenye barabara ya jangwani ‘iliyotoka Yerusalemu hadi Gaza,’ Ukristo ulienea Afrika. (Mdo 8:26-39) Wakati huohuo, ujumbe huo ulikuwa na matokeo huko Lida, jiji lililokuwa kwenye Nchi Tambarare ya Sharoni, na kwenye bandari ya Yopa. (Mdo 9:35, 42) Baada ya hapo, Petro alienda Kaisaria na akamsaidia Kornelio, afisa wa jeshi la Roma, pamoja na jamaa zake na marafiki wake kuwa Wakristo waliotiwa mafuta kwa roho.—Mdo 10:1-48.
Paulo, ambaye hapo awali aliwanyanyasa Wakristo, akawa mtume kwa mataifa. Katika safari zake tatu za umishonari, na alipoelekea Roma, alisafiri kwa meli na pia kupitia nchi kavu. Mitume na watu wengine walieneza habari njema kwenye miji yenye watu wengi katika Milki ya Roma. Paulo alitamani sana kufika Uhispania (Ona ukurasa wa 2.), naye Petro alitumikia maeneo ya mashariki kama vile Kristo, wafuasi wake walieneza Ukristo katika nchi Babiloni. (1Pe 5:13) Kwa kweli, chini ya uongozi wa nyingine. Kufikia mwaka wa 60/61 W.K., ‘habari njema ilikuwa imehubiriwa katika uumbaji wote ulio chini ya mbingu.’ (Kol 1:6, 23) Tangu wakati huo, habari njema zimehubiriwa “mpaka sehemu ya mbali zaidi ya dunia.”
[Sanduku katika ukurasa wa 32]
WALITOKA . . .
Wayahudi na wageuzwa-imani waliosikia habari njema siku ya Pentekoste mwaka wa 33 W.K. walitoka Parthia, Umedi, Elamu, Mesopotamia, Yudea, Kapadokia, Ponto, Asia, Frigia, Pamfilia, Misri, Libya, Roma, Krete, na Arabia. Wengi walibatizwa. Unafikiri walifanya nini waliporudi makwao?
[Sanduku katika ukurasa wa 33]
MAKUTANIKO SABA
Yesu alituma ujumbe kwa makutaniko saba huko Asia Ndogo. Ona mahali yalipokuwa: Efeso na Smirna yalikuwa pwani; Pergamamu, Filadelfia, na Laodikia yalikuwa bara; Thiatira lilikuwa kando ya mto; na Sardi lilikuwa kwenye barabara muhimu iliyotumiwa na wafanyabiashara. Magofu yaliyofukuliwa ya majiji hayo yanathibitisha kwamba sehemu hizo zinazotajwa katika Biblia ni halisi.
[Ramani katika ukurasa wa 32]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Ogozeko ya Ukristo
Maeneo Ambayo Yalifikiwa kwa Uharaka na Habari Njema
B1 ILIRIKAMU
B1 ITALIA
B1 Roma
C1 MAKEDONIA
C2 UGIRIKI
C2 Athene
C2 KRETE
C3 Kirene
C3 LIBYA
D1 BITHINIA
D2 GALATIA
D2 ASIA
D2 FRIGIA
D2 PAMFILIA
D2 SAIPRASI
D3 MISRI
D4 ETHIOPIA
E1 PONTO
E2 KAPADOKIA
E2 KILIKIA
E2 MESOPOTAMIA
E2 SIRIA
E3 SAMARIA
E3 Yerusalemu
E3 YUDEA
F2 UMEDI
F3 Babiloni
F3 ELAMU
F4 ARABIA
G2 PARITHIA
[Bahari na Ziwa]
C2 Bahari ya Mediterania
D1 Bahari Nyeusi
E4 Bahari Nyekundu
F3 Ghuba ya Uajemi
[Ramani katika ukurasa wa 32, 33]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
Safari Za Paulo
Safari ya Kwanza ya Umishonari (Mdo 13:1–14:28)
H3 Antiokia (ya Siria)
H3 Seleukia
G4 SAIPRASI
G3 Salamisi
G4 Pafosi
G3 PAMFILIA
F3 Perga
F3 PISIDIA
F2 Antiokia (ya Pisidia)
G2 Ikoniamu
G2 LIKAONIA
G2 Listra
G3 Derbe
G2 Listra
G2 Ikoniamu
F2 Antiokia (ya Pisidia)
F3 PISIDIA
G3 PAMFILIA
F3 Perga
F3 Atalia
H3 Antiokia (ya Siria)
Safari ya Pili ya Umishonari (Mdo 15:36–18:22)
H3 Antiokia (ya Siria)
H3 SIRIA
H3 KILIKIA
H3 Tarso
G3 Derbe
G2 Listra
G2 Ikoniamu
F2 Antiokia (ya Pisidia)
F2 FRIGIA
G2 GALATIA
E2 MISIA
E2 Troasi
E1 SAMOTHRAKE
D1 Neapolisi
D1 Filipi
C1 MAKEDONIA
D1 Amfipoli
D1 Thesalonike
D1 Berea
C2 UGIRIKI
D2 Athene
D2 Korintho
D3 AKAYA
E2 Efeso
G4 Kaisaria
H5 Yerusalemu
H3 Antiokia (ya Siria)
Safari ya Tatu ya Umishonari (Mdo 18:22–21:19)
H3 SIRIA
H3 Antiokia (ya Siria)
G2 GALATIA
F2 FRIGIA
H3 KILIKIA
H3 Tarso
G3 Derbe
G2 Listra
G2 Ikoniamu
F2 Antiokia (ya Pisidia)
E2 Efeso
E2 ASIA
E2 Troasi
D1 Filipi
C1 MAKEDONIA
D1 Amfipoli
D1 Thesalonike
D1 Berea
C2 UGIRIKI
D2 Athene
D2 Korintho
D1 Berea
D1 Thesalonike
D1 Amfipoli
D1 Filipi
E2 Troasi
E2 Asosi
E2 Mitilene
E2 KIOSI
E2 SAMOSI
E3 Mileto
E3 Kosi
E3 RODESI
F3 Patara
H4 Tiro
H4 Tolemai
G4 Kaisaria
H5 Yerusalemu
Safari ya Kwenda Roma (Mdo 23:11–28:31)
H5 Yerusalemu
G4 Kaisaria
H4 Sidoni
F3 Mira
F3 LIKIA
E3 Kinido
D3 KRETE
D4 KAUDA
A3 MALTA
A3 SICILY
A3 Sirakusi
A1 ITALIA
B2 Regiamu
A1 Puteoli
A1 Roma
Barabara Kuu (Ona kichapo)
Makutaniko Saba
E2 Pergamamu
E2 Thiatira
E2 Sardi
E2 Smirna
E2 Efeso
F2 Filadelfia
F2 Laodikia
[Mahali pengine]
E3 PATMO
F2 Kolosai
F5 Aleksandria
F5 MISRI
G1 BITHINIA
G5 Yopa
G5 Lida
G5 Gaza
H1 PONTO
H2 KAPADOKIA
H4 Damasko
H4 Pella
[Bahari na Ziwa]
D4 Bahari ya Mediterania
[Picha katika ukurasa wa 33]
Jumba la maonyesho huko Mileto, ambako Paulo alikutana na wazee kutoka Efeso
[Picha katika ukurasa wa 33]
Madhabahu ya Zeusi huko Pergamamu. Wakristo katika jiji hili waliishi ‘mahali kiti cha ufalme cha Shetani kilipokuwa’—Ufu 2:13