Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • lfb somo la 79 uku. 186-uku. 187 fu. 2
  • Yesu Anafanya Miujiza Mingi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Anafanya Miujiza Mingi
  • Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Anafufua Wafu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Tunaweza Kufufuliwa!
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Machozi Yakabadilika Kuwa Pindi Yenye Furaha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Watoto Wafufuliwa kwa Wafu
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
Pata Habari Zaidi
Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
lfb somo la 79 uku. 186-uku. 187 fu. 2
Wagonjwa wakija kwa Yesu ili waponywe

SOMO LA 79

Yesu Anafanya Miujiza Mingi

Yesu alikuja duniani kutangaza habari njema ya Ufalme wa Mungu. Ili kuonyesha mambo ambayo Yesu atatimiza akiwa Mfalme, Yehova alimpa roho takatifu ili afanye miujiza. Angeweza kuponya ugonjwa wowote. Popote alipoenda wagonjwa walimwendea ili awasaidie, naye akawaponya wote. Vipofu waliona, viziwi wakasikia, vilema wakatembea, na wale waliosumbuliwa na roho waovu wakawekwa huru. Waliponywa hata walipogusa tu upindo wa vazi lake. Watu walimfuata Yesu popote alipoenda. Hata alipotaka kuwa peke yake, kamwe Yesu hakumfukuza mtu yeyote.

Pindi moja, watu walimleta mwanamume aliyekuwa amepooza katika nyumba ambayo Yesu alikuwa akiishi. Lakini nyumba hiyo ilikuwa imejaa sana hivi kwamba hawangeweza kumwingiza ndani. Kwa hiyo, wakatoboa tundu kwenye paa na kumshusha mwanamume huyo kwa Yesu. Kisha Yesu akamwambia mwanamume huyo: ‘Simama utembee.’ Aliposimama, watu walishangaa sana.

Pindi nyingine, Yesu alipokuwa akiingia katika kijiji fulani, wanaume kumi waliokuwa na ukoma walisimama mbali na kumwambia Yesu kwa sauti kubwa: ‘Yesu, tusaidie!’ Katika siku hizo, watu wenye ukoma hawakuruhusiwa kuwakaribia watu wengine. Yesu akawaambia wanaume hao waende hekaluni, kama Sheria ya Yehova ilivyosema kwamba watu wenye ukoma wanapaswa kwenda hekaluni baada ya kuponywa. Walipokuwa njiani, wakaponywa. Mmoja wao alipotambua kwamba ameponywa, alirudi kumshukuru Yesu na kumsifu Mungu. Kati ya wanaume wote kumi, ni huyo mmoja tu aliyemshukuru Yesu.

Mwanamke ambaye alikuwa mgonjwa kwa miaka 12 alitamani sana kuponywa. Alikuja nyuma ya Yesu akiwa katikati ya umati na kugusa upindo wa vazi lake la nje. Mara moja, akaponywa. Hilo lilipotukia, Yesu akauliza: “Ni nani aliyenigusa?” Ingawa mwanamke huyo aliogopa sana, alijitokeza na kumwambia ukweli. Yesu alimfariji kwa kumwambia: ‘Binti yangu, nenda kwa amani.’

Ofisa anayeitwa Yairo alimsihi Yesu hivi: ‘Njoo nyumbani kwangu! Binti yangu ni mgonjwa sana.’ Lakini kabla ya Yesu kufika nyumbani kwa Yairo, yule msichana akafa. Yesu alipofika, aliona watu wengi waliokuja kuomboleza na familia hiyo. Yesu akawaambia: ‘Msilie; msichana huyu amelala tu.’ Kisha akamshika msichana huyo mkono na kusema: “Msichana, inuka!” Yule msichana akainuka mara moja, na Yesu akawaambia wazazi wake wampe chakula. Hebu wazia jinsi wazazi hao walivyohisi!

Yesu akimfufua binti ya Yairo

“Mungu [alimtia] mafuta kwa roho takatifu na nguvu, naye akapita katika nchi akitenda mema na kuwaponya wote waliokandamizwa na Ibilisi, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.”​—Matendo 10:38

Maswali: Kwa nini Yesu alikuwa na uwezo wa kuponya magonjwa ya aina zote? Ni nini kilichompata binti ya Yairo?

Mathayo 9:18-26; 14:36; Marko 2:1-12; 5:21-43; 6:55, 56; Luka 6:19; 8:41-56; 17:11-19

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki