Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 8/1 kur. 351-355
  • Je! Serikali Yaweza Kuwa Huru na Upotovu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Serikali Yaweza Kuwa Huru na Upotovu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • AGANO LA SERIKALI ISIYOPOTOKA
  • MTAWALA ASIYEPOTOKA ATOKEZWA
  • MTAWALA ALIYEJARIBIWA NA KUHAKIKISHWA
  • Serikali ya Mungu ya Amani
    Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani
  • Namna Ufalme wa Mungu Unavyoweza Kukufaidi Wewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Ufalme wa Mungu
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Serikali ya Mungu—Tumaini Pekee La Wanadamu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 8/1 kur. 351-355

Je! Serikali Yaweza Kuwa Huru na Upotovu?

Makala hii ni ya kutumia kwa mafunzo ya kitabu ya kundi

“Wenye haki wakiwa na amri, watu hufurahi.”​—Mit. 29:2, AV.

1-3. Watu wanaonaje serikali leo?

JE! WEWE waonaje serikali? Watu katika nchi mbalimbali wameonyesha uchungu mwingi na shuku juu ya watawala. Wengi wanaviacha vyama vikubwa vikubwa vya kisiasa. Wengine wanakuwa wenye kujitegemea wenyewe au kujiunga na chama kipya, huku wengine wakijitenga na siasa kabisa. Wengine wanaona kwamba kusihi wenzao wagomee kazi na kufanya maandamano kutaleta badiliko fulani.

2 Si kwamba watu wanaepa serikali peke yake. Wanawaonea shuku wale waliomo katika vyeo vya serikali. Nia hii inaonyeshwa sana na watu ulimwenguni mwote, zaidi katika nchi ambako watu wanaruhusiwa kuzungumza juu ya mambo ya serikali.

3 Upotovu kwa upande wa watawala umemfanya Arnold A. Hutschnecker, tabibu na mwandishi, apendekeze kwamba “wagombea uchaguzi, kabla hawajaruhusiwa waingie katika shindano la kisiasa, inawapasa waangaliwe na baraza ya madaktari na matabibu wa akili kuhakikisha kwamba ni wenye afya akilini na mwilini.”

4. Kwa sababu gani hapana mwanadamu wala baraza ya wanadamu iwezayo kutawala wanadamu ifaavyo?

4 Karibu kila mtu anakubali kwamba serikali ya namna fulani yahitajiwa. Lakini utawala wa watu wenye ghasia na mchafuko wa utawala ndio usiotamanika. Lakini furaha ya watu inategemea sana ukamilifu na uwezo wa wale waliomo katika vyeo vya utawala. Na, kwa habari yao wenyewe, hapana mwanadamu wala baraza ya wanadamu yenye uwezo wa kutawala kwa njia ya haki kabisa. Wanadamu wote ni wasiokamilika na kwa hiyo wako chini ya mikazo na vishawishi hivyo kwamba hawawezi kwa nguvu zao wenyewe kupinga wakipewa mamlaka watawale mwanadamu mwenzao. Mtu ambaye alikuwa mfalme na mchunguzi sana wa serikali alisema juu ya misiba iliyokuwa imetokea “wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasara yake.”​—Mhu. 8:9.

5, 6. N’nani peke yake awezaye kutokeza serikali itamanikayo, na je! ana nia ya kufanya hivyo?

5 Kwa hiyo, lazima utawala utoke katika chanzo kilicho juu zaidi ya mwanadamu. Ni Muumba peke yake awezaye kutunga sheria zenye kufanya kazi kwa usawa na inavyofaa kwa faida ya wote, kisha anaweza kuzifikiliza kwa ukamili na kwa njia isiyo ya upendeleo. Yeye peke yake ndiye anayejua mwanadamu alivyofanyizwa na mambo anayoyahitaji apate furaha. Lakini je! Muumba anayo nia ya kuleta serikali kama hiyo? Je! anakusudia kufanya hivyo?

6 Ndiyo, anataka. Yeye amekwisha kuikusudia na akamchagua mtawala asiyepotoka. Je! twaweza kuwa na hakika kwamba uchaguzi wake unafaa? Je! twaweza kumwamini na kumtumaini yeye aliyewekwa naye, kwamba mtawala huyu ataiendeleza serikali yake kuwa huru na upotovu? Ni faida kwetu kuchunguza kwa uangalifu, tupate uhakikisho na uongozi.

AGANO LA SERIKALI ISIYOPOTOKA

7-9. (a) Kwa sababu gani umepita muda mwingi sana tangu Mungu alipofanya agano la ufalme, na hali dunia ingali chini ya utawala wa mwanadamu? (b) Kwa sababu gani Mungu alisimamisha ufalme wa kidunia na taifa moja?

7 Mungu amekwisha fanya agano la kifalme, agizo, la serikali hiyo. Alifanya hivi zamani sana na mfalme aliyemchagua mwenyewe. Kwa sababu gani agano hili likafanywa zamani sana, na hali wanadamu hawajapata kuona utawala mkamilifu hata kidogo?

8 Mungu alilifanya agano hili wakati huo wa zamani kwa faida yetu. Kwa njia hiyo aliruhusu wakati ili matukio yapate kuonekana ambayo yangetuwezesha sisi tuone kushindwa kwa serikali zilizoundwa na mwanadamu nasi tupate kuchagua kwa busara namna ya serikali tunayotaka kutumikia. Twaweza kusadiki kwamba inawezekana kwetu kuitumaini serikali ambayo Mungu anakusudia. Ebu na tuangalie yale ambayo agano hili la maana linatoa na kuahidi.

9 Wakati ambapo Mungu alifanya agano hili la serikali juu ya dunia, yeye alikuwa amekwisha fanya taifa la Israeli kama watu waitwao kwa jina lake. Aliusimamisha ufalme wake wa kidunia juu ya taifa hilo, siyo kwa sababu ya upendeleo, bali kusudi awafunulie wanadamu njia yake ya kutenda na namna ya serikali anayokusudia. Ufalme huo ulikuwa wa mfano tu. Kwa namna ambavyo Mungu alishughulika nao, sisi twaweza kuwa na msingi wa kuiamini serikali ya Mungu ya dunia yote.​—Kum. 4:5-8; Zab. 67:1-7.

10-12. (a) Kwa sababu gani Mungu akamchagua Daudi kama mtu ambaye angefanya naye agano lake la ufalme? (b) Agano hilo liliahidi nini, na je! Mungu aliliacha wakati wo wote?

10 Yehova Mungu alilifanya agano la ufalme na mwanamume aliyeitwa Daudi, mfalme wa Israeli wa wakati huo. Hii ni kwa sababu Daudi alikuwa mwabudu wa Yehova wa moyo wote. Aliitoa nafsi yake yote aendeleze ibada ya kweli katika milki yake yote. Ukizisoma Zaburi au mashairi ya kinubi yaliyoandikwa na Daudi, utaona alivyojisikia juu ya serikali ya kimungu. Kwa mfano, katika Zaburi 40, Daudi alisema hivi: “Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; naam, sheria yako imo moyoni mwangu.”​—Zab. 40:8.

11 Daudi alitamani kuliheshimu jina la Mungu na ibada kwa kujenga hekalu. Kwa kushukuru Yehova alifanya agano au ahadi nzito ya kumjengea Daudi nyumba, siyo makao ya halisi, bali nyumba ya ukoo wa wafalme katika jamaa ya Daudi. Alimwambia Daudi hivi: “Nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara milele.”​—2 Sam. 7:11-16.

12 Kijapokuwa kiti cha enzi cha Daudi mikononi mwa ukoo wake wa kifalme kilipinduliwa na Wababeli mwaka wa 607 B.C.E., kisisimamishwe tena duniani, Mungu hakulisahau wala hakuliacha agano hilo. Ikawaje hivyo?​—Eze. 21:25-27; Isa. 9:6, 7; Matendo 13:34.

MTAWALA ASIYEPOTOKA ATOKEZWA

13, 14. (a) Mungu alionyeshaje kwamba hakuwa amelisahau agano hilo la ufalme lililofanywa pamoja na Daudi, kwa habari ya kuzaliwa kwa Yesu? (b) Yesu aliingia katika mwendo gani alipomfikia Yohana abatizwe?

13 Hii ni kwa sababu Mungu hakukusudia kamwe kiti hicho cha enzi kisimamishwe duniani milele. Mfalme wa milele alipaswa awe wa ukoo wa Daudi. Yehova aliuweka ukoo huo salama, kupitia kwa Mfalme Sulemani, mwana na mrithi wa Daudi, na kupitia kwa Nathani vile vile, mwana mwingine. Karibu mwaka wa 2 B.C.E. Mungu alichagua msichana bikira aliyeitwa Mariamu, wa ukoo wa Nathani, naye akamfanya achukue mimba kwa roho takatifu. Kwa kweli, Mungu alihamisha uhai wa Mwanawe wa kimbinguni, aliyemwumba kwanza, akamleta kwenye chembe ya yai katika tumbo la uzazi la Mariamu. Kwa hiyo mtoto aliyezaliwa alikuwa Mwana wa Mungu. Hakukuwako uchafu wo wote katika hili. (Luka 1:26-33) Mungu alimweleza Yusufu jambo hili kupitia kwa malaika wake kijana ambaye alikuwa amechumbia Mariamu. Mtu huyu mwenye haki alimchukua Mariamu kama mkewe kwa uaminifu na utii, na wakati mtoto alipozaliwa akaitwa Yesu kwa uongozi wa kimungu, Yusufu alimlea Yesu kama mwanawe. Kufuata hapo Yusufu na Mariamu walipata watoto wengine.​—Mt. 1:18-25; 13:53-56.

14 Kwa hiyo Yesu alikuwa ndiye mrithi wa asili wa Daudi kupitia kwa mama yake, mzao wa mwana wa Daudi Nathani. Lakini namna gani juu ya haki ya kifalme, iliyokuwa ya ukoo wa Sulemani? Kulingana na sheria Yesu alikuwa nayo haki hii vile vile, kwa maana baba yake mlezi Yusufu alikuwa mzao wa Mfalme Sulemani. Kwa hiyo, Yesu alijitoa kwa mjumbe wa Mungu Yohana Mbatizaji abatizwe alipokuwa mwenye umri wa miaka 30, akiwa kama mrithi astahiliye wa Mfalme Daudi. Hapo Yesu alikuwa akiingia katika mwendo ambao ungemjaribu yeye na kumhakikisha kuwa mtawala anayestahili kutumainiwa kabisa na asiyepotoka juu ya kiti cha enzi cha Daudi milele.​—Ebr. 10:5-10; 5:8-10.

15. Kutiwa mafuta kwa Yesu kulitofautianaje na kwa Daudi, nako kulimaanisha nini kwake?

15 Lakini, utawala huu haukupaswa uendeshwe kutoka kiti cha enzi cha kidunia. Alipobatizwa Yesu akawa Masihi, Kristo, Mtiwa Mafuta wa Mungu. Wafalme wengine wa ukoo wa Daudi walikuwa wamekwisha tiwa mafuta halisi, lakini Yesu alitiwa mafuta kwa roho takatifu na akazaliwa kama Mwana wa kiroho wa Mungu. (Mt. 3:13-17; Matendo 10:38) Mwishowe alipaswa kufa na kufufuliwa aende mbinguni, ambako alikuwa amekuwa hapo kwanza na Baba yake, hata kabla ya kuimarishwa kwa ulimwengu.​—Yohana 1:1-3, 18; 8:58; Kol. 1:13-17.

MTAWALA ALIYEJARIBIWA NA KUHAKIKISHWA

16. Mwana wa Mungu alikuwaje na sifa za utawala hata kabla hajaja duniani?

16 Twawezaje kuwa na hakika kwamba serikali ya Masihi itakuwa isiyopotoka? Mungu aliutabiri na kuutayarisha utawala wake kwa karne nyingi. Hata kabla ya Mwanawe kuja duniani Mungu alimtumia yeye, kama msimamizi asiyeonekana wa taifa la Israeli. (Kut. 33:1, 2; 23:20-23) Akiwa katika cheo hiki Mwana wa Mungu alikuwa na ujuzi mwingi katika kutumia sheria za Mungu na katika njia ya Mungu ya kushughulika na wanadamu. Zaidi ya hayo, wakati mwingi kabla ya hapo, Mwana huyu, ambaye alikuja kuitwa Yesu Kristo, alikuwa “stadi wa kazi” wakati wa uumbaji wenyewe wa vitu vyote akisimamiwa na Yehova. Kwa hiyo yeye alipendezwa sana na wanadamu.​—Mit. 8:22, 30, 31.

17. Mungu alihitaji nini kutoka kwa watawala katika taifa lake la mfano la kitheokrasi?

17 Kwa habari ya kutokupotoka kwake, njia yake ya kuishi duniani ilihakikisha kwamba yeye alikuwa asiyeweza kukubali rushwa asiyeweza kulazimishwa afanye mabaya, kuondoka hata hatua moja katika kanuni za haki na uaminifu. Yeye alitimiza sifa za Mungu zilizotajwa alizopaswa kuwa nazo mtawala. Kwa wale ambao wangewekwa kama waamuzi na maafisa katika serikali yake ya mfano ya Israeli, Mungu aliamuru hivi: “Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza daawa ya wenye haki. Yaliyo haki kabisa ndiyo utakayoyafuata, ili upate kuishi.”​—⁠Kum. 16:19, 20.

18, 19. Yesu alijionyeshaje kuwa asiyeweza kukubali rushwa?

18 Chukua, kwa mfano, jaribio kubwa la kupewa rushwa ambalo Yesu alikutana nalo mapema katika huduma yake ya kidunia. Shetani Ibilisi, ambaye Maandiko yanasema ni “mungu wa dunia hii” na anayeongoza hasa falme zilizoundwa na mwanadamu za ulimwengu huu, alimtolea Yesu toleo ambalo hapana mtawala ye yote wa kibinadamu leo angelikataa. (2 Kor. 4:4). Yesu alionyeshwa sura yote ya falme zote za ulimwengu. Yesu alipewa toleo la hizi kwa sharti la kwamba atende tendo moja tu la ibada kwa Ibilisi. Ebu wazia​—utawala wa ulimwengu ukitolewa na mtu ambaye angeweza kuutoa mara ile ile! Kama mtawala alifikiri angeweza kuufaidi ulimwengu au alikuwa mchoyo kabisa au sivyo​—ni mtu gani wa kisiasa ambaye angeweza kukataa toleo hilo?

19 Lakini Yesu alijua kwamba tendo moja la kutoaminika lilimaanisha kuikana enzi yote ya Yehova. Alijua kwamba Yehova peke yake ndiye Aliye Mwema, na kwamba kutoka Chanzo hiki peke yake serikali ingeweza kuja ambayo ingeleta amani na haki duniani. (Marko 10:18) Vile vile alijua kwamba, ijapokuwa anaweza akatawala kwa muda mrefu kama mtawala wa ulimwengu wa namna hiyo juu ya falme za kisiasa, mwishowe Yehova angeiharibu serikali yake. (Dan. 2:44) Bila ya kulitafakari toleo hili hata kidogo, alimjibu mara ile ile: “Nenda zako, Shetani.”​—Mt. 4:1-11.

20. Ajapokuwa mrithi wa agano la ufalme lililofanywa pamoja na Daudi, kwa sababu gani Yesu hakujaribu kujifanya mfalme wa Israeli?

20 Yesu hakujaribu kujifanya mfalme wa kidunia hata juu ya nyumba ya Daudi au juu ya nyumba ya Yakobo, baba wa taifa lake. Yeye aliisukumia mbali jitihada ya wengi ya kumfanya mfalme. (Yohana 6:14, 15) Alilitazamia agano la Yehova alilofanya na ukoo wa Daudi la kumletea yeye ufalme katika wakati wa Mungu. Yeye alijihakikisha kuwa ndiye mfalme astahiliye aliyechaguliwa na asiyepotoka wa serikali ya kimbinguni ya Mungu. Alitoa ushuhuda wa ufalme wake mbele ya Gavana wa Kirumi Pontio Pilato, lakini wakati ule ule akaeleza hivi: “Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. . . . ufalme wangu sio wa hapa. “​Yohana 18:33-37.

21. Kama aliyetazamiwa kuwa mfalme, Yesu alionyeshaje kujitoa kwake kwa kweli kusikotikisika?

21 Mikazo mikubwa sana ilimjia Yesu​—chuki kutoka kwa watu wake mwenyewe, uchongezi, mateso rasmi. Mwishowe aliuawa juu ya mti akishtakiwa mambo mabaya sana, yaliyotungwa kwa uongo​—mashtaka ya kufuru na ya kuchochea watu waasi serikali. Yeye angaliweza kuepuka namna hii ya kifo kwa kuridhiana, kwa kudhoofisha nguvu za kweli awapendeze viongozi wa kidini na wa kisiasa. Lakini yeye alisimama upande wa kweli ijapo dhihaka, chuki, taabu na hata kifo.​—Yohana 8:31, 32; 1 Tim. 6:13.

22. Kwa sababu gani maadui wa Yesu wasingeweza kumwogofisha Yesu, wamfanye apotoshe kweli na haki?

22 Zaidi ya hayo, Yesu asingeweza kuogofishwa apotoshe haki, kama vile ambavyo wanasiasa wengi wamefanyiwa. Hapana mtu ambaye angeweza kupata ubaya wo wote ambao ungeweza kutumiwa umshawishi au kumhangaisha, hata dhambi “ndogo ndogo” zinazofanywa sana na watu kwa jumla. Maadui wake wa kidini bila shaka wangaliweza kulifahamu hata kosa lililo dogo zaidi kutoka sheria kamilifu ya Mungu. Lakini Yesu aliweza kuwaambia waziwazi hivi: “Kwa sababu nasema iliyo kweli, hamnisadiki. Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi?” (Yohana 8:45, 46) Kabla ya kufa kwake angeweza kusema: “Mtawala wa ulimwengu [Ibilisi ] anakuja [amfishe Yesu]. Naye hana lo lote la kushughulika na mimi.”​—Yohana 14:30, NW.

23. Yesu anastahilije kama mfalme juu ya shauri la upendo kwa raia zake?

23 Kwa habari ya upendo wake kwa watu ambao atawatawala, Yesu alitoa uhai wake kusudi kwamba waweze kuondoshewa dhambi zao na kutokamilika. Yeye alilinunua taifa la kibinadamu​—wote, tangu mkubwa zaidi hata aliye mdogo zaidi. (1 Tim. 2:5, 6) Kama Mfalme wa serikali yenye haki ya Mungu yeye atakuwa na msingi halali ambao juu yake anaweza kutumia mamlaka yake kuwaponya kwa kiroho na kwa kimwili wafikie ukamilifu wa kibinadamu, kusudi wapate uzima wa milele.​—Ebr. 9:28.

24. Mtume Petro alishuhudiaje maisha ya Yesu duniani yasiyo na kosa?

24 Ni nani basi awezaye kutoa kosa katika maisha ya kidunia ya Masihi, Kristo, Yeye aliyetiwa mafuta atawale kama mfalme juu ya wanadamu wote, awe mbinguni au duniani? Hapana awezaye. Akiyataja maisha ya Yesu Kristo duniani yasiyo na kosa, mtume Petro alimwambia akida wa Kirumi Kornelio na marafiki zake wa Kitaifa hivi: “Jambo lile ninyi mmelijua, lililoenea katika Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliouhubiri Yohana; habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa [roho takatifu] na nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye. Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu.”​—Matendo 10:37-39.

25. Kwa sababu gani ni jambo la haraka kuondoa imani sasa katika utawala wa mwanadamu na kuiweka katika ufalme wa Yehova wa Kimasihi?

25 Hali inayoharibika ya serikali leo inaelekeza kwenye mwisho wa utawala wa mwanadamu akiongozwa na Shetani. Kukaribia kwake kunafanya liwe jambo la haraka kwa wote kuitazamia serikali ya Mungu ya haki na uadilifu. Inawapasa wote wanaotaka uzima kuiunga mkono serikali hiyo kwa kujifunza juu yake na kuishuhudia kwa wengine. Mashahidi wa Yehova, wanaotumia nguvu nyingi na wakati ili waishuhudie, watafurahi kukusaidia wewe uwe mfuasi mwenye bidii wa serikali ya Mungu isiyopotoka chini ya Yesu Kristo.

​—Kutoka Kitabu God’s Kingdom of a Thousand Years Has Approached.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki