Baada ya Matengenezo ya Dini Kuharibiwa, Njia Gani?
Msomaji ataona inafaidi kusoma Yeremia sura za 40 mpaka 49 kabla ya kuchunguza makala hii na ile inayofuata.
“Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya [Yehova] kwa ulegevu; na alaaniwe azuiaye upanga wake usimwage damu.”—Yer. 48:10.
1. Kuharibiwa kwa Matengenezo ya Dini kutatokeza tatizo gani kwa waokokaji?
MATENGENEZO ya Dini za ulimwengu yameangamizwa! ” Twaweza kutazamia watu wenye kuchukia dini zote zenye kupendwa na watu wengi wayaseme maneno hayo kwa shangwe, wakati dini zote za leo zitakapoharibiwa kwa nguvu. Waokokaji wa tukio hilo la kushangaza sana wataenda njia gani? Wakati huo watakuwa na jambo gani la kugeukia? Twauliza maulizo hayo bila kucheza.
2. Ni ulizo gani lililotokezwa kwa sababu ya kutabiri kwa Yeremia, na baada ya karibu miaka 40 ya kutabiri hivyo, alijikuta wapi?
2 Kwa kutoamini wengine ambao wameshikamana na namna fulani ya dini yenye kupendwa na watu wengi mpaka sasa wanaweza kuuliza hivi, ‘Je! Muumba wa mbingu na dunia ataruhusu jambo kama hilo? ’ Ulizo hilo linafanana na lile lililoulizwa miaka ipatayo 2,655 iliyopita kwa sababu ya Myahudi wa nasaba ya kikuhani, nabii kijana Yeremia wa mji wa Anathothi katika Mashariki ya Kati. Ilielekea kuwa alikuwa akitabiri mabaya juu ya dini iliyokuwa ikifuatwa na watu wake mwenyewe katika wakati huo. Kulingana na Yeremia, hekalu lao, ambalo ndilo peke yake lililokubaliwa na sheria ya kidini, lingeteketezwa kabisa. Mji wao wenye hekalu, Yerusalemu, ungefanywa kuwa lundo la takataka. Watu wenye kufuata namna ya dini yenye kupendwa na watu wengi wangehamishwa kwenye nchi ya washindi wao, wakae huko miaka 70. Kutabiri kwa Yeremia juu ya misiba hiyo kulitokeza upinzani mkali. Kuelekea mwisho wa miaka 40 ya kutabiri hayo Yeremia alijikuta amezuiwa katika Yerusalemu, chini ya utawala wa Sedekia, mfalme wa mwisho wa jamaa ya kifalme ya Daudi kuketi juu ya kiti cha enzi.
3. Kwa kuruhusu msiba huo wa kidini, je! Yehova alikuwa akiharibu ibada yake mwenyewe, au namna gani?
3 Mungu yule ambaye jina lake liliitwa juu ya hekalu la Yerusalemu aliruhusu msiba huo wa kidini utokee. Kwa kweli, Yerusalemu ulipata ujumbe huo wa kuhukumiwa maangamizi kutoka kwa Mungu huyo mwenyewe, Yehova. Mambo gani hayo? Je! angeharibu dirii yake mwenyewe, ibada ya kumwabudu yeye kama Mungu wa kweli? Sivyo kabisa! Yeye alikusudia tu kuharibu namna ya ibada yake iliyochafuliwa na yenye kupotoshwa, iliyokuwa ikifanyiwa katika hekalu lililoitwa kwa jina lake, ambayo iliaibisha jina takatifu. Neno la Yehova kupitia kwa kinywa cha Yeremia lilishinda! Wale waliokuwa wakilikataa kwa ushupavu (shingo ngumu) walishindwa. Katika mwezi wa kiangazi wa Abi, mwezi wa tano katika kalenda ya mwaka wao, kuanzia siku ya saba mpaka ya 10 ya mwezi huo, hekalu hilo liliangushwa, na mji wa Yerusalemu uliobomolewa maboma, uliharibiwa. Kabla ya hayo, Sedekia, aliyekuwa mfalme, alikamatwa akitoroka nao maelfu ya waokokaji Wayahudi waliokonda waliendeshwa kwa miguu kama wafungwa, wakielekezwa kwenye uhamisho wenye kuchosha katika Babeli, yenye kutawala ulimwengu wakati huo.
4. Je! historia yote hiyo ya kale ni yenye maana na yenye kutuhusu sisi leo?
4 Haya, sasa, je! historia yote hiyo ya kale inatuhusu kweli kweli sisi leo? Ndiyo! Kwa sababu gani? Kwa sababu ilikuwa ya kiunabii, na kwa hiyo ilipaswa kuandikwa na kuhifadhiwa katika kurasa za Biblia Takatifu katika lugha nyingi zenye kuzungumzwa mpaka siku zetu. Mchunguzi mkubwa wa historia hiyo ya kale, Myahudi ambaye watu wake walihusika moja kwa moja katika historia hiyo yenye kutosha machozi, alikazia maana ya historia hiyo ya kale kwa kuandika maneno haya katika karne ya kwanza ya Wakati wa Kawaida wetu: “Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi, ambao mwisho wa nyakati unatukabili.”—1 Kor. 10:11, HNWW.
5. Paulo aliandika 1 Wakorintho 10:11 kabla ya msiba gani wa kidini, na sababu gani jambo kama hilo halitarudiwa tena?
5 Maneno hayo yenye kuogopesha ndiyo mtume Mkristo Paulo aliandika, karibu miaka 15 kabla ya mji uliojengwa tena wa Yerusalemu kuharibiwa, pamoja na hekalu lake, katika mwaka 70 W.K., wakati huo ukiharibiwa na vikosi vya majeshi ya Kirumi. Hakutakuwako mara ya tatu ya kutukia kwa jambo hilo, kwa kuwa hakuna hekalu la Kiyahudi linaloletea sifa Yerusalemu wa leo. Sasa dini tatu kubwa zinadai kupendezwa na mji huo ulio wa kweli, dini ya Jumuiya ya Wakristo, dini ya Waislamu na dini ya Wayahudi.
6. Sehemu ya kwanza ya Matengenezo ya Dini kuharibiwa itakuwa sehemu gani, na kisha kwenda kwenye sehemu nyinginezo za Matengenezo ya Dini kutamaanisha nini?
6 Kunazo dini za kale zaidi kuliko ile ya Jumuiya ya Wakristo. Na hata hivyo, kulingana na yale ambayo Yeremia wa Yerusalemu wa kwanza alivyoonyesha, Jumuiya ya Wakristo ndiyo itakuwa sehemu ya kwanza ya Matengenezo ya Dini kuharibiwa. Ehee, ndiyo, Yerusalemu ulifananisha kiunabii Jumuiya ya Wakristo, kwa kuwa inadai kufuata dini iliyoanzishwa katika Yerusalemu wa pili katika mwaka 33 W.K. Baada ya mfano huo wa Yerusalemu wa siku za Yeremia uliohukumiwa maangamizi kuharibiwa, basi washiriki wake wo wote watakaookoka wataenda njia gani? Wataenda kwenye dini yo yote ile isiyo ya Kikristo itakayookoka? Kufanya kwao hivyo kutamaanisha kukimbilia sehemu nyingine za jambo lile lililowekewa uharibifu wa milele, yaani, Matengenezo ya Dini.
7. Baada ya kuharibiwa kwa Yerusalemu. Wababeli walimruhusu Yeremia na mwandishi waishi wapi, nayo ni sikukuu gani iliyokuwa ikikaribia wakati huo?
7 Ebu tuone namna jambo hilo lilivyoonyeshwa baada ya Yerusalemu wa kwanza kuharibiwa katika mwaka 607 K.W.K., katika siku za Yeremia. Baadhi ya Wayahudi maskini wa nchi waliruhusiwa kubaki katika nchi iliyotekwa ya Yuda chini ya Gedalia, ambaye Mfalme mshindi Nebukadreza alikuwa amemweka kuwa liwali wa nchi hiyo. Jambo hilo lilitokea katika mwezi wa tano (Abi) wa mwaka 607 K.W.K. Yeremia na mwandishi wake Baruku walikuwa wamehifadhiwa hai, naye amiri wa jeshi la Babeli alimpa Yeremia uchaguzi wake wa kubaki pamoja na maskini wa nchi chini ya Liwali Gedalia. Sasa vipi? Majira ya mavuno ya vuli katika mwezi wa saba (Ethanimu, au Tishri) yalikuwa yakikaribia. Hivyo wakati uliowekwa wa kusherehekea sikukuu ya kukusanywa, au vibanda, kwa siku saba (Tishri 15-21) ulikuwa karibu. Lakini, ole! hakukuwa hekalu la Yerusalemu la kusherehekea karamu hiyo kwa furaha.—Kum. 16:13-16.
8. Je! Wayahudi watoro walirudi Yuda ili washerehekee sikukuu ya kukusanywa?
8 Jeshi la Babeli lilikuwa limeondoka katika nchi hiyo, isipokuwa vikosi vya majeshi yenye kushikilia sehemu zilizotekwa, nalo likachukua Wayahudi wengi waliookoka kama mateka. Kwa hiyo watoro Wayahudi walianza kurudi kutoka nchi jirani zilizokuwa karibu na kuingia katika nchi ya Yuda. Je! wao walikuwa wakirudi katika nchi ya kwao ili kutii Mtoa-sheria, Yehova, kwa kusherehekea sikukuu ya vibanda, au ya kukusanya, hata bila ya Yerusalemu kuwa na hekalu lake? Kama ambavyo mambo yalikuwa, hawakufanya hivyo.
9. Sababu gani kulikuwa ulizo juu ya ni njia gani ambayo watu wenye kurudi na maskini wa nchi ya Yuda wangeenda?
9 Wenye kurudi na maskini wa nchi walienda njia gani? Hawakuwa na lazima ya kuondoka katika nchi hiyo. Walakini Yeremia alikuwa ametabiri miaka 70 ya nchi kuwa mahame kabisa, pasipo mwanadamu wala mnyama wa kufugwa, kuwa inakaribia kutokea juu ya nchi hiyo. Bado Yeremia akawaambia wakaaji wa nchi hiyo wakae humo kwa amani, pasipo kuogopa cho chote kutoka kwa Wababeli waliokuwa wameondoka. Liwali wao, Gedalia, alikuwa Myahudi kama wao, ila sasa alikuwa anamtii Mfalme Nebukadreza wa Babeli. Hivyo Yehova Mungu wao hakuwa akiwalazimisha kutoka katika nchi yao waliyopewa na Mungu, hata ingawa alikuwa amemwongoza Yeremia kwa roho atabiri miaka 70 ya mahame kamili ya nchi ya Yuda.
MWUAJI ASHAMBULIA
10. Sababu gani hali ya kidini iliyowaelekea “maskini wa nchi” huko katika nchi ya Yuda ilikuwa yenye kusikitisha?
10 Lo! namna hao “maskini wa nchi” walioachwa katika nchi ya Yuda walivyokuwa wanaielekea hali ya kidini yenye kusikitisha! (Yer. 40:7, AV) Hakuna hekalu katika Yerusalemu la kuomba Yehova! Hakuna kuhani, Mlawi, isipokuwa Yeremia! Hakuna madhabahu ya kutoa dhabihu juu yake! Ndiyo, na hakuna “sanduku la agano” la dhahabu ambalo juu yake lilikuwa na sanamu za malaika wawili, ambalo kuelekea kwalo kuhani mkuu angenyunyiza damu ya dhabihu za Siku ya Upatanisho katika Tishri 10. Lilikuwa limetoweka mahali asipojua mtu ye yote mpaka siku hii!—Hos. 3:4.
11. Sababu gani Mfalme Baalisi wa Waamoni alimwona Ishmaeli mwana wa Nethania kuwa alikuwa chombo kinachofaa cha kumwondolea mbali Gedalia, liwali Myahudi?
11 Alitokea mlaghai (mtu mbaya sana) katika tamasha ya kutendeka kwa mambo! Yeye alikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania. Inaelekea kwamba Mfalme Baalisi wa Waamoni ambaye Ishmaeli alikuwa amekimbilia kwake walipokuja Wababeli, aliona kwamba Ishmaeli alifaa kuajiriwa ili amwue Gedalia, ambaye Mfalme Nebukadreza aliweka awe liwali wa mkoa wa Yuda. Sababu gani hivyo? Kwa sababu Ishmaeli alikuwa wa ‘uzao wa kifalme.’ Kwa hiyo kupitia kwa Elishama, babu yake, Ishmaeli alikuwa wa kifalme naye alikuwa mmoja wa ‘wanaume wakuu wa mfalme.’ (Yer. 41:1, NW) Hivyo, mshiriki huyo mwenye cheo wa Mfalme Sedekia aliyepinduliwa hangekubali kufanywa kwa Gedalia kuwa liwali ingawa yeye hakuwa wa ‘uzao wa kifalme.’ Kwa hiyo Mfalme Baalisi wa Waamoni, ambaye alikuwa amefurahia kuharibiwa kwa Yerusalemu, akamfanya Ishmaeli kuwa chombo chake katika kumwondolea mbali Gedalia.—Zab. 83:7, 8; Yer. 40:14.
12. Ishmaeli alilitekelezaje tendo lake lisilo halali, hata hivyo sababu gani baadaye alilazimika kukimbia?
12 Lijapokuwa onyo la Yohana mwana wa Karea, Gedalia alikaribisha Ishmaeli pamoja na washiriki wake 10 kwenye chakula katika mji mpya wenye makao ya serikali wa Mizpa, maili kadha kaskazini mwa magofu ya Yerusalemu. Ingawa kulikuwako askari kadha Wababeli, Ishmaeli akiwa na genge alishtua wote waliokuwako chakulani na waliokuwako karibu na kuwaua wote isivyo halali. (Yer. 41:2, 3) Bado wengine waliuawa na Ishmaeli pamoja na genge lake lenye hila. Jambo hilo lilitokea katika mwezi wa saba, Tishri, mwezi ambao kwa kawaida sherehe ya vibanda ilifanywa kwa siku saba. Watu wa Mizpa sasa wakawa na maelekeo ya kumfuata mnyang’anyaji huyo wa mamlaka kama watu waliotekwa nyara naye. Walakini, wakati Yohana mwana wa Karea alipojitokeza na kumpinga Ishmaeli, ndipo Ishmaeli na watu wake wanane walipotorokea nchi ya Amoni, ambayo ilikuwa bado haijatiishwa na Mfalme Nebukadreza wa Babeli.—Yer. 41:10-15; 49:1-5.
13. Yohana na wafuasi wake walipoomba, Yehova alimwongoza Yeremia kwa roho awape ujumbe gani? Nao waliitikiaje?
13 Kwa sababu ya jambo lililoipata serikali ya muda iliyokuwa imewekwa na Wababeli, Yohana na watu hao waliona sababu ya kuogopa mamlaka hiyo mpya ya ulimwengu, Milki ya Babeli, ambayo Yehova Mungu alikuwa akiitumia kama chombo chake cha kuua katika Mashariki ya Kati. Sasa walipaswa kwenda njia gani? Kwa utaratibu Yohana na wakuu wake wamkaribia Yeremia, ambaye kwa usahihi alikuwa ametabiri kuharibiwa kwa Yerusalemu. Waliahidi kwamba ujumbe wa Yehova kupitia kwa Yeremia uwe ungewapendeza ama sivyo, wangeutii. Siku kumi baadaye walipomwendea Yeremia ujumbe wa Yehova ulikuja kupitia kwake. Wasingepaswa kushindwa na woga, bali wangepaswa kubaki katika nchi hiyo wakiitii Babeli. Walakini iwapo kwa kukosa imani wangehama kuelekea kusini kuingia Misri, wangepatwa huko na upanga wenye kushinda wa mfalme wa Babeli, na kwa njaa na kwa tauni. Wangeangamia katika nchi ya Misri iliyohukumiwa maangamizi isipokuwa baki dogo. Hawangerudi kwa amani katika mkoa wa Yuda baada ya kupinduliwa kwa Milki ya Babeli. Je! Yohana na wafuasi wake walitii ujumbe huo wa kimungu? Sivyo kabisa! Waliutaja kuwa ni wa uongo. Walimwita Yeremia mwongo.—Yer. 42:1–43:3.
14. Ni nani ambao hawakushikamana na ahadi yao, na sababu gani sikukuu ya kukusanywa haikushekewa katika mwaka 607 K.W.K.?
14 Hata hivyo mwongo si alikuwa kila mmoja wao, kwa kuwa walikuwa wametoa ahadi ya kiapo kutii ujumbe ambao wangepewa na Yeremia hata kama haungewapendeza? Tayari walikuwa njiani kuelekea upande wa kusini kwenda Misri, na sasa walikuwa wameazimia kuendelea kukazana mpaka wafike katika nchi ya Nailo. Hawakutaka kutii utawala wa Mamlaka ya Tatu ya Ulimwengu, ile ya Babeli. Hapo kwanza Misri ilikuwa mwenzi wao katika kupinga mamlaka yenye kupanuka ya Babeli. Kwa kuwa sasa nchi ya Yuda ilikuwa imekuwa chini ya utawala wa Babeli, waliazimia kwamba mtu ye yote asiachwe katika nchi hiyo apate kuitii Babeli. Wenye kukubali kujitiisha chini ya Babeli, yaani, Yeremia na mwandishi wake Baruku, wasingeachwa. Kwa hiyo wakawaburuta watumishi hawa wa Yehova pamoja nao. Pasipo wao kukusudia iwe hivyo, karibu na wakati ambao nchi ya Yuda ingepaswa kusherehekea sikukuu ya kukusanywa, au ya vibanda, kwa furaha, katika Tishri 15-21, 607 K.W.K., hao waasi wa mapenzi ya Yehova waliondoka katika nchi hiyo kama vile tu alivyokuwa ametabiri, mahame yasiyo na mkaaji wa kibinadamu na mnyama wa kufugwa.—Yer. 43:4-7.
15. Matukio hayo ya siku za Yeremia yalihusianaje na mambo ya siku zetu wenyewe na yenye kutuhusu sisi?
15 Mapenzi ya Mungu Mwenye Nguvu Zote hayawezi kuzuiliwa hata kidogo. Neno lake la unabii haliwezi kuthibitishwa kamwe kuwa si sahihi. Wayahudi wasiotaka kushirikiana walipoondoka katika nchi ya Yuda, miaka 70 iliyotabiriwa ya ukiwa wa nchi pasipo mkaaji Mwisraeli na mnyama wa kufugwa ilianza. Ndipo pia, “nyakati saba” za mfano ambazo Yehova alimfanya Mfalme Nebukadreza aote juu yake naye Danieli atoe maelezo juu yake zilianza muda wake wa miaka 2,520. (Dan. 4:13-27; Luka 21:24) Kwa hiyo halikuwa jambo la kujitokeza hivi tu kwamba Vita ya Ulimwengu ya Kwanza ikatokea juu ya ulimwengu wenye amani, ili kuonyesha mwisho wa zile “nyakati saba” katika mwezi wa Tishri katika mwaka 1914 W.K. Kweli kweli, basi, matukio ya siku za Yeremia yalihusiana na nyakati zetu. Maana ya matukio hayo inatuhusu sana sasa!
16. Sababu gani kutorokea Misri kwa Wayahudi hao hakukuwa njia inayofaa, nao mwendo wa Wayahudi hao unatufanya sisi kutazamia nini katika wakati ujao?
16 Baada ya dini iliyosimamishwa na Wayahudi wenye kukaidi Sheria kule Yerusalemu kuanguka katika mwaka 607 K.W.K., je! Wayahudi wale waliokimbilia Misri waliepuka jambo lile walilochukia? Je! walichagua njia bora zaidi, njia inayofaa? Sivyo hata kidogo, iwapo walipata kuwa tamasha yenye kuogopesha sana ya yale yatakayopata watu wa kidini ambao wanakataa kutii Neno la Yehova. Ingawa Yeremia alilazimika kukaa Misri, hakuacha kutabiri akiwa kule. Roho ya Yehova iliendelea kumsukuma Yeremia atabiri, ndiyo, kwa wakimbizi Wayahudi wasioamini na juu ya nchi ya kukaa waliochagua. Maandishi yake yaliyoongozwa kwa roho yangaliko mpaka wakati huu wenye hatari. Yanatumika kama mifano ya kisasa ya hao Wayahudi wenye kuasi wa siku za Yeremia. Kwa sababu ya jambo hilo, twaweza kutazamia nini katika siku za wakati ujao zilizo karibu?
17. Ni tendo gani tusiloweza kutazamia upande wa waokokaji wa kuharibiwa kwa Jumuiya ya Wakristo watakaoshuhudia kwa macho yao, na sababu gani hivyo?
17 Twapaswa kutazamia kuharibiwa kwa sehemu yenye nguvu zaidi ya Matengenezo ya Dini, yaani, Jumuiya ya Wakristo pamoja na mchafuko wake wote wa madhehebu za kidini. Jambo hilo litatokea katika wakati wa Yehova usiobadilika. Kwa hiyo, ulizo ni hili, Wakati jambo hilo litakapotokea, basi watakaoshuhudia tukio hilo lenye kushangaza watachukua mwendo gani? Kulingana na kiolezo kilichowekwa katika mwaka 607 K.W.K. na Ishmaeli na Yohana na wafuasi wao waliokataa kutii shauri la Yehova, hatuwezi kutazamia kundi kubwa lisilo na hesabu la watu hao wenye kushuhudia kwa macho wageukie Ukristo wa kweli unaofuatwa na jamii ya Yeremia ya kisasa na wenzi wao washikamanifu. Ukristo wa kweli unatia ndani kuabudu Mungu wa Yeremia, Yehova, Baba wa kimbinguni wa Yesu Kristo. Yeye alizungumza juu ya kumwabudu Yehova aliposema hivi kwa mwanamke Msamaria kisimani: “Saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba [kwa] roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu [kwa] roho na kweli.”—Yohana 4:23, 24.
18. Wakati Yesu Kristo alipokuwako duniani alikuwa shahidi wa nani, na ni nani sasa wanaopaswa kuwa mashahidi kama yeye?
18 Hata Mkristo hawezi kupuza kumwabudu Yehova kama Mungu. Katika Ufunuo 1:5 Mwana wa Mungu alijiita mwenyewe “Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu.” Alipokuwa duniani kama mwanadamu yeye alikuwa Myahudi, Mwisraeli, ambaye taifa lake liliandikiwa maneno ya Isaya 43:10: “Ninyi ni mashahidi wangu, asema [Yehova], na mtumishi niliyemchagua.” Yesu alionyesha kwamba yeye alikuwa shahidi mwaminifu na wa kweli wa Yehova Mungu. Wanafunzi wake wa kweli leo wanapaswa kuwa mashahidi wa namna ile ile, wa Yehova.
19. Baada ya Jumuiya ya Wakristo kuharibiwa, je! waokokaji walioshuhudia kwa macho watakwenda kwenye Mashahidi wa Yehova, nayo matengenezo mengine ya kidini yanatoa tumaini gani kwa waokokaji?
19 Hatuwezi kutaja maandiko yo yote ya kiunabii ya Biblia kuonyesha kwamba baada ya mfano wa kisasa wa Yerusalemu wa kale kuharibiwa katika “dhiki kubwa” inayokuja, washiriki wa kale wasio na hesabu wa Jumuiya ya Wakristo wataongolewa na kujiweka upande mmoja na wale Wakristo wenye kuteswa wanaojulikana kama Mashahidi wa Yehova. Huenda watu wengi wakalia kwa sababu ya faida walizopoteza kwa ajili ya kuharibiwa kwa moto kwa Jumuiya ya Wakristo yenye kupenda mali, kama vile wanabiashara wale ambao Ufunuo, sura ya 18, unawafananisha kama wakilia kwa sababu ya kuteketezwa kabisa kwa Babeli Mkuu. Walikuwa wamepoteza biashara pamoja naye yenye kuwatajirisha. Huenda watu wengine wenye kufikiria mambo ya dini wakaziendea dini nyingine zisizo za Kikristo zitakazobaki kidogo baada ya Jumuiya ya Wakristo kuharibiwa. Watu hao watakuwa tu wanaenda kwenye tengenezo jingine la kidini lililohukumiwa maangamizi, kwa kuwa yote ni ya Babeli Mkuu, milki ya ulimwengu ya dini ya uongo. Sehemu zake zote zimekusudiwa kuangamizwa!
20. Twaweza kujuaje njia ambayo wale watakaookoka kuharibiwa kwa Babeli Mkuu watachukua?
20 Watakaookoka kuharibiwa kwa Babeli Mkuu wataenda wapi au wataenda njia gani? Maandiko ya kiunabii yaliyoongozwa kwa roho yanaonyesha nini? Je! wataenda, wanaweza kwenda, kwenye upande wa wale wanaofananishwa na Yeremia na mwandishi wake Baruku? Matukio ya kiunabii wakati wa siku za mwisho za waabudu hao wa Yehova yanatoa jibu.