Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w81 8/15 uku. 3
  • Nani Anayeweza Kuridhika?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nani Anayeweza Kuridhika?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Habari Zinazolingana
  • Unaweza Kuridhika na Fungu Lako Maishani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Kisiwa cha Cocos—Hadithi Zake za Hazina Zilizozikwa
    Amkeni!—1997
  • Pata Uradhi kwa Kutumia Kanuni za Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • ‘Pata Kimbilio Katika Jina la Yehova’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
w81 8/15 uku. 3

Nani Anayeweza Kuridhika?

WATU wengi wanaamini kwamba kutafuta kuridhika kunaweza kutokeza furaha kama wangehamia kwenye kisiwa cha mbali chenye joto na kilicho salama. Hakika, wakiwa hapo wangeweza kufurahia maisha yenye utulivu wakiota jua, wakiwa na chakula kingi na bila kuwa na wasiwasi wo wote.

Katika kitabu Rascals in Paradise, James A. Michener na A. Grove Day anasema juu ya “tukio la kihadithi tu katika historia ya hivi karibuni ya Pasifiki.” Kwa halisi, hadithi hiyo inasema kwamba katika miaka iliyoanzia na mwaka wa 1930 Mwaustralia mmoja alikata kauli kwamba vita kubwa ilikuwa inakaribia. Akitaka kuepuka kujiingiza katika tukio hilo lenye kuleta msiba, kwa kufuata utaratibu alitafuta mahali pa kukimbilia.

“Mwishowe,” tunaambiwa, “kwa kutumia akili sana, aliamua kwamba kimbilio peke yake lililo salama kutoka kwa wazimu wa ulimwengu ni kisiwa fulani chenye joto. . . . alifanya uchunguzi juu ya Pasifiki naye akaonelea uchaguzi wake uwe kisiwa kimojawapo chenye kila namna ya faida: kilicho mbali, salama, chenye maisha mazuri . . . mwishoni-mwishoni mwa kiangazi cha mwaka 1939, juma moja kabla ya Ujeremani kuvamia Poland, Mwaustralia huyo mwenye hekima alikimbilia mahali alipochagua katika Pasifiki ya Kusini. Akaenda kwenye kisiwa kisichojulikana sana cha Guadalcanal.” Lakini je! alipata usalama na uradhi huko?

Ole, wa mkimbizi huyo, hata kisiwa hicho kilicho mbali cha Guadalcanal kikawa mahali penye kupiganiwa vikali katika miaka ya 1942 na 1943! Kweli kweli, katika sehemu kubwa ya Vita ya Ulimwengu ya Pili, kisiwa hicho kilikuwa paradiso ya kufanya lo lote bila kujali.

Yote hayo yalitokea makumi mengi ya miaka iliyopita. Lakini namna gani siku za leo? Mtazamaji mnyofu anaona ni nini?

Migomo, maandamano ya kupinga, watoto kutoroka, kuacha shule, matumizi yasiyo halali ya dawa za kulevya, nyumba zilizogawanyika na talaka—yote hayo yanakuwa mambo ya kawaida. Sababu gani? Ni nini linalotokeza mengi ya matatizo hayo? Kutoridhika!

Ebu fikiri, pia, juu ya tisho la wakati huu juu ya amani. Fikiria uwezekano wa kutokea mauaji makubwa yenye kuletwa na silaha za nuklea. Nani anayeweza kuridhika kati ya hali kama hizo?

Leo, kama ilivyokuwa katika Vita ya Ulimwengu ya Pili, hakuna kisiwa chenye joto kilicho peke yake ambacho ni salama tunachoweza kukimbilia. Kukiwako ndege za kusafiria, njia za kuwasiliana na wengi—ndiyo, na uchafuaji wa hewa—hakuna ye yote wetu anayeweza kupata mahali ambapo sasa panatoa usalama na utulivu kamili. Lakini, je! hiyo inamaanisha kwamba wanaume wote, wanawake na vijana hawana jambo jingine ila maisha yasiyo na furaha na yasiyotosheleza? Hapana. Nalo jambo hilo tutaliona tunapofikiria ulizo hili lenye uharaka, Unaweza kuridhika na fungu lako maishani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki