Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w87 10/1 uku. 21
  • Chifu Atetea

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Chifu Atetea
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Habari Zinazolingana
  • Jambo Kuu Maishani Mwako Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Sehemu ya 4—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Sehemu ya 5—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya Dunia
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Walimtumaini Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
w87 10/1 uku. 21

Ripoti ya Watangazaji Ufalme

Chifu Atetea

NI JAMBO lenye kutia moyo kujua kwamba bado kuna watu walio katika cheo cha juu katika ulimwengu huu ambao wanapenda unyofu na haki na ambao wanatoa sauti kutetea sifa hizo. Mfano ni chifu mmoja katika nchi ya Kiafrika ambako kazi ya Mashahidi wa Yehova ina vizuizi. Acheni ripoti ituambie:

“Juzijuzi vikundi tofauti vya kidini vilifanya mkusanyiko wa kimadhehebu katika mji wetu, na hiyo ilitia ndani Wakatoliki, Wapresbiteri, Wapentekoste, na kadhalika. Chifu Mkuu alialikwa kuhutubia mkusanyiko kuelekea vile vipindi vya kumalizia. Kwa mshangao wa kusanyiko zima, yeye aliambia hao, miongoni mwa mambo mengine, waige unyofu na viwango vya juu vya kiadili vya Mashahidi wa Yehova, akiongeza kwamba kama wote wangekuwa kama Mashahidi wa Yehova, kungekuwa na amani katika taifa lile.

“Siku iliyofuata washiriki mashuhuri wa makanisa yaliyowakilishwa kwenye mkusanyiko walikuja kwenye jumba kuu la Chifu na kuteta kwa ukali dhidi ya sehemu ile ya hotuba yake iliyosifu Mashahidi na wakamwuliza kama yeye hakujua kwamba Mashahidi walikuwa wamepigwa marufuku katika nchi ile. Chifu alijibu kwamba alijua hivyo lakini akaambia hao kwamba yeye hakupata kosa katika Mashahidi wa Yehova. Yeye aliendelea kusema: ‘Kwa miaka yangu yote ya kuwa Chifu Mkuu, hakuna mara moja ambayo mmoja wa Mashahidi wa Yehova ameletwa kwenye mahakama yangu kwa kutenda kosa zito. Kwa upande ule mwingine, ikiwa muhogo umeibwa kutoka shamba fulani, mara nyingi inakuwa kwamba Mkatoliki ndiye mwivi. Ikiwa kiazi kikuu kimeibwa, ni Mpresbiteri ambaye analaumika. Washiriki wa kanisa lenu wamechafua nchi yangu kwa visa vya kutoa mimba, na hali hakuna mmoja wa Mashahidi wa Yehova ameletwa kwenye mahakama yangu kwa makosa kama hayo. Je! sheria za Mungu hazikatazi maovu hayo, au je! makanisa hayafungwi tena na wajibu wa kufuata sheria ya Mungu.’ Wale viongozi wa kidini hawakuwa na jibu.

“Baadaye, yule Chifu Mkuu aliita wawakilishi wa Mashahidi wa Yehova na akawahimiza wajitunze vizuri wao wenyewe ili suto lo lote lisiletwe juu ya jina la Mungu wao na juu ya jina lake mwenyewe akiwa ndiye Chifu Mkuu ambaye ametetea Mashahidi wa Yehova.”

Ripoti inaonyesha kwamba sasa wapya wengi wanachukua msimamo wao kwa ajili ya ukweli. Shahidi mmoja anasema kwamba yeye ameweza juzijuzi kuanza mafunzo ya Biblia pamoja na machifu watatu katika eneo lile, mmoja wao akiwa ni yule Chifu Mkuu, na wote watatu wanahudhuria mikutano ya Mashahidi wa Yehova!

Yehova Mungu anaona wale ambao wanapenda ukweli na uadilifu na kuutetea kwa ajili ya watumishi wake.​—Mathayo 10:42.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki