Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 4/15 kur. 3-4
  • Ndoto ya Amani ya Ulimwengu—Njozi Yenye Kosa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ndoto ya Amani ya Ulimwengu—Njozi Yenye Kosa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nani Awezaye Kuleta Amani Yenye Kudumu?
    Amkeni!—1996
  • Ni Nani Wanaosababisha Tisho la Vita vya Nyuklia?
    Amkeni!—2004
  • Mwaka 1986—Je! Ni wa “Kulinda Amani”?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Tisho la Nyukilia—Laondolewa Milele!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 4/15 kur. 3-4

Ndoto ya Amani ya Ulimwengu—Njozi Yenye Kosa

MAONI ya kutazamia mazuri juu ya mataraja ya amani ya ulimwengu yanapanda juu sana. Katika safu yake kwa The Toronto Star, Carol Goar aliandika: “Maafikiano ya amani yanafanikiwa sana kutoka Afghanistani kufika Angola. Mapambano ya mikoa ambayo yalielekea kutosuluhika miezi michache iliyopita yanaonyesha ishara za kupungua. Nao Umoja wa Mataifa unapata uzaliwa mpya wenye kuchangamsha moyo.” Hilo, asema Goar, ‘limeanzisha msambao wa tumaini kote katika tufe.’ Tahariri moja katika USA Today ilipiga mbiu vivyo hivyo hivi: “Amani inazuka kote kote ulimwenguni.”

Hasa jambo linalostahili kuangaliwa katika nyakati za majuzi ni kile ambacho UN Chronicle ilikieleza kuwa “rapprochement [mapatano] yanayoendelea kati ya Soviet Union na United States.” Kuondolewa kwa vikosi, matukio yenye kushangaza katika Ulaya Mashariki, mazungumzo juu ya kupunguza vikosi na silaha—matukio haya yamezusha matumaini kwamba yale mataifa yenye nguvu zaidi huenda mwishowe yakazuia mashindano ya kuunda silaha. Katika ulimwengu ambamo matumizi ya kijeshi yanasemekana humaliza uchumi wa zaidi ya dola milioni elfu 850 kila mwaka, hili ni taraja lenye kukaribishwa sana.

Hata hivyo, kuna uwezekano gani kwamba ndoto ya mwanadamu ya amani ya ulimwengu itatimia? Hata watazamaji wenye maoni bora zaidi ya kutazamia mazuri wanakubali kwamba kutoka kupunguza silaha mpaka kuzimaliza kabisa ni hatua kubwa mno. Kumaliza kabisa silaha za nyukilia kungetaka kadiri isiyopata kufikiwa ya kutumainiana. Hata hivyo, kwa kuhuzunisha, yale mataifa yenye nguvu zaidi yana historia ndefu ya kutotumainiana. Kama ilivyosemwa kwa unabii katika Biblia, huu umekuwa muhula ambamo wanadamu wamethibitika kuwa “wasiotaka kufanya suluhu [“wavunja-mapatano,” King James Version].”—2 Timotheo 3:3.

Na zaidi, si kila mtu anasadiki kwamba kumalizwa kwa silaha za nyukilia kungeleta amani. Hata kama mataifa yangeshawishwa yaondolee mbali marundo yao ya silaha za nyukilia, silaha za kawaida zingali zaweza kuua kwa kufanikiwa sana. Vita ya Ulimwengu 1 na 2 hutoa ushuhuda mzito wa uhakika huo. Zaidi ya hilo, ile tekinolojia inayohitajiwa kuunda tena silaha za nyukilia ingebaki—tayari na ikingojea ishara za kwanza za wasiwasi wa kisiasa. Wengine, kama mwanasayansi wa kisiasa Richard Ned Lebow, hata wanabisha hivi: “Pengine kuwa na silaha chache za nyukilia karibu kunawaweka watu wakiwa wenye tahadhari.”

Lakini maadamu kuna silaha za nyukilia, tisho la angamizo la silaha za nyukilia litakuwa dhihaka kwa dai lolote la kupata amani; na ndivyo kutakavyokuwa kuendelea kwa yale matatizo yasiyo ya kivita yanayonyang’anya mamilioni amani katika maisha yao ya kila siku. Katibu mkuu wa UM Javier Pérez de Cuéllar alisema juu ya “hali mbaya ya mamilioni ya wananchi wenzetu wasio na makao au wanaoishi katika makao ya hali isiyotosha kabisa. Tatizo hilo linazidi kuwa baya.” UN Chronicle yaripoti zaidi kwamba kutositawi kiuchumi kunasumbua “theluthi mbili za ainabinadamu, katika visa fulani kwa kadiri ya umaskini na ufukara usiopambanulika na yale mateso yanayoletwa na vita.” Na namna gani juu ya hali ya wakimbizi wa ulimwengu wanaokadiriwa kuwa milioni 12? Je! kupunguzwa kwa silaha au hata kumalizwa kabisa kwa silaha kutaleta amani katika maisha yao?

Kwa wazi, ndoto ya mwanadamu ya amani ya ulimwengu ni njozi yenye kosa—isiyoona mbali, hafifu, yenye mipaka. Je! kuna taraja bora zaidi kwa amani? Lipo kweli kweli. Katika toleo lililotangulia la gazeti hili, tuliona kwamba Biblia inatoa tumaini hakika kwa amani.a Karibuni Yesu Kristo, akiwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu, ataleta amani inayopita kwa mbali sana mataraja yoyote ya binadamu. Lakini amani hiyo itamaanisha nini hasa kwa ainabinadamu? Makala inayofuata itazungumzia hilo.

[Maelezo ya Chini]

a Ona “Ni Nani Ataongoza Ainabinadamu Kwenye Amani?” katika toleo letu la Aprili 1, 1990.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki