Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 5/15 uku. 30
  • Muono-Ndani Juu ya Habari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Muono-Ndani Juu ya Habari
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Ni ya Kizamani?
  • Uzuizi Bora Kabisa
  • Jinsi ya Kuwalinda Watoto Wako
    Amkeni!—2003
  • Jinsi Ambavyo Dawa za Kulevya Haramu Huathiri Maisha Yako
    Amkeni!—1999
  • Vijana na Dawa za Kulevya
    Amkeni!—2003
  • Je, Vita Dhidi ya Dawa za Kulevya Itashinda?
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 5/15 uku. 30

Muono-Ndani Juu ya Habari

Je! Ni ya Kizamani?

Kulingana na padri mmoja Mwanglikani katika Adelaide, Australia, maonyo dhidi ya usisimuaji wa mwili ambao waweza kuongoza kwenye uasherati na uzinzi ni ya kizamani na yatoka kwenye vyanzo visivyo vya Kikristo. Katika uchunguzi wake wa majuzi kuhusu hali ya uume na uke, yeye ataarifu kwamba watu waliopatana kufunga ndoa hawawi kwa lazima wanatenda dhambi wakifanya ngono kabla ya ndoa. Pia uchunguzi huo wakazania kwamba ugoni-jinsia-moja ungeweza kukubalika katika visa fulani. Kulingana na Courier Mail ya Brisbane, mneni mmoja wa Kanisa la Muungamanisho (Uniting Church) katika Australia “aliafikiana na kanuni za msingi za ripoti hiyo.”

Hata hivyo, Biblia hutaarifu wazi kwamba ni mapenzi ya Mungu kwamba wote ‘waepukane na uasherati’ na kwamba “waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu . . . wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti.” (1 Wathesalonike 4:3, 4; 1 Wakorintho 6:9, 10) Kwa uhakika, wale ambao huikubali Biblia kuwa Neno la Mungu lililovuviwa hutambua kwamba maoni yalo juu ya ngono hutoka kwa Muumba mwenye hekima yote. Tokeo juu ya wale ambao huishi kulingana na viwango vya Biblia huthibitisha kwamba miongozo hii ya kiadili ambayo huitwa ya kizamani eti bado huchangia kufanyiza familia zenye uthabiti na huandaa ulinzi salama dhidi ya makovu ya kina kirefu katika hisia-moyo na magonjwa ya kuchukiza sana ambayo hutokana na mwenendo wa ufisadi.

Uzuizi Bora Kabisa

Utumizi mbaya wa dawa za kulevya wabaki ukiwa tatizo zito. Kwa hiyo basi, ni njia gani iliyo bora kabisa kwa kulinda vijana na utumizi mbaya wa dawa za kulevya? Katika mahoji yaliyochapishwa katika gazeti la Kibrazili O Estado de S.Paulo, profesa na daktari wa akili Mfaransa Claude Olievenstein alikazia uhitaji wa miongozo na tegemezo lenye upendo. Alisema hivi: “Leo watu waongeapo juu ya dawa za kulevya, fungu lenye kutimizwa na polisi, mfumo wa kihukumu, na shule hutiliwa mkazo. Hata hivyo, uhitaji ulio mkubwa ni ule wa uzuizi wa kifamilia [wa utumizi wa dawa za kulevya]. . . . Watoto wengi hawajui mamlaka ya kibaba ni nini. Baba huwa hayupo; yaonekana amejiuzulu.”

Akieleza kwa nini ni muhimu kuzuia kutumia dawa za kulevya katika familia, Dakt. Olievenstein aliongeza hivi: “Twaishi katika jamii yenye kujitafutia faida ambapo watu huyaonea aibu maadili. Watoto wetu waanzapo kudhihirisha tabia fulani kwa sababu ya dawa za kulevya, hiyo huwa ni kwa sababu sisi tumeacha kufanya maadili yajulikane. Jamii yetu imekuwa sugu, iliyokufa ganzi, yenye kufikiria shughuli za viwanda. Watu hufikiria ile jitihada kali tu ya kutafuta riziki maishani.”

Kulingana na gazeti Superinteressante, uchunguzi mmoja wa United States huhakikishia umaana wa mamlaka ya kibaba. Jarida hilo lataarifu hivi: “Wabalehe waliofanya vizuri kabisa katika mitihani ya shule na walio thabiti zaidi kihisia-moyo walikuwa wa kutoka kwenye familia ambazo wazazi walijizoeza mamlaka ya kukazia sheria za wazi juu ya mwenendo na wakatoa uhuru usiovuka mipaka iliyoelezwa wazi. Vivyo hivyo, kadiri ya wabalehe wenye kuzoelea dawa za kulevya na kileo ni ya chini zaidi katika familia za jinsi hiyo.”

Ikiwa na sababu njema, Biblia hushauri wazazi hivi: “Mrudi mwanao naye atakustarehesha; naam, atakufurahisha nafsi yako.” (Mithali 29:17) Ndiyo, sahihisho lenye msingi wa Biblia laweza kusaidia wazazi kuzuia utumizi mbaya wa dawa za kulevya na kufanya ubora wa maisha upate maendeleo kwa ajili ya familia nzima.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki