‘Alipiga Vita Vilivyo Vizuri’
Ndugu F. E. Skinner alimaliza mwendo wa maisha yake ya kidunia siku ya Julai 4, 1990. Edwin Skinner alikuwa na umri wa miaka 96 na alikuwa ametumikia masilahi ya Ufalme wa Yehova katika India tangu Julai 1926. Alibatizwa katika Uingereza katika 1919. Hadithi ya maisha yake ilitokea katika Mnara wa Mlinzi la Januari 1, 1990. Ndugu Skinner alikuwa mwanamume mwenye imani na uvumilivu kweli kweli katika kupiga mbio ya mwendo hadi mwisho, na hakika amepata thawabu yake.—2 Timotheo 4:7, 8.