Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 10/1 uku. 21
  • Njaa Kubwa Yatabiriwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Njaa Kubwa Yatabiriwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Njaa Ina Maana Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Suluhisho Ni Nini?
    Amkeni!—1996
  • Idadi Yenye Kuongezeka ya Wakimbizi
    Amkeni!—1996
  • Kupata Makao ya Kudumu
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 10/1 uku. 21

Njaa Kubwa Yatabiriwa

KATIKA miaka ya hivi karibuni tisho la njaa kubwa limepata kuwa jambo la kawaida katika ripoti za habari ya ulimwengu, kwa njia ya kuumiza. Picha za kuteseka zisizosahaulika zimetoka Ethiopia na kwingineko. Katika 1992 fikira za ulimwengu zilielekezwa kwenye wale katika Somalia, wenye kupatwa na msiba wa njaa kubwa, iliyosababishwa na ukame na vita. International Herald Tribune liliripoti katika Septemba 1992 hivi: “Hakuna ajuaye ni Wasomalia wangapi ambao wamekufa, lakini [shirika la] Msalaba Mwekundu laweka tarakimu hiyo kuwa zaidi ya 100,000. Mamia, kama si maelfu, hufa kila siku.”

Tarakimu hizo hazionyeshi kikweli ile huzuni na yale maumivu ya watu mmoja-mmoja wanaohusika. Yvette Pierpaoli, mwakilishi wa Ulaya wa shirika la Refugees International (Wakimbizi wa Kimataifa), aliandika hivi katika gazeti la UM Refugees: “Katika New York au Geneva, swali la wakimbizi laonekana moja kwa moja, tarakimu zinatajwa zenye sufuri nyingi mno [hivi kwamba] ni vigumu kuzifahamu. Lakini maelfu ya maili kutoka hapo, kwenye mipaka ya nchi zenye mchafuko, hisia zako za moyoni zaisonga koo na kule kuteseka kwingi kwakufanya utake kulia kwa nguvu.”

Ingawa shirika la Msalaba Mwekundu lasema kwamba jitihada zalo za kusaidia Somalia zawakilisha utendaji walo mkubwa zaidi wa kutoa msaada wenye huruma, watazamaji wengi wanalalamika kwamba kwa ujumla ni msaada mdogo sana ambao umetolewa, na umetolewa kwa kuchelewa mno. Pierpaoli aomboleza hivi: “Nchi ambazo zimefanya utoaji zinasita kuendelea kuutoa, zikiwa zimechoka kutegemeza Afrika inayoporomoka. . . . Wanawalaumu Waafrika kwa ajili ya usimamizi wao mbaya, pupa ya viongozi wao, mapingano yanayoonekana kuendelea daima.”

Biblia ilitabiri wakati ambapo kungekuwa upungufu wa chakula “mahali mahali.” Upungufu huo wa chakula, pamoja na matukio mengine mengi, kama vile vita, matetemeko ya dunia, na magonjwa ya kipuku, yanaonyesha kwamba Ufalme wa Mungu u karibu. (Luka 21:11, 31) Biblia huendelea kuonyesha kwamba chini ya Ufalme huo wa Mungu wenye ukarimu, kutakuwa na wingi wa chakula kwa ainakibinadamu yote. “Nchi [itazaa] nafaka kwa wingi,” akaandika mtunga-zaburi. “Vilima [vitajaa] mavuno.”—Zaburi 72:16, Habari Njema kwa Watu Wote.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki