Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 4/1 uku. 3
  • Ulimwengu Bora Zaidi—Je! Ni Ndoto Tu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ulimwengu Bora Zaidi—Je! Ni Ndoto Tu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Ulimwengu Bora Zaidi—U Karibu!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Wakaaji wa Nje ya Dunia Hii—Ndoto ya Tangu Kale
    Amkeni!—1990
  • Je, Ndoto Zaweza Kutabiri Wakati Ujao?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Je, Ndoto Ni Ujumbe Kutoka kwa Mungu?
    Amkeni!—2001
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 4/1 uku. 3

Ulimwengu Bora Zaidi—Je! Ni Ndoto Tu?

IKIWA ungalikuwa mfuasi wa dini ya Mazda iliyohubiriwa na nabii wa Iran aitwaye Zoroasta, ungalingojea siku ambayo dunia ingerudia uzuri wayo wa awali. Ikiwa ungaliishi katika Ugiriki ya kale, labda ungaliwazia kufikia kwenye vile Visiwa vya Ufanisi vyenye hali bora au kuona kurudi kwa Enzi Bora iliyosimuliwa na mtunga-mashairi Hesiod katika karne ya nane K.W.K. Mhindi mmoja wa Guaraní katika Amerika Kusini huenda angali akitafuta-tafuta lile Bara Lisilo na Uovu. Hali ukiishi katika wakati wetu, labda watumaini kwamba ulimwengu utaboreka kwa sababu ya mawazo fulani ya kisiasa au kwa sababu ya ufahamu wa mazingira wa ki-siku-hizi.

Enzi Bora, Visiwa vya Ufanisi, Bara Lisilo na Uovu—hayo ni baadhi ya majina mengi yanayotumiwa kueleza tamaa ile moja, tumaini la ulimwengu bora zaidi.

Ulimwengu huu, ulio ulimwengu wetu, si mahali pazuri hata kidogo. Uhalifu unaozidi kuwa wenye ukatili, vita kati ya ndugu na dada vyenye jeuri isiyo na kifani, uuaji wa jamii nzima-nzima za watu, kutojali kuteseka kwa wengine, umaskini na njaa, ukosefu wa kazi ya kuajiriwa na ukosefu wa ushirikiano, matatizo ya kimazingira, magonjwa yasiyotibika yanayowakumba mamilioni ya watu—orodha ya ole zilizopo yaonekana haina mwisho. Akifikiria vile vita vinavyopiganwa wakati huu, mwandishi wa habari mmoja Mwitalia alisema hivi: “Swali lizukalo kiasili ni kama uadui si hisia yenye nguvu zaidi wakati wetu.” Ukifikiria jinsi hali ilivyo, je, wadhani ni jambo lililo halisi kutumainia kuwa na hali tofauti, iliyo bora zaidi? Au kutumainia huko ni kutamani hali ya Utopia (mahali pakamilifu kimawazo) tu, ndoto ambayo haitatimia kamwe? Je! twaishi katika ulimwengu bora zaidi ya mwingine wowote?

Hayo si mahangaiko mapya. Kwa muda wa karne nyingi watu wamekuwa wakiwazia ulimwengu ambamo upatano, haki, ufanisi, na upendo ungekuwa mwingi sana. Baadaye, wanafalsafa kadhaa walieleza kikamili mawazo yao juu ya Majimbo mazuri, mabara mbalimbali yaliyo bora zaidi. Lakini, kwa kuhuzunisha, hawajaweza kamwe kueleza jinsi ya kuyafanikisha.

Je! orodha hiyo ya tangu zamani za kale ya ndoto, Utopia mbalimbali, na matumaini ya wanadamu ya kuwa na jamii iliyo bora zaidi yaweza kutufundisha jambo lolote?

[Picha katika ukurasa wa 3]

Je! huu ndio ulimwengu bora zaidi ya mwingine wowote?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki