Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 9/1 kur. 27-28
  • Je! Vizuizi Hukuvunja Moyo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Vizuizi Hukuvunja Moyo?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ukichwa wa Kimaandiko
  • Vizuizi kwa Vijana
  • Mume Anayejipatia Heshima Nyingi
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Watu Huru Lakini Wanaotakwa Watoe Hesabu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Kutimiza Fungu Letu la Kuendeleza Maisha Yenye Furaha ya Jamaa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Dumisha Amani Nyumbani Mwako
    Siri ya Furaha ya Familia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 9/1 kur. 27-28

Je! Vizuizi Hukuvunja Moyo?

VIZUIZI! Kwa kweli hakuna mtu avipendaye; lakini ni lazima sisi sote tuvivumilie kwa kadiri fulani. Je, nyakati nyingine wewe huvunjika moyo kwa sababu maisha yako yaonekana kama yamezuiwa sana? Labda ungehisi vema zaidi kama ungebadili maoni yako. Badala ya kukasirika kwa sababu ya mambo usiyoweza kufanya, mbona usitumie kwa njia bora zaidi uhuru wowote ulio nao?

Kwa kielelezo, wengi ambao ni maskini kiuchumi hutamani kwamba afadhali wangekuwa matajiri. Lakini, ingawa umaskini hutufanya tusitimize mengi katika mfumo huu wa mambo, mambo yaliyo ya maana maishani yanapatikana kwa wote. Watu walio maskini na vilevile walio matajiri wote hubanwa na mapenzi, hufunga ndoa, hulea watoto, hufurahia urafiki mzuri na kadhalika. La maana zaidi, watu maskini na vilevile walio matajiri wamjua Yehova na hutazamia ulimwengu mpya ulioahidiwa. Watu walio maskini na vilevile matajiri hufanya maendeleo katika hekima na ujuzi wa Kikristo, ulio bora kuliko utajiri. (Mithali 2:1-9; Mhubiri 7:12) Wote—matajiri na maskini—waweza kujifanyia jina zuri kwa Yehova. (Mhubiri 7:1) Katika siku za Paulo kutaniko la Kikristo lilifanyizwa sanasana na watu wa ngazi ya chini—baadhi yao wakiwa watumwa—waliotumia kwa hekima uhuru wowote ulioruhusiwa na hali zao.—1 Wakorintho 1:26-29.

Ukichwa wa Kimaandiko

Katika ndoa ya Kikristo, mke humtii mume wake—mpango uliokusudiwa unufaishe familia nzima. (Waefeso 5:22-24) Je, mke apaswa kuhisi kwamba amedharauliwa kwa sababu ya jambo hilo? La hasha. Mume na mke ni timu. Ukichwa wa mwanamume, ukitumiwa kwa njia ya Kikristo, haumwekei mke wake vizuizi vingi na kumpa fursa nyingi za kutumia uwezo wake vizuri. (Waefeso 5:25, 31) “Mke mwema” wa Mithali sura ya 31 alijishughulisha na mambo mengi yapendezayo na kuhitaji ustadi na bidii. Kwa wazi, utii kwa mume wake haukumfadhaisha.—Mithali 31:10-29.

Vivyo hivyo, mwanamke haruhusiwi kuchukua uongozi juu ya wanaume wanaostahili katika kutaniko la Kikristo. (1 Wakorintho 14:34; 1 Timotheo 2:11, 12) Je, wanawake Wakristo wasiridhike chini ya kizuizi hicho? La. Wengi wanashukuru kuona kwamba upande huo wa utumishi wa Kikristo unashughulikiwa katika njia ya kitheokrasi. Wao wana furaha kunufaika kwa uchungaji na ufundishaji wa wazee waliowekwa rasmi nao hujishughulisha na kazi muhimu ya kuhubiri na kufanya wanafunzi. (Mathayo 24:14; 28:19, 20) Wanawake wa Kikristo hutimiza mengi kwa kazi hiyo, na kufanya hivyo huwaletea staha machoni pa Yehova Mungu.—Zaburi 68:11; Mithali 3:35.

Vizuizi kwa Vijana

Nyakati nyingine vijana pia hulalamika kwamba maisha yao imewekewa vizuizi vingi mno, mara nyingi kwa sababu wao huwa chini ya mamlaka ya wazazi wao. Lakini hilo pia ni jambo la Kimaandiko. (Waefeso 6:1) Badala ya kuudhiwa na vizuizi ambavyo wazazi wao huwawekea, vijana Wakristo wenye hekima huzingatia uhuru wanaopata—mara nyingi kutia ndani uhuru kutokana na madaraka mazito. Hivyo wao waweza kutumia vizuri zaidi nguvu zao za ujana na hali zao kujitayarisha wenyewe kwa ajili ya maisha ya utu mzima.

Mmoja aliyekuwa mwangalizi wa mzunguko nchini Brazili akumbuka sana mvulana mmoja mwenye miaka 12 katika kikundi kidogo kilichokuwa peke yacho aliyekuwa na kizuizi kwa mambo ambayo angefanya. Yule aliyekuwa anasimamia rekodi alikuwa mwenye shughuli katika kazi ya kimwili naye hangeweza kuzingatia sana kikundi hicho, lakini alifanya mpango wa kijana huyo kumsaidia. Alijifunza vizuri akajua fomu zote zilipokuwa na nyakati zote alikuwa tayari kutoa msaada. Upendezi wake ulitia moyo sana, naye alikuwa mwandamani mwaminifu katika utumishi wa shambani. Kijana huyo sasa ni mzee aliyewekwa rasmi.

Kuna hali nyingi zinazoweza kuzuia uhuru wa mtu. Watu wengine huzuiwa na magonjwa. Wengine huishi katika nyumba zilizogawanyika na kupata kwamba uhuru wao umezuiwa na matakwa ya mwenzi asiyeamini. Ingawa wale wanaoishi wakiwa na vizuizi huenda wakatamani kwamba afadhali mambo yangekuwa tofauti, bado wao waweza kuishi maisha yenye kuridhisha. Gazeti hili limekuwa na masimulizi mengi ya watu mmoja-mmoja kama hao ambao wamekuwa wenye kitia-moyo sana kwa wengine kwa sababu walimtegemea Yehova na kutumia vizuri zaidi hali zao.

Akizungumza kuhusu hali iliyokuwa ya kawaida katika siku yake, mtume Paulo alisema: “Je! uliitwa u mtumwa? usione ni vibaya; lakini kama ukiweza kuwa na uhuru, afadhali kuutumia.” (1 Wakorintho 7:21) Hayo ni maoni yaliyosawazika kama nini! Hali nyinginezo hubadilika. Vijana hukua. Nyakati nyingine wenzi wasioamini hukubali kweli. Hali za kiuchumi hubadilika na kuwa bora zaidi. Wagonjwa wanaweza kupata nafuu. Katika hali nyinginezo, huenda hali zisibadilike mpaka ulimwengu mpya wa Yehova ufike. Hata hivyo, utafaidika na nini ukiudhika kwa sababu huwezi kufanya mambo ambayo wengine waweza kufanya?

Je, umepata kuona ndege wakipaa angani juu ya ardhi na kutamani uzuri na uhuru wa miendo yao? Labda ulitamani kwamba ungepaa kama wao. Naam, huwezi na hutaweza kupuruka kama ndege! Lakini yaelekea kwamba hulalamiki. Badala ya hivyo, wewe hushangilia kwa sababu ya uwezo wako mbalimbali uliopewa na Mungu. Hupati tatizo lolote kutembea ardhini. Vivyo hivyo, hali zetu za maishani ziwe nini, tukizingatia akilini mambo tuwezayo kufanya badala ya kuudhika juu ya mambo tusiyoweza kufanya, maisha yataridhisha, nasi tutapata shangwe katika utumishi wa Yehova.—Zaburi 126:5, 6.

[Picha katika ukurasa wa 28]

Je, wahisi kwamba wazazi wako hukuzuia?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki