Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 7/1 kur. 3-4
  • “Kweli Ni Nini?”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Kweli Ni Nini?”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Shambulio Dhidi ya Kweli
  • Itikadi ya Uhusianifu
  • Pontio Pilato Alikuwa Nani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Kwa Nini Utafute Kweli?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Kutoka kwa Pilato Mpaka kwa Herode na Kurudi Tena
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Kutoka kwa Pilato Mpaka kwa Herode na Kurudi Tena
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 7/1 kur. 3-4

“Kweli Ni Nini?”

WATU hawa wawili walioketi wakikabiliana walitofautiana kabisa. Mmoja alikuwa mwanasiasa mwenye madharau, aliyetamani makuu, tajiri, aliye tayari kufanya jambo lolote ili kuendeleza kazi-maisha yake mwenyewe. Yule mwingine alikuwa mwalimu aliyekataa utajiri na umashuhuri naye alikuwa tayari kudhabihu uhai wake ili kuokoa uhai wa wengine. Kwa wazi, watu hawa wawili hawakuwa na maoni sawa! Katika jambo moja hasa, hawakusikilizana kabisa—lile suala la kweli.

Watu hawa walikuwa Pontio Pilato na Yesu Kristo. Yesu alikuwa amesimama mbele ya Pilato akiwa mhalifu mshutumiwa. Kwa nini? Yesu alieleza kwamba sababu ya hilo—kwa kweli, sababu yenyewe iliyomfanya aje duniani na kuanzisha huduma yake—ilikuwa kitu kimoja: kweli. “Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni,” akasema, “ili niishuhudie kweli.”—Yohana 18:37.

Jibu la Pilato lilikuwa swali kubwa sana: “Kweli ni nini?” (Yohana 18:38) Je, hakika alitaka jibu? Labda sivyo. Yesu alikuwa mtu ambaye angejibu swali lolote aliloulizwa kwa unyofu, lakini hakumjibu Pilato. Na Biblia yasema kwamba baada ya kuuliza swali lake, Pilato alitoka mara hiyo nje ya ukumbi wake wa wageni. Yaelekea gavana huyo wa Roma aliuliza swali lake kwa madharau ya kutoamini, kana kwamba kusema, “Kweli? Hiyo ni nini? Hakuna kitu kama hicho!”a

Maoni ya Pilato ya kutilia shaka kweli ni ya kawaida leo. Wengi huamini kwamba kweli ni husianifu—kwa maneno mengine, kwamba jambo lililo kweli kwa mtu mmoja laweza kuwa si kweli kwa mwingine, hivi kwamba wote wawili waweza kuwa “sawa.” Itikadi hii imeenea sana hivi kwamba kuna neno hutumiwa kuihusu—“uhusianifu.” Je, hivyo ndivyo wewe huliona suala la kweli? Ikiwa ndivyo, je, yawezekana kwamba umechukua maoni hayo bila kuyafikiria kwa uzito? Hata kama hujachukua maoni hayo, je, wajua ni kadiri gani falsafa hii huathiri maisha yako?

Shambulio Dhidi ya Kweli

Pontio Pilato hakuwa mtu wa kwanza kutilia shaka wazo la kweli kamili. Wanafalsafa fulani wa kale Wagiriki walifanya kazi-maisha zao kuwa tu kufundisha mashaka hayo! Karne tano kabla ya Pilato, Parmenidi (ambaye ameonwa kuwa mwanzilishi wa metafizikia ya Ulaya) aliamini kwamba ujuzi kamili haungeweza kupatikana. Demokrito, anayeonwa kuwa “mashuhuri zaidi kati ya wanafalsafa wa kale,” alisisitiza hivi: “Kweli imezikwa chini sana. . . . Hatujui lolote kwa hakika.” Labda aliyeheshimiwa zaidi ya wote, Sokrate, alisema kwamba kile alichojua hakika ni kwamba hakujua chochote.

Shambulio hilo kwa wazo la kwamba kweli yaweza kujulikana limeendelea kufikia leo hii. Kwa mfano, baadhi ya wanafalsafa husema kwamba kwa kuwa ujuzi hutufikia kupitia hisi zetu, zinazoweza kudanganywa, hakuna ujuzi ulio kweli uwezao kuthibitishwa. Mwanafalsafa Mfaransa aliye pia mwanahisabati René Descartes aliamua kuchunguza vitu vyote alivyodhani kuwa alivijua kwa hakika. Alitupilia mbali kweli zote isipokuwa moja aliyoona kuwa haiwezi kupingwa: “Cogito ergo sum,” au, “Nafikiri, basi ndivyo.”

Itikadi ya Uhusianifu

Uhusianifu hauaminiwi na wanafalsafa pekee. Unafundishwa na viongozi wa kidini, hukaziwa shuleni, na kuenezwa na vyombo vya habari. Askofu wa Episkopali John S. Spong alisema hivi miaka michache iliyopita: “Ni lazima . . . tuache kufikiri kwamba tuna kweli na lazima wengine wawe na maoni kama yetu na kutambua kwamba hakuna mtu yeyote awezaye kupata kweli kamili.” Uhusianifu wa Spong, kama ule wa makasisi wengi leo, huacha haraka mafundisho ya maadili ya Biblia kwa kupendelea falsafa ya “kila mtu na [maoni] yake.” Kwa kielelezo, katika jitihada ya kufanya wagoni-jinsia-moja kuhisi “starehe” zaidi katika Kanisa la Episkopali, Spong aliandika kitabu akidai kwamba mtume Paulo alikuwa mgoni-jinsia-moja!

Katika nchi nyingi mifumo ya shule huonekana kuleta kufikiri kwa aina hiyo. Allan Bloom aliandika hivi katika kitabu chake The Closing of the American Mind: “Kuna jambo moja ambalo profesa aweza kuwa na hakika kabisa juu yalo: karibu kila mwanafunzi anayeenda chuo kikuu huamini, au husema aamini, kwamba kweli ni husianifu.” Bloom alipata kwamba akipinga itikadi ya wanafunzi wake juu ya suala hili, wao walikuwa wakishtuka, “kana kwamba alikuwa akitilia shaka kwamba 2 + 2 si 4.”

Kufikiri huko kwaendelezwa katika njia nyinginezo nyingi. Mathalani, maripota wa televisheni na magazeti mara nyingi huonekana kupendezwa zaidi na kutumbuiza wasikilizaji wao kuliko kupata ukweli wa jambo fulani. Programu nyinginezo za habari hata zimerekebisha au kutumia filamu bandia ili kuzifanya zionekane zenye kutazamisha zaidi. Na katika vitumbuizo shambulizi kali zaidi linaelekezewa kweli. Kweli za maadili ambazo wazazi wetu na babu na nyanya zetu waliishi kulingana nazo huonwa sana kuwa zisizofaa na mara nyingi hudhihakiwa kabisa.

Bila shaka, wengine huenda wakabisha kwamba uhusianifu wawakilisha kufikiri kwa uhuru na kwa hiyo una uvutano mzuri katika jamii ya kibinadamu. Lakini, je, kweli unafanya hivyo? Na vipi juu ya athari yao kwako? Je, waamini kwamba kweli inahusu tu au hata haipo? Ikiwa ndivyo, unaweza kuona kuitafuta kuwa kupoteza wakati tu. Mtazamo kama huo utaathiri wakati wako ujao.

[Maelezo ya Chini]

a Kulingana na msomi wa Biblia R. C. H. Lenski, “sauti [ya Pilato] ni ile ya mtu asiyejali wa kilimwengu ambaye kwa swali lake akusudia kusema kwamba kitu chochote cha asili ya kweli ya kidini ni kisio bure tu.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki