Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 10/15 kur. 3-4
  • Furaha—Vigumu Kuipata

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Furaha—Vigumu Kuipata
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ufunguo wa Kutokuwa na Furaha
  • Mradi Mgumu Kuufikia
  • Jitihada ya Kutafuta Furaha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Kupata Furaha ya Kweli kunategemea Wewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Je, Mali Zaweza Kukufanya Uwe Mwenye Furaha?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Afya Na Furaha—Waweza Kuzipataje?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 10/15 kur. 3-4

Furaha—Vigumu Kuipata

KWA muda mrefu, hasira, hangaiko, na mshuko-moyo ni mambo ambayo yamefanyiwa uchunguzi na wanasayansi. Hata hivyo, miaka ya majuzi wanasayansi wenye kuongoza wamekuwa wakikazia utafiti wao jambo limpatalo mwanadamu ambalo ni lenye kujenga na kutamanika—furaha.

Ni nini kiwezacho kufanya wanadamu wawe wenye furaha zaidi? Je, watu wangekuwa wenye furaha zaidi ikiwa wangekuwa wachanga zaidi, matajiri zaidi, wenye afya zaidi, warefu zaidi, au wembamba zaidi? Ni nini ulio ufunguo wa kupata furaha ya kweli? Watu walio wengi huliona kuwa jambo gumu au lisilowezekana, kujibu swali hilo. Wakifikiria kule kushindwa kupata furaha kulikoenea sana, labda watu fulani wangeliiona kuwa jambo rahisi zaidi kutoa jibu juu ya lile ambalo si ufunguo wa kupata furaha.

Kwa muda mrefu, wanasaikolojia wenye kuongoza walipendekeza falsafa ikaziayo mahitaji na tamaa za mtu mmoja-mmoja kuwa ufunguo wa kupata furaha. Waliwatia moyo watu wasio na furaha wakazie fikira kutosheleza mahitaji yao wakiwa mtu mmoja-mmoja bila kuhusisha wengine. Mafungu ya maneno yenye kupendwa sana kama vile “uwe mwenye kujifikiria kibinafsi,” “tambua hisia zako za ndani,” na “pata kujua utu wako wa kweli” yametumiwa katika matibabu ya kisaikolojia. Lakini, baadhi ya wale wataalamu wenye kuendeleza njia hiyo ya kufikiri sasa wakubali kwamba mtazamo huo wa kujifikiria binafsi hauleti furaha ya kudumu. Ubinafsi hakika utaleta maumivu na hali ya kutokuwa na furaha. Ubinafsi si ufunguo wa kupata furaha.

Ufunguo wa Kutokuwa na Furaha

Wale ambao hutafuta kupata furaha katika ufuatiaji wa raha wanatafuta mahali pasipofaa. Fikiria kielelezo cha Mfalme Solomoni mwenye hekima wa Israeli la kale. Katika kitabu cha Biblia cha Mhubiri, yeye aeleza hivi: “Sikuyanyima macho yangu cho chote yalichokitamani; wala sikuuzuia moyo wangu katika furaha yo yote; maana moyo wangu ulifurahi kwa sababu ya kazi yangu yote, na hii ilikuwa sehemu yangu katika kazi yangu yote.” (Mhubiri 2:10) Solomoni alijijengea nyumba, akajipandia mashamba ya mizabibu, akajifanyizia bustani, viunga, na birika za maji. (Mhubiri 2:4-6) Wakati mmoja aliuliza hivi: “Ni nani awezaye kula au kujiburudisha kuliko mimi?” (Mhubiri 2:25) Alitumbuizwa na waimbaji na wanamuziki walio bora zaidi, na alionea shangwe kuandamana na wanawake waliokuwa warembo zaidi nchini.—Mhubiri 2:8.

Hoja ni, Solomoni hakujizuia ilipohusu utendaji mbalimbali wenye raha. Alifikia mkataa gani baada ya kupata raha nyingi maishani? Alisema hivi: “Nikaziangalia kazi zote zilizofanywa kwa mikono yangu, na taabu yote niliyotaabika katika kuzitenda; na tazama, yote ni ubatili na kujilisha upepo, wala faida hakuna chini ya jua.”—Mhubiri 2:11.

Matokeo ya uchunguzi wa huyo mfalme mwenye hekima yabaki yakiwa sahihi hadi siku hii. Mathalani, fikiria nchi yenye mali kama Marekani. Wakati wa miaka 30 iliyopita, Wamarekani wameongeza kwa karibu maradufu idadi ya mali zao za kimwili, kama vile magari na televisheni. Lakini, kulingana na wataalamu wa afya ya kiakili, Wamarekani hawana furaha zaidi kwa vyovyote. Kulingana na chanzo kimoja, “viwango vya mshuko-moyo vimeongezeka sana katika kipindi hichohicho. Kujiua kwa matineja kumeongezeka mara tatu. Viwango vya talaka vimeongezeka maradufu.” Hivi majuzi watafiti wamefikia mikataa hiyohiyo baada ya kuchunguza uhusiano kati ya fedha na furaha miongoni mwa idadi ya watu wa nchi tofauti-tofauti zipatazo 50. Kwa kusema kisahili, huwezi kununua furaha.

Kinyume cha hilo, ule ufuatiaji wa mali ungeweza kwa kufaa kuitwa ufunguo wa kutokuwa na furaha. Mtume Paulo alionya hivi: “Wale waazimiao kuwa matajiri huanguka ndani ya kishawishi na mtego na tamaa nyingi zisizo za akili na zenye kuumiza, ambazo hutumbukiza watu ndani ya uharibifu na uangamizo. Kwa maana kupenda fedha ni mzizi wa mambo mabaya ya namna zote, na kwa kujitahidi kufikilia kupenda huku wengine wameongozwa wapotee njia kutoka kwenye imani na wamejichoma wenyewe kotekote kwa maumivu mengi.”—1 Timotheo 6:9, 10.

Furaha ya kudumu haiwezi kuhakikishwa na mali, wala afya, wala ujana, wala uzuri, wala nguvu, wala kuunganishwa kokote kwa vitu hivyo. Kwa nini isiwe hivyo? Kwa sababu hatuna nguvu za kuzuia mambo mabaya yasitukie. Mfalme Solomoni alisema hivi kwa kufaa: “Mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafula.”—Mhubiri 9:12.

Mradi Mgumu Kuufikia

Hakuna kiasi chochote cha utafiti wa kisayansi kiwezacho kutokeza njia au mkakati wa kupata furaha. Solomoni alisema hivi pia: “Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati [“tukio lisilotazamiwa,” NW] huwapata wote.”—Mhubiri 9:11.

Wengi ambao hukubaliana na maneno yaliyo juu wamekata kauli kwamba kutarajia maisha yenye furaha kikweli ni jambo lisilo la kihalisi. Mwelimishaji mmoja mashuhuri alitaarifu kwamba “furaha ni hali ya kuwaziwa.” Watu wengine huamini kwamba ufunguo wa kupata furaha ni siri iliyo fumbo, kwamba uwezo wa kufumbua hiyo siri huenda ukapatikana kwa waamini-mafumbo wachache wenye kipawa cha akili.

Hata hivyo, katika kutafuta kwao furaha, watu waendelea kujaribu mitindo-maisha ya namna mbalimbali. Kujapokuwa kushindwa kwa waliowatangulia, wengi leo bado hufuatia mali, ukuu, afya, au raha kuwa ponyo la hali yao ya kutokuwa na furaha. Huo utafutaji waendelea kwa sababu kindani kabisa, watu walio wengi huamini kwamba furaha ya kudumu si hali ya kuwaziwa tu. Wao hutumaini kwamba furaha si ndoto iliyo ngumu kupata. Basi huenda ukauliza, ‘Naweza kuipataje?’

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki