Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 8/1 uku. 30
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Yesu Amponya Mvulana Mwenye Roho Mwovu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Mvulana Mwenye Kupagawa na Roho Mwovu Aponywa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Mvulana Mwenye Kupagawa na Shetani Aponywa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 8/1 uku. 30

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Kulingana na Mathayo 17:20, mitume walishindwa kumponya mvulana aliyekuwa anateseka ‘kwa sababu ya imani yao kidogo.’ Hata hivyo, kwenye Marko 9:29, kushindwa kwao kwahusianishwa na uhitaji wa sala. Kwa nini sababu tofauti zinatolewa katika masimulizi tofauti ya Gospeli?

Kwa hakika, masimulizi hayo mawili ni yenye kutegemezana, wala hayahitilafiani. Kwanza, angalia Mathayo 17:14-20. Mtu fulani aliripoti kwamba mwana wake alikuwa na kifafa lakini wanafunzi wa Yesu hawakuweza kumponya huyo mvulana. Ndipo Yesu akamponya mvulana huyo kwa kumfukuza roho mwovu aliyekuwa akimtesa. Wanafunzi waliuliza ni kwa nini hawakuweza kumfukuza huyo roho mwovu. Kulingana na simulizi la Mathayo, Yesu alijibu hivi: “Kwa sababu ya imani yenu kidogo, kwa maana kwa kweli nawaambia nyinyi, Mkiwa na imani yenye ukubwa wa punje ya haradali, mtaambia mlima huu ‘Hama kutoka hapa hadi pale,’ nao utahama, na hakuna jambo litakalokuwa haliwezekani kwenu.”

Sasa fungua Marko 9:14-29, ambapo twapata habari zaidi. Kwa mfano, andiko la Marko 9:17 latoa habari kwamba katika kisa hiki kule kukamatwa na kifafa kulisababishwa na roho mwovu. Yafaa ifahamike kwamba Biblia yasema penginepo kwamba Yesu aliponya watu wenye kifafa na walio na roho waovu. (Mathayo 4:24) Katika kisa hiki kisicho cha kawaida, kushikwa huko kulisababishwa na ‘roho asiyesema na aliye kiziwi,’ ambaye tabibu Luka amthibitisha kuwa roho mwovu. (Luka 9:39; Wakolosai 4:14) Ona kwenye Marko 9:18 lile fungu la maneno, “Popote pale [huyo roho mwovu] amkamatapo.” Kwa hiyo kijana huyo hakuwa akisumbuliwa mfululizo na huyo roho mwovu, bali alisumbuliwa pindi kwa pindi tu. Hata hivyo, wanafunzi hawakuweza kumfukuza huyo roho mwovu na hivyo kumponya mvulana huyo. Walipouliza ni kwa nini, Yesu aliwajibu hivi: “Aina hii haiwezi kutoka kwa chochote ila kwa sala.”

Ingawa hivyo, usomaji wa makini wa simulizi la Marko, huonyesha kwamba halihitilafiani na yale aliyorekodi Mathayo. Kwenye Marko 9:19, twasoma kwamba Yesu alisikitikia ukosefu wa imani wa kizazi hicho. Na katika mstari wa 23, imerekodiwa kwamba alimwambia baba ya mvulana huyo hivi: “Mambo yote yaweza kuwa kwa mtu ikiwa ana imani.” Kwa hiyo Marko pia akazia umuhimu wa imani. Ni kwamba tu katika mstari wa 29, Marko anatokeza jambo la ziada. Marko aongeza yale Yesu aliyosema kuhusu sala, ambayo wala Mathayo wala Luka hawakutia ndani.

Twaweza kusema nini basi? Katika pindi nyingine mitume 12 na pia wanafunzi 70 walifukuza roho waovu. (Marko 3:15; 6:13; Luka 10:17) Lakini katika kisa hiki wanafunzi hawakuweza kumfukuza huyo roho mwovu. Kwa nini? Tukijumlisha habari zote zilizotajwa katika masimulizi mbalimbali, twapaswa kufikia mkataa kwamba, katika kisa hicho hawakuwa tayari kufanya hivyo. Labda sehemu moja ya tatizo hilo ilihusisha aina ya roho mwovu aliyehusika, kwa kuwa yaonekana kwamba huenda roho waovu wakawa na nyutu, mapendezi na hata uwezo mbalimbali. Kuhusiana na huyo, hasa imani yenye nguvu na sala yenye bidii kwa ajili ya msaada wa Mungu ilihitajika. Bila shaka, Yesu alikuwa na imani hiyo. Pia alikuwa na utegemezo wa Baba yake, aliye Msikiaji wa sala. (Zaburi 65:2) Yesu angeweza kumponya mvulana aliyekuwa anateseka kwa kumfukuza roho mwovu, na alifanya hivyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki