Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w06 3/15 uku. 3
  • Kifo Kinaogopesha!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kifo Kinaogopesha!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Msaada kwa Kihoro Chako
    Amkeni!—1994
  • Epuka Kujitakia Makuu!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Absalomu Aliasi kwa Sababu ya Kiburi
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
  • Wewe Unajua Kuvumilia Huzuni Nyingi?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
w06 3/15 uku. 3

Kifo Kinaogopesha!

“KUANZIA wakati mwanadamu anapozaliwa kuna uwezekano wa kwamba anaweza kufa wakati wowote,” akaandika mwanahistoria Mwingereza, Arnold Toynbee. Aliongeza hivi: “Ni wazi kwamba kila mtu atakufa mwishowe.” Kifo huleta huzuni nyingi sana wakati mtu wa familia tunayempenda sana au rafiki wa karibu anapokufa!

Kifo kimewaogopesha wanadamu kwa maelfu ya miaka. Sisi huwa hoi mpendwa wetu anapokufa. Isitoshe, watu wote hupatwa na huzuni inayosababishwa na kifo. Hakuna mtu anayeweza kuepuka kifo. “Hata iwe tuna elimu au hatuna, huzuni hutufanya tuwe kama watoto wadogo na hututatanisha. Hata wenye hekima hushindwa la kufanya.” Ndivyo alivyoandika mwandishi wa karne ya 19. Kifo hutufanya tuwe kama watoto wadogo walio hoi ambao hawana uwezo wa kubadili mambo. Hasara inayosababishwa na kifo haiwezi kuondolewa na mali wala mamlaka. Wenye hekima na wenye akili hawawezi kufanya lolote. Wote hulia, wawe wenye nguvu au dhaifu.

Mfalme Daudi wa Israeli la kale alihisi hivyo wakati Absalomu mwana wake alipokufa. Alipopata habari kwamba mwana wake amekufa, mfalme alianza kulia na kusema hivi: “Mwanangu Absalomu, mwanangu, mwanangu Absalomu! Laiti mimi mwenyewe ningekufa badala yako, Absalomu mwanangu, mwanangu!” (2 Samweli 18:33) Mfalme huyo mwenye nguvu aliyekuwa ameshinda maadui wenye nguvu alijihisi hoi na kutamani kwamba ni afadhali yeye mwenyewe angeshindwa na ‘adui wa mwisho, kifo,’ badala ya mwana wake.—1 Wakorintho 15:26.

Je, kuna suluhisho la kifo? Ikiwa lipo, wafu wana tumaini gani? Je, tutaweza kuwaona tena wapendwa wetu? Makala inayofuata inatoa majibu ya Kimaandiko kwa maswali hayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki