Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w06 7/1 uku. 31
  • Imani Yake Huwatia Wengine Moyo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Imani Yake Huwatia Wengine Moyo
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Athawabishwa Baada ya Kutafuta kwa Muda Mrefu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • “Sijawahi Kamwe Kuhisi Upendo Kama Huu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • “Nimeshika Imani”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Hata Pafu la Chuma Halikumzuia Kuhubiri
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
w06 7/1 uku. 31

Imani Yake Huwatia Wengine Moyo

SILVIA alipozaliwa Desemba 1992, alionekana kuwa msichana mwenye afya nzuri kabisa. Lakini alipokuwa na umri wa miaka miwili, iligunduliwa kwamba anaugua ugonjwa fulani (cystic fibrosis) ambao hauna tiba. Hatua kwa hatua ugonjwa huo husababisha matatizo makubwa ya kupumua na ya kusaga chakula. Ili kukabiliana nao, Silvia humeza tembe 36 kila siku, hutumia dawa za kuvuta pumzi, na kupata matibabu ya viungo. Kwa kuwa mapafu yake hufanya kazi kwa asilimia 25 tu ya kiwango cha kawaida, ni lazima atumie kifaa chenye oksijeni, hata anapoondoka nyumbani.

“Inashangaza jinsi Silvia anavyokabiliana na ugonjwa huo,” anasema Teresa, mama yake. “Imani yake ni thabiti kwa sababu ya ujuzi wake wa Maandiko. Imani hiyo humsaidia kukabiliana na huzuni na maumivu. Sikuzote yeye hukumbuka ahadi ya Yehova ya ulimwengu mpya, ambamo wagonjwa wote wataponywa.” (Ufunuo 21:4) Nyakati nyingine familia yao inapovunjika moyo, Silvia huwatia moyo anapotabasamu. Yeye huwaambia wazazi wake na ndugu yake hivi: “Uzima katika ulimwengu mpya utatufanya tusahau matatizo yote tunayopata sasa.”

Silvia huwahubiria watu kwa ukawaida kuhusu habari njema ya Neno la Mungu, na watu hao huona uso wake uking’aa kwa furaha na shangwe. Washiriki wa kutaniko la Kikristo ambako yeye huhudhuria mikutano katika Visiwa vya Canary hufurahia pia kusikia maelezo yake mikutanoni. Isitoshe, baada ya kila mkutano, Silvia hutenga wakati kuzungumza na ndugu na dada zake Wakristo. Uchangamfu na urafiki wake umewachochea wote kutanikoni kumpenda.

Antonio, baba yake, anasema hivi: “Silvia hutufundisha jambo muhimu sana. Hata tukiwa na matatizo, uhai ni zawadi kutoka kwa Mungu, nasi tunapaswa kuuthamini.” Kama Silvia, watumishi wote wa Mungu, vijana kwa wazee, wanangojea kwa hamu wakati ambapo “hakuna mkaaji atakayesema: ‘Mimi ni mgonjwa.’”—Isaya 33:24.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Silvia anasoma mstari katika Biblia huku mama yake akibeba kifaa chenye oksijeni

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki