Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w15 4/1 uku. 15
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Habari Zinazolingana
  • Imani Kubwa ya Ofisa wa Jeshi
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Yule Amiri-Mia Mroma Mwenye Fadhili
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Yehova Huona Nini Anaponitazama?
    Huduma Yetu ya Ufalme—2014
  • “Endeleeni Kutahini Kama Nyinyi Mmo Katika Imani”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
w15 4/1 uku. 15

JE, WAJUA?

Ofisa katika jeshi la Roma alikuwa na daraka gani?

Sanamu ya ofisa jeshi wa Roma

Jiwe la ofisa-jeshi Marcus Favonius Facilis

Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo yanarejelea mara kadhaa kuhusu maofisa wa Kiroma. Ofisa jeshi aliyesimamia mauaji ya Yesu na pia Kornelio aliyekuwa Mtu wa Mataifa wa kwanza kukubali Ukristo. Ofisa aliyeamuru mtume Paulo apigwe mijeledi na Yulio aliyekabidhiwa Paulo ili ampeleke Roma, walikuwa pia maofisa-jeshi.—Marko 15:39; Matendo 10:1; 22:25; 27:1.

Kwa kawaida, ofisa-jeshi alisimamia kikosi kilichokuwa na askari wa miguu kati ya 50 na 100. Majukumu yake yalitia ndani kuwazoeza na kuwatia nidhamu, kukagua mavazi na vifaa vyao na pia kusimamia shughuli zao za kijeshi.

Cheo cha ofisa jeshi kilikuwa cheo cha juu zaidi ambacho askari wa kawaida angefikia. Wale waliofikia cheo hicho walipaswa kuwa askari waliozoezwa na pia viongozi wazuri. Ufanisi na nidhamu ya jeshi la Roma ulitegemea uongozi wao. Chanzo kimoja kinasema kwamba maofisa-jeshi ‘walikuwa wenye uzoefu zaidi na wenye ujuzi mwingi katika jeshi la Roma.’

Vioo vya nyakati za Biblia vina tofauti gani na vioo vya leo?

Kioo cha zamani kutoka Misri

Kioo cha zamani kutoka Misri

Tofauti na vioo vya leo, vioo vya nyakati za Biblia vilitengenezwa kwa chuma iliyong’arishwa sana, kwa kawaida, shaba, hasa shaba nyekundu, fedha, dhahabu, mchanganyiko wa dhahabu na fedha. Vioo vinatajwa kwa mara ya kwanza katika Biblia katika maelezo ya ujenzi wa maskani yaliyotumiwa kwa mara ya kwanza na Waisraeli yakiwa kitovu cha ibada. Wanawake walitoa vioo vikiwa michango katika ujenzi wa beseni ya shaba na kinara chake. (Kutoka 38:8) Huenda vioo hivyo vilihitaji kuyeyushwa ili vitumiwe katika ujenzi huo.

Uvumbuzi wa vitu vya kale katika eneo linalozunguka Israeli, umeonyesha kwamba vioo vya kale vilipatikana pamoja na vito na vitu vingine vya mapambo ya kike. Vioo hivyo vilikuwa na umbo la mviringo na kishikio chake kilitengenezwa kwa mbao, chuma au pembe ya ndovu, na kilikuwa na umbo kama la mwanamke. Sehemu isiyong’arishwa ya kioo hicho haikurembeshwa.

Vioo hivyo havikung’aa waziwazi vikilinganishwa na vioo vya sasa. Huenda mtume Paulo alirejelea vioo vya aina hiyo aliposema hivi: “Sasa tunaona kwa njia isiyo ya waziwazi kupitia kioo cha chuma.”—1 Wakorintho 13:12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki