Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp19 Na. 2 uku. 3
  • Unapohisi Umechoshwa na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unapohisi Umechoshwa na Maisha
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
  • Habari Zinazolingana
  • Unapohisi Umelemewa na Hali Ngumu Maishani
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2023
  • Unapofiwa na Mtu Unayempenda
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
  • Janga la Asili Linapotokea
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
  • Majanga Yanapotokea
    Amkeni!—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
wp19 Na. 2 uku. 3
Mwanamke analia akiwa kazini

Unapohisi Umechoshwa na Maisha

HALI zinapokuwa shwari, maisha huwa mazuri sana. Lakini nyakati fulani, matatizo yanaweza kufanya tuhisi tumechoshwa na maisha.

Kwa mfano, Sally,a anayeishi Marekani, alisema hivi baada ya kimbunga kuharibu karibu kila kitu alichokuwa nacho: “Sikuwa na nguvu za kuendelea kupambana. Mara kwa mara nilihisi nikiwa karibu kabisa kukata tamaa.”

Au namna gani ukifiwa na mtu unayempenda? Janice, anayeishi Australia, anasema: “Baada ya kufiwa na wanangu wote wawili, nilipoteza kabisa mwelekeo wa maisha, hivyo ilibidi nianze kujikusanya upya. Nilimsihi Mungu na kumwambia: ‘Nimechoka! Tafadhali niache tu nipumzike. Sitaki kuamka tena.’”

Kwa upande mwingine, Daniel alichanganyikiwa sana mke wake alipofanya uzinzi. Anasema: “Mke wangu aliponiambia amefanya uzinzi, nilihisi kama nimechomwa kisu moyoni. Nilihisi maumivu makali yakinichoma tena na tena—na hali hiyo iliendelea kwa miezi kadhaa.”

Katika toleo hili la Mnara wa Mlinzi tutachunguza sababu za kutokata tamaa hata

  • Unapokumbwa na janga la asili

  • Unapofiwa na mtu unayempenda

  • Mwenzi wa ndoa anapofanya uzinzi

  • Unapokuwa na ugonjwa mbaya

  • Unapohisi umelemewa na unatamani kufa

Kwanza, tuzungumzie jinsi tunavyoweza kuvumilia tunapokumbwa na janga la asili.

a Baadhi ya majina katika makala za toleo hili yamebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki