Kutangaza Habari Njema Kuonyesha Mnara wa Mlinzi
1Kwa nguvu sana Biblia inasihi aina ya binadamu watafute maarifa ya Mungu na ya Mwanaye, Yesu Kristo. Maarifa haya ni yenye thamani zaidi ya dhahabu au fedha. (Mit. 8:10) Kwa nini? Kwa sababu maarifa hayo sahihi yanaongoza kwenye uhai wa milele. (Yoh. 17:3) Hata hivyo, maarifa sahihi hayapatikani au kudumishwa pasipo jitihada kubwa ya kibinafsi. Si ajabu kwamba Sulemani alisema: “Ukiutafuta . . . ndipo utakapofahamu kumcha BWANA [Yehova, NW], na kupata kumjua Mungu.”—Mit. 1:7, 2:4, 5.
2Ulimwengu wa aina ya binadamu umo gizani kwa habari ya makusudi ya Mungu, lakini maarifa ya Yehova yaliyo bora sana yanatujia kupitia makala zenye thamani na za wakati unaofaa zinazochapishwa katika Mnara wa Mlinzi. (Isa. 60:2) Ni pendeleo lililoje tulilo nalo kushiriki pamoja na wengine habari hii ya muhimu! Wakati wa Aprili na Mei, mfululizo wa makala kuhusu kufunuliwa wazi kwa Babuloni Mkubwa na kufishwa kwake zitazungumziwa.
TUNAWEZA KUKAZIA NINI?
3Matoleo ya Aprili ya Mnara wa Mlinzi yanachunguza utambulishi wa “Babuloni Mkubwa, mama ya makahaba.” (Ufu. 17:5, NW) Baada ya kujijulisha, amsha udadisi wa mwenye nyumba katika makala haya kwa kuuliza maswali yenye kufanya afikiri kama vile: Huyu Babuloni anafananisha nini? Babuloni Mkubwa ni nani? Kwa nini analaumiwa kwa maneno makali sana katika Biblia? Uharibifu wake utaathirije kizazi chetu na wakati wako ujao? Kwa kutojibu maswali hayo unaweza kuelekezewa fikira na mtu mmoja mmoja.
4Ikiwa kundi lenu bado halijapokea matoleo haya mazuri basi kwa mafanikio yanayolingana na hayo mnaweza kutoa matoleo ya karibuni yanayopatikana ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Kwa kielelezo, matoleo ya Februari yanaonyesha makala za Ukumbusho kuhusu agano na habari za hotuba ya watu wote kutoka mkusanyiko wetu wa wilaya wa karibuni juu ya “Haki kwa Ajili ya Wote Kupitia Hakimu Mwekwa wa Mungu.” Siku ya magazeti hakikisha unakazia fikira kufanya utoaji mfupi usiozidi sekunde 60.
5Aprili utaanza kampeni mpya ya uandikishaji wa Mnara wa Mlinzi. Tofauti na utoaji mfupi unaopendekezwa kwa siku ya kila juma ya kutoa magazeti, tutataka kutumia Kichwa cha Mazungumzo tunapotoa uandikishaji. Wale wasiotaka kuandikisha magazeti wanapasa kutiwa moyo wakubali matoleo ya karibuni ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni!
6Je! wewe unathamini kikamili thamani inayozidi ya Mnara wa Mlinzi? Ni kifaa chenye umaana cha kuelimisha aina ya binadamu katika njia za Yehova za uadilifu. (Mt. 5:6) Katika kugawanya jarida hili lenye kutokeza, tuna pendeleo la kuonya mataifa juu ya uharibifu unaokaribia wa Babuloni Mkubwa.