Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Pitio vitabu vikiwa vimefungwa la habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Januari 6 hadi Aprili 20, 1992. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Angalia: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila moja ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Chini ya Sheria ya Musa, dhambi na watenda dhambi wote walionwa kwa hali ile ile. [si uku. 29 fu. 34 (Chapa ya 1983., uku. 29 fu. 34)]
2. Jina Hesabu linarejezea kuhesabu watu kulikotukia kwenye Mlima Sinai na baadaye kwenye Nyanda za Moabu. [si uku. 30 fu. 2 (uku. 30 fu. 2)]
3. Ijapokuwa Hesabu ni mfano bora katika unyoofu, Musa alificha kupungukiwa kwake mwenyewe. [si uku. 31 fu. 7 (uku. 31 fu. 7)]
4. Chini ya agano la Sheria, siku zote dhambi ilitaka dhabihu ya kupatanisha, ungamo, toba, na kufanya marekebisho kwa kadiri iwezekanavyo. [si uku. 29 fu. 32 (uku. 29 fu. 32)]
5. Ile ‘laana ya peupe’ ilikuwa kwa kweli ni ukufuru. (Law. 5:1) [Usomaji Biblia kila juma; ona w87-SW 9/1 uku. 13.]
6. Kutoa dhabihu ya ng’ombe dume kwa kuhani mkuu kuwa toleo la dhambi “kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe, na kwa ajili ya nyumba yake” kulifananisha dhabihu ya Yesu kama inavyotumika kwa “nyumba yake” ya makuhani wa chini. (Law. 16:6) [Usomaji Biblia kila juma; ona w87-SW 3/1 uku. 28.]
7. Si vema kamwe kumtoza ndugu riba (faida). (Law. 25:35-37) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 2/15 uku. 30 au w84-SW 9/1 uku. 22.]
8. Sheria zilizohusu kutakaswa kwa wenye ukoma na nyumba zilizoambukizwa magonjwa zilionyesha ufahamu wa viini vya magonjwa na kulinda dhidi ya maambukizo. (Law., sura 14) [Usomaji Biblia kila juma; ona g81 9/22 uku. 25.]
9. Katikati au juu ya makerubi waliokuwa juu ya kifuniko cha sanduku la agano, kulitokea ile taa ya Shekina ya kimuujiza ikiwa ufananisho wa kuwapo kwa Mungu katika Patakatifu Zaidi. (Hes. 7:89) [Usomaji Biblia kila juma; ona kj uku. 165.]
10. Waisraeli walipaswa kufanya “vishada katika ncha” za nguo zao ili kwamba wasifanane na Wamoabu, Wamisri, au wengine na ili wakumbushwe kwamba walikuwa tofauti. (Hes. 15:38-40) [Usomaji Biblia kila juma; ona w83 10/15 uku. 20 au w84-SW 3/15 uku. 18.]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Mambo ya Walawi chaadhimishaje jina la Yehova? [si uku. 26 fu. 9 (uku. 26 fu. 9)]
12. Ni kazi gani ya kikuhani itakayotimizwa na Kuhani Mkuu, Yesu Kristo, na makuhani wa chini wake katika kipindi cha Utawala wa Miaka Elfu? [si uku. 30 fu. 39 (uku. 30 fu. 39)]
13. Katazo la kula mafuta linawakumbusha watumishi wa Yehova nini leo? (Law. 3:17) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 2/15 uku. 29 au w84-SW 9/1 uku. 21.]
14. Ni nini huenda ikawa ilihusika katika dhambi ya Nadabu na Abihu? (Law. 10:1, 2) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 2/15 uku. 29 au w84-SW 9/1 uku. 22.]
15. Kwa nini kuzaa mtoto kulimfanya mwanamke “najisi” (mchafu)? (Law. 12:2, 5) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 2/15 uku. 29 au w84-SW 9/1 uku. 22.]
16. Kwa nini adhabu ya kifo iliamriwa kwa yeyote ‘aliyelaani’ wazazi wake? (Law. 20:9) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 2/15 kur. 29-30 au w84-SW 9/1 uku. 22.]
17. Ni nini linalomaanishwa na ‘wanawake kumi kuoka mkate katika tanuu moja’? (Law. 26:26) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 2/15 uku. 30 au w84-SW 9/1 uku. 22.]
18. Kwa nini Miriamu aliongea dhidi ya Musa kwa sababu ya mke wa Musa Mkushi? (Hes. 12:1) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 4/15 uku. 29 au w84-SW 10/15 kur. 23-24.]
19. Ni jambo gani la maana alilopuuza Kora? (Hes. 16:1-3) [Usomaji Biblia kila juma; ona w78 11/15 uku. 14.]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila ya taarifa zifuatazo:
20. Mambo ya Walawi kiliandikwa na Musa katika mwaka wa . [si uku. 25 fu. 4 (uku. 25 fu. 4)]
21. Kichwa kikuu cha chaendelea kotekote katika Mambo ya Walawi, nacho chataja takwa hilo kuliko kitabu kinginecho chote cha Biblia. [si uku. 26 fu. 9 (uku. 26 fu. 9)]
22. Utimizo mbalimbali wa vifananisho vingi vya kiunabii katika Mambo ya Walawi unaelezwa katika kitabu cha . [si uku. 29 fu. 37 (uku. 29 fu. 37)]
23. Kitabu cha Hesabu chahusisha kipindi cha wakati kuanzia hadi K.W.K. [si uku. 30 fu. 4 (uku. 30 fu. 4)]
24. Katika kitabu cha Hesabu, mwendo wa Israeli wa kutokutii na wa uasi unatumiwa ili kukazia uhitaji muhimu . [si uku. 31 fu. 9 (uku. 31 fu. 9)]
25. Amri zilizo katika Mambo ya Walawi kuhusu hufunua maarifa ya mambo ya hakika ambayo hayakuthaminiwa na wanatiba wa kilimwengu mpaka maelfu ya miaka mingi baadaye. [si uku. 26 fu. 7 (uku. 26 fu. 7)]
Chagua jibu sahihi katika kila ya taarifa zifuatazo:
26. Kitabu cha Mambo ya Walawi chahusisha muda wa (miaka 40; mwaka mmoja; mwezi mmoja). [si uku. 25 fu. 3 (uku. 25 fu. 3)]
27. Kitabu cha Hesabu kilimalizwa na Musa katika mwaka wa (1513; 1512; 1473) K.W.K. [si uku. 30 fu. 4 (uku. 30 fu. 4)]
28. ‘Kutaabisha nafsi’ kwa wazi kulirejezea (kufunga; kujipiga mwenyewe; kujizuia kutokana na tafrija zozote). (Law. 16:29) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 2/15 uku. 29 au w84-SW 9/1 uku. 22.]
29. ‘Kupooza paja’ kwa mwanamke kulimaanisha hasa kwamba (angeacha kumtumikia Yehova; mguu wake ungeacha kufanya kazi; viungo vyake vya uzazi vingekwisha nguvu, na kufanya asiweze kuchukua mimba). (Hes. 5:21) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 4/15 uku. 29 au w84-SW 10/15 uku. 23.]
30. “Kitabu cha vita vya Yehova” kilikuwa (mambo ya uasi-imani; rekodi ya kihistoria yenye kutegemeka; masimulizi yaliyotungwa ya hadithi za Biblia). (Hes. 21:14, 15) [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 4/15 uku. 30 au w84-SW 10/15 uku. 24.]
Linganisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Law. 2:11, 12; Law. 17:10-14; Law. 19:32; Hes. 15:30, 31; Ebr. 13:11
31. Kwa sababu damu ni takatifu haiwezi kutwaliwa mwilini katika namna yoyote. [si uku. 29 fu. 38 (uku. 29 fu. 33)]
32. Katika Siku ya Upatanisho mizoga ya wanyama kwa ajili ya dhambi ilipelekwa nje ya kambi na kuteketezwa. [si uku. 29 fu. 38 (uku.29 fu. 38)]
33. Wakati “asali” ilipomaanisha maji ya matunda, basi ingeweza kuchacha na hivyo, isingekubalika kuwa dhabihu. [Usomaji Biblia kila juma; ona w84 2/15 uku. 29 au w84-SW 9/1 uku. 21.]
34. Heshima kwa watu wazee ilikuwa sera ya kitaifa katika Israeli. [Usomaji Biblia kila juma; ona w87-SW 6/1 uku. 5.]
35. Wavunja sheria ya Mungu kwa kusudi bila kutubu, waliuawa. [Usomaji Biblia kila juma; ona w91-SW 4/15 uku. 15.]