Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/98 kur. 5-6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1998
Huduma Yetu ya Ufalme—1998
km 12/98 kur. 5-6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Septemba 7 hadi Desemba 21, 1998. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Kwenye 2 Timotheo 1:6, “zawadi” hurejezea uwezo wa kusema katika lugha mbalimbali ambazo Timotheo alikuwa amepewa kupitia utendaji wa roho takatifu ya Mungu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w85-E 5/1 uku. 16 fu. 15.]

2. Mkristo aliyekomaa ‘huzoeza nguvu zake za ufahamu kutofautisha lililo sahihi na lililo kosa’ kwa kulifanya liwe zoea kutumia ujuzi wowote ule alio nao wa Neno la Mungu. (Ebr. 5:14) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-E 2/1 uku. 22 fu. 7.]

3. Ijapokuwa huenda ikawa Mashahidi wa Yehova wamesajiliwa na serikali kuwa shirika la kidini, bila shaka idhini ya kuendelea na ibada ya kweli haitokani na mwanadamu yeyote au serikali yoyote ya kibinadamu. [jv-SW uku. 696 fu. 1]

4. Mwandikaji wa Biblia Yakobo ni Yakobo yuleyule aliyekuwa msemaji kwa ajili ya “mitume na wazee” wakati wa uamuzi kuhusu tohara. (Mdo. 15:6, 13; Yak. 1:1) [si-SW uku. 248 fu. 2-3]

5. Ijapokuwa 1 Petro 5:13 husema kwamba Petro alikuwa Babiloni alipoandika barua yake ya kwanza, uthibitisho waonyesha kwamba jina Babiloni ni jina la siri linalorejezea Roma. [si-SW uku. 252 fu. 4]

6. Msemo “mpinga-Kristo anakuja” kwenye 1 Yohana 2:18 hurejezea mtu mmoja. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona rs-SW uku. 212 fu. 3.]

7. Amri iliyo kwenye 2 Yohana 10 ya kutopokea nyumbani kwa mtu au kusalimu watu fulani hurejezea watu ambao huendeleza mafundisho yasiyo ya kweli. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w86-SW 1/15 uku. 29 fu. 1-3.]

8. Kitabu cha Ufunuo kimewekwa kuwa cha mwisho katika Biblia, kwa sababu ndicho kilikuwa kitabu cha mwisho kuandikwa na mtume Yohana. [si-SW uku. 263 fu. 1]

9. Ufunuo 13:11-15 hufananisha kwa usahihi jinsi Serikali ya Ulimwengu ya Uingereza na Amerika ilivyokuja kuwa mdhamini mkuu na mpaji wa uhai kwa Shirika la Mataifa na mwandamizi wake, Umoja wa Mataifa. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 12/15 uku. 19 fu. 3.]

10. Amri ya kupendana, iliyoandikwa kwenye Yohana 13:34, ilikuwa “amri mpya” kwa sababu ilikuwa mpya zaidi kuliko Sheria ya Kimusa. [jv-SW uku. 711 fu. 3]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Yamaanisha nini kwamba mwangalizi lazima asiwe “mpiga-watu”? (Tito 1:7) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 9/1 uku. 27 fu. 21.]

12. Ni maneno gani ya msingi yaliyo kwenye 1 Yohana 2:2 ambayo hutusaidia tutambue vikundi viwili ambavyo vyanufaika na kifo cha kujidhabihu cha Yesu? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 1/15 uku. 12 fu. 11.]

13. Yesu alimaanisha nini aliposema, “Dhabihu na toleo hukutaka”? (Ebr. 10:5) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 7/1 uku. 14 fu. 3.]

14. Wakristo wanaweza ‘kushindaje ulimwengu’? (1 Yh. 5:3, 4) [si-SW uku. 258 fu. 12]

15. Usemi wa Petro ‘kuweka karibu akilini siku ya Yehova’ wahusisha nini? (2 Pet. 3:12) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w97-SW 9/1 uku. 19 fu. 2.]

16. Ni nini kinachohusishwa na usafi wa kiroho, nao wasaidiaje kulinda familia ya mtu? (2 Kor. 7:1) [fy-SW uku. 46 fu. 14]

17. Kupatana na Ufunuo 1:7, wale waliomdunga Yesu watamwonaje ‘akija pamoja na mawingu’? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w93-SW 5/1 uku. 22 fu. 7.]

18. Wakristo wenye kulinda ‘hujikaziaje uangalifu kwa wao wenyewe na kuwa macho’? (Luka 21:34, 36) [jv-SW uku. 714 fu. 4]

19. Wale wanaofanyiza tengenezo moja la kweli la Kikristo leo wanafikiaje uelewevu wa Neno la Mungu? [jv-SW uku. 708 fu. 3]

20. Ni matakwa gani ya Kimaandiko ambayo lazima yatimizwe na tengenezo pekee la Kikristo la kweli katika siku za mwisho? [jv-SW uku. 706 fu. 3]

Toa neno au fungu la maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Ni lazima mume na mke _________________________ kwa mmoja na mwenzake, wakikumbuka kwamba ______________________________ ni wa maana zaidi ya sura ya nje. [fy-SW uku. 26 sanduku la kupitia]

22. Barua ya Paulo kwa Waebrania yaonyesha kwamba sehemu mbalimbali za _________________________ zilikuwa kigezo kilichofanywa na Mungu kikielekezea kwenye mambo makubwa zaidi yaliyokuwa mbele, yote yakifikia upeo katika _________________________ , ule utimizo wa Sheria. [si-SW uku. 247 fu. 23]

23. Kwenye 2 Petro 1:5-8, mtume Petro apendekeza _________________________ ili kujenga sifa za kimungu ambazo zitatuzuia kuwa ama _________________________ ama _________________________ . [si-SW uku. 255 fu. 9]

24. Waume na wake wawasilianapo _________________________ na _________________________ ni muhimu sana. [fy-SW uku. 36 fu. 21]

25. Ili tukimbie shindano la mbio lililo mbele yetu, twahitaji kuondoa kila uzito na _________________________ ambayo hututatanisha kwa urahisi, ambayo ni _________________________. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w98-SW 1/1 uku. 10 fu. 15.]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Wakati wa kifungo cha Paulo cha kwanza katika Roma, (Onesiforo; Onesimo; Onani) mtumwa mtoro wa nyumbani mwa (Filipo, Festo; Filemoni), alikuwa miongoni mwao waliosikiliza mahubiri yake. [si-SW uku. 242 fu. 2]

27. (Upendo; Staha; Ukaribishaji-wageni) wafafanuliwa kuwa “kuwapa wengine ufikirio, kuwaheshimu.” [fy-SW uku. 30 fu. 7]

28. Kwenye Luka 14:28, Yesu asema juu ya (kupanga kimbele; kutopoteza pesa; kuepuka kukopa fedha). [fy-SW uku. 40 fu. 4]

29. “Ubwana” unaotajwa kwenye Yuda 8 hurejezea (Cheo cha Yesu; enzi kuu ya Yehova; mamlaka katika kutaniko la Kikristo iliyopewa na Mungu). [si-SW uku. 263 fu. 9]

30. Kwenye Ufunuo 11:11, zile “siku tatu na nusu,” wakati ambapo mabaki ya watiwa-mafuta walionekana wakiwa maiti zilizokufa machoni pa adui zao, hurejezea (miaka mitatu na nusu; kipindi kifupi cha wakati; miezi mitatu na nusu). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona re-SW uku. 167 fu. 21.]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Mit. 8:30; Mt. 19:13-15; Ebr. 2:1; Yak. 4:15; 1 Pet. 3:4

31. Ili tukinze kupeperushwa mbali na propaganda yenye kuendelea inayowekwa mbele yetu na ulimwengu huu, twapaswa “kukazia uangalifu zaidi kuliko ilivyo kawaida” kwa Neno la Mungu kupitia mazoea mazuri ya funzo na ratiba nzuri ya usomaji wa Biblia. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w98-SW 1/1 uku. 7 fu. 9.]

32. Wakati wowote tufanyapo mipango ya wakati ujao, twapaswa kufikiria kwa sala jinsi ambavyo mipango hiyo inafaana na makusudi ya Mungu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w97-SW 11/15 uku. 21 fu. 10-11.]

33. “Roho ya utulivu na ya upole” ya mke na mama Mkristo haimpendezi mume wake tu bali la maana zaidi humpendeza Mungu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 5/15 uku. 19 fu. 12.]

34. Akifuata kielelezo cha Yehova, baba mzuri apaswa kujitahidi kusitawisha uhusiano mchangamfu wenye upendo pamoja na mtoto wake tangu mwanzo wa maisha ya mtoto. [fy-SW uku. 54 fu. 7]

35. Kwa kuwa Yesu hakuwa mwenye upendeleo katika kuwabariki watoto wachanga, mtu hapaswi kuwaona watoto wa kiume kuwa bora kuliko watoto wa kike. [fy-SW uku. 52 fu. 4]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki