Sanduku La Swali
◼ Je, uko tayari kwa hali ya dharura?
Katika ulimwengu wa sasa, “wakati na tukio lisilotazamiwa” mara nyingi hutukia wakati uleule na kutokeza dharura ya kitiba, kutia ndani msongo wa kutiwa damu mishipani. (Mhu. 9:11, NW) Ili tujitayarishe kwa tukio hilo, Yehova ameandaa msaada katika njia nyingi kupitia tengenezo lake, lakini anatutazamia tufanye sehemu yetu. Hapa chini kuna orodha ya kukusaidia.
• Beba kadi ya Mwelekezo wa Mapema Kuhusu Tiba/Ondoleo la Hatia nyakati zote.
• Hakikisha kwamba watoto wako wanabeba Kadi ya Utambulishi ya wakati wa sasa.
• Pitia nyongeza ya Huduma ya Ufalme Yetu ya Septemba 1992, ukijizoeza jinsi ya kusababu na madaktari na mahakimu kuhusu tiba ya mtoto wako.
• Pitia makala zinazohusu visehemu maalum vya damu na vibadala vya damu. (Vichapo vinavyopendekezwa: Mnara wa Mlinzi, Oktoba 1, 1994, ukurasa wa 31; Juni 1, 1990, ukurasa wa 30-31; Machi 1, 1989, ukurasa wa 30-31; Amkeni!, Desemba 8, 1994, ukurasa wa 23-27; Agosti 8, 1993, ukurasa wa 22-25; Novemba 22, 1991, (la Kiingereza), ukurasa wa 10; na nyongeza za Huduma ya Ufalme Yetu, Septemba 1992 na Novemba 1990. Viweke kwenye faili viwe tayari unapovihitaji.)
• Amua kwa kutegemea dhamiri yako kama waweza kuruhusu kutumiwa kwa mashine ya kuzungusha damu nje ya mwili wako au waweza kukubali vitu vilivyo na visehemu vya damu.
• Kabla ya kwenda hospitalini, ikiwezekana, wajulishe wazee ili waweze kukutegemeza na kuwasiliana na Halmashauri ya Uhusiano na Hospitali ikihitajika. Kuhusu mtoto mchanga, waombe wazee waijulishe Halmashauri hiyo mapema.
Tangaza Waziwazi Msimamo Wako wa Kukataa Damu: Ripoti zaonyesha kwamba akina ndugu na dada fulani hungoja hadi dakika ya mwisho ndipo wawaambie madaktari kwamba hawataki damu. Hilo si jambo la haki kutendea wafanyakazi wa kitiba nalo hukufanya uwe katika hatari ya kutiwa damu mishipani. Madaktari wakijua masadikisho yako na matakwa yako yanategemezwa kwa hati zilizotiwa sahihi ambazo zaeleza mielekezo hususa, huwasaidia kuendelea bila kukawia na mara nyingi huwapa uchaguzi wa ziada kwa tiba isiyohusisha damu.
Kwa kuwa hali ya dharura ya kitiba yaweza kutokea wakati wowote, mara nyingi wakati ambapo huitazamii, chukua hatua sasa za kujilinda mwenyewe na watoto wako usitiwe damu mishipani.—Mit. 16:20; 22:3.