Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/01 uku. 4
  • Kuhubiri Tukitumia Video —To the Ends of the Earth

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuhubiri Tukitumia Video —To the Ends of the Earth
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2001
  • Habari Zinazolingana
  • Wamishonari Wasukuma Mpanuko wa Ulimwenguni Pote
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
  • Kufanya Wanafunzi wa Kweli Leo
    Amkeni!—1994
  • Kutoka Kuwa Wanafunzi Wenye Mafanikio Hadi Kuwa Wamishonari Wenye Mafanikio
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Wamisionari wa Gileadi—Wamejitoa kwa Kusudi Moja
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2001
km 12/01 uku. 4

Kuhubiri Tukitumia Video —To the Ends of the Earth

Ni nani ambao yaelekea watatazama video To the Ends of the Earth tena na tena? Ni wale walio na mradi wa kuwa mishonari. Kwa nini? Ili wajifahamishe na shule ya Biblia ya Gileadi ya Watchtower. Video hii ilitayarishwa ili kuadhimisha ukumbusho wa miaka 50 ya shule hii ya pekee ambayo ilianzishwa ili kupanua kazi ya kuhubiri hadi “miisho yote ya dunia.” (Zab. 22:27) Kuitazama video hii kutaongeza uthamini kwa kazi iliyo ya maana zaidi ya kuhubiri habari njema na kutakuchochea uongeze utendaji wako. Fikiria kwa uzito: (1) Mapema miaka ya 1940, ni nini kilichokuwa hangaiko kuu la tengenezo la Yehova? (Mdo. 1:8) (2) Mwaka wa 1942, ni unabii gani wa Biblia wenye kushangaza uliokuwa unatimizwa, na tulizingatia jambo gani tofauti na ulimwengu kwa ujumla? (Ufu. 17:8; w89-SW 4/15 uku. 14 fu. 12) (3) Ni mipango gani iliyofanywa ili kutumia kwa manufaa kipindi cha amani kilichotazamiwa baada ya Vita ya Ulimwengu ya Pili? (jv-SW uku. 522 fu. 1-2) (4) Ni sifa gani za wanafunzi wa darasa la kwanza la Shule ya Gileadi zinazokuvutia? (5) Katika miaka 50 ya kwanza ya Gileadi, ni wanafunzi wangapi waliohitimu, na walitumwa katika nchi ngapi? (6) Wanafunzi hufunzwa Biblia kwa undani kadiri gani? (7) Ni nini ambacho humfanya mtu awe mishonari na mwalimu bora wa Neno la Mungu? (8) Maisha ya mishonari yakoje, na ni magumu gani ambayo wao hupata? (9) Mishonari huhisije kuhusu njia yao ya maisha, nao hupata shangwe gani kutokana na maisha yao ya kujitolea? (10) Maelfu ya mishonari wametimiza nini kufikia sasa? Toa mifano. (11) Una maoni gani kuhusu akina ndugu na dada ambao wameenda kwenye “miisho yote ya dunia” kuhubiri? (12) Mfano uliowekwa na mishonari unakutia moyo ufanye nini, na kwa nini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki