Utayatumiaje Maisha Yako?
1 Nyakati nyingine watoto huulizwa, “Ungependa kufanya nini ukiwa mkubwa?” Ulipokuwa mvulana mdogo, je, ulisema kwamba ungependa kuwa mchungaji wa ng’ombe? mzima moto? au mwangalizi wa mzunguko? Au ulipokuwa msichana mdogo, ulisema ungependa kuwa mcheza-dansi? muuguzi? au mmishonari? Lakini sasa kwa sababu umekua, unapaswa kujiuliza swali lingine, ‘Nitatumiaje maisha yangu?’ Je, uko tayari kufanya uamuzi?
2 Ili kukusaidia kufanya maamuzi yanayofaa, tengenezo la Yehova lilitoa DVD yenye kichwa Young People Ask—What Will I Do With My Life? Tafadhali itazame, na ufikirie kwa uzito kuhusu yaliyomo, kutia ndani drama, mahojiano, na habari nyingine za ziada. Yaliyomo yameorodheshwa kwenye sanduku “Main Menu.”
3 Drama: Unapotazama drama hiyo, fikiria maswali haya: (1) Kuna ulinganifu gani kati ya Timotheo, anayezungumziwa kwenye Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, na Andre? (Mdo. 16:1; 1 Tim. 4:8; 2 Tim. 1:5) (2) Ni nani aliyekuwa akimshinikiza Andre akazane zaidi katika riadha, na alifanyaje hivyo? (3) Ni nani waliomsaidia Timotheo na Andre wafanye vema, na walitumia njia gani kufanya hivyo? (2 Tim. 1:1-4; 3:14, 15) (4) Mashauri yanayopatikana kwenye Mathayo 6:24 na Wafilipi 3:8 yalimwathirije Andre, na yanakuathirije?
4 Maonyesho Mbalimbali (Scenes): Baada ya kutazama drama yote, tazama tena sehemu zifuatazo, na ujibu maswali haya. “Paul and Timothy”: Ni yapi yaliyo mashauri ya mwisho ya Paulo kwa Timotheo? (2 Tim. 4:5) “Giving Jehovah Your Best”: Una malengo gani ya kiroho? “Taking a Stand for Jehovah”: Furaha ya kweli inatoka wapi? “Grandmother’s Advice”: Kuna ubaya gani kuwa maarufu katika ulimwengu wa Shetani? (Mt. 4:9) “No Regrets”: Kutambua jambo gani kunaweza kukufanya uridhike maishani?—Met. 10:22.
5 Mahojiano (Interviews): Unapotazama kila moja ya sehemu zifuatazo, unaona ni jambo gani unaloweza kufanya ili umpe Yehova kilicho bora? (1) “Dedication to Vain Pursuits or to God?” (Kujitoa kwa Mambo Yasiyo ya Maana au kwa Mungu?) (1 Yoh. 2:17); (2) “Learning to Enjoy Your Ministry” (Kujifunza Kufurahia Huduma Yako) (Zab. 27:14); na (3) “An Open Door to Service” (Mlango Ulio Wazi wa Utumishi).—Mt. 6:33.
6 Kufikiria Mambo Yaliyopita (Looking Back): Unaweza kujibuje? (1) Ndugu na dada walioonyeshwa katika sehemu hii walikuwa wakifuatilia kazi gani, na kwa nini? (2) Walipata mafanikio gani? (3) Ni nini kilichobadili maisha yao? (2 Kor. 5:15) (4) Wamejitahidi kufikia miradi gani ya kitheokrasi badala ya kazi walizokuwa nazo, na ni kwa nini waliona hawawezi kufuatilia miradi ya aina mbili? (5) Wana majuto yoyote kwa sababu walibadili mambo waliyofuatilia maishani? (6) Walisema jambo gani ambalo limekufanya ufikiri kuhusu jinsi utakavyoyatumia maisha yako?
7 Mahojiano ya Ziada (Supplementary Interviews): Katika mahojiano hayo, umejifunza jambo gani ambalo limekuchochea ujihusishe zaidi katika utumishi wako kwa Yehova? (1) “The Value of Personal Study,” (Thamani ya Funzo la Kibinafsi) (2) “Alternative Witnessing,” (Mahubiri ya Badala) (3) “Bethel Service,” (Utumishi wa Betheli) (4) “Gilead Missionary Training,” (Shule ya Wamishonari ya Gileadi) na (5) “Ministerial Training School,” (Shule ya Mazoezi ya Kihuduma). Pitia sehemu yenye kichwa “Index to Published Information on Related Subjects,” na usome habari za ziada kuhusu kile kinachokupendeza zaidi.
8 Basi umeamua jinsi utakavyoyatumia maisha yako? Paulo alimhimiza Timotheo: “Tafakari mambo haya; zama katika hayo, ili maendeleo yako yawe wazi kwa watu wote.” (1 Tim. 4:15) Tunakuhimiza ufanye vivyo hivyo kuhusu yale ambayo umeona na kusikia katika DVD hiyo. Mwombe Yehova akusaidie kufanya uamuzi unaofaa ambao utakuletea shangwe na uradhi katika maisha yako sasa na maisha yenye furaha na yanayothawabisha wakati ujao.
[Sanduku katika ukurasa wa 6]
MAIN MENU
Play Drama
Scenes (sehemu 11)
Interviews
Play All
Sections (sehemu 3)
Looking Back
Supplementary Material
Supplementary Interviews
Index to Published Information on Related Subjects
Subtitles
Hearing Impaired
None
Ili kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine bonyeza sehemu iliyoandikwa Next ▶, ◀ Back, na Main Menu.