Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Agosti 31, 2009. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 20 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Julai 6 hadi Agosti 31, 2009.
1. Kwa nini mtu ‘aliyewalaani’ wazazi wake alihukumiwa kifo? (Law. 20:9) [w04 5/15 uku. 24 fu. 7]
2. Kwa kuwa wanaume wote Waisraeli walitakiwa kuhudhuria Sherehe ya Keki Zisizo na Chachu, ni nani aliyevuna matunda ya kwanza ya toleo la shayiri? (Law. 23:5, 11) [w07 7/15 uku. 26 fu. 3]
3. Ni nini kinachoonyeshwa kimbele na mwaka wa Yubile? (Law. 25:10, 11) [w04 7/15 uku. 26-27]
4. Je, Waisraeli walizitumia zile ishara, au “alama,” zinazotajwa katika Hesabu 2:2 katika ibada? [w02 9/15 uku. 21 fu. 4]
5. Wahubiri wa wakati wote wa Ufalme leo, wanaonyesha roho au mtazamo gani, ambao Wanadhiri katika taifa la kale la Israeli walikuwa nao? (Hes. 6:3, 5, 6) [w04 8/1 uku. 24-25]
6. Ni kanuni gani kuhusu kustaafu kwa Walawi ambayo watu wa Yehova wanaweza kufuata leo? (Hes. 8:25, 26) [w04 8/1 uku. 25 fu. 1]
7. Kwa nini Waisraeli walionyesha “tamaa ya uchoyo,” nasi tunajifunza nini kutokana na jambo hilo? (Hes. 11:4) [w01 6/15 uku. 14-15; w95 3/1 uku. 16 fu. 10]
8. Kwa nini Miriamu tu ndiye aliyeshikwa na ukoma, na tunajifunza jambo gani muhimu kutokana na hilo? (Hes. 12:9-11) [w04 8/1 uku. 26 fu. 2; it-2 uku. 415 fu. 1]
9. Yoshua na Kalebu walimaanisha nini walipowaita Wakanaani “mkate”? (Hes. 14:9) [w06 10/1 uku. 17 fu. 5; it-1 uku. 363-364]
10. Kuna mfano gani wenye kuonya katika Hesabu 21:5? [w99 8/15 uku. 26-27]