Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Maswali yafuatayo yatazungumziwa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanza Juni 28, 2010. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 20 linalotegemea habari zilizozungumziwa katika hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Mei 3 hadi Juni 28, 2010.
1. Tunaweza kujifunza nini kutokana na jinsi Daudi alivyoomboleza kifo cha Abneri? (2 Sam. 3:31-34) [w05 5/15 uku. 17 fu. 6; w06 7/15 uku. 21 fu. 9-10]
2. Nathani alifanya kosa gani, na kwa nini hakukataliwa asiwe nabii wa Yehova? (2 Sam. 7:3) [rs uku. 178 fu. 3]
3. Andiko la 2 Samweli 7:14 lilitimizwaje? [it-1-E uku. 273 fu. 3; it-2-E uku. 818 fu. 2]
4. Kwa nini mambo ambayo Daudi alimtendea Mefiboshethi yalikuwa fadhili zenye upendo, nayo yanapaswa kutusukuma tufanye nini? (2 Sam. 9:7) [w02 5/15 uku. 19 fu. 5]
5. Tunajifunza nini kutokana na uhusiano kati ya Itai Mgathi na Mfalme Daudi? (2 Sam. 15:19-22) [w09 5/15 uku. 27-28]
6. Maandiko yanaonyeshaje kwamba shtaka la Ziba kumwelekea Mefiboshethi lilikuwa la uwongo? (2 Sam. 16:1-4) [w02 2/15 uku. 14-15 fu. 11, maelezo ya chini.]
7. Wakati Daudi alipomwomba Barzilai mwenye umri wa miaka 80 awe akiishi katika makao yake ya kifalme, kwa nini Barzilai alimpendekeza Kimhamu? (2 Sam. 19:33-37) [w07 6/1 uku. 24 fu. 13]
8. Ni katika njia gani ambayo unyenyekevu wa Yehova ulimfanya Daudi awe mkuu? (2 Sam. 22:36) [w07 11/1 uku. 5 fu. 2; w04 11/1 uku. 29]
9. Kwa nini Adoniya alijaribu kunyakua utawala Daudi alipokuwa angali hai? (1 Fal. 1:5) [w05 7/1 uku. 28 fu. 5]
10. Kwa nini Yehova alijibu sala ya Sulemani alipoomba hekima na utambuzi? (1 Fal. 3:9) [w05 7/1 uku. 30 fu. 2]