Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb16 Juni uku. 2
  • Kuboresha Ustadi Wetu Katika Huduma—Tumia Video Kufundisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuboresha Ustadi Wetu Katika Huduma—Tumia Video Kufundisha
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
  • Habari Zinazolingana
  • Tumia Video Kuwafundisha Wanafunzi Wako wa Biblia
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2019
  • Tumia Video Kufundisha
    Huduma ya Ufalme—2006
  • Matokeo ya Video Zinazotoa Ushahidi
    Huduma Yetu ya Ufalme—2002
  • Je, Inafaa Nitazame Video za Muziki?
    Amkeni!—2003
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
mwb16 Juni uku. 2

MAISHA YA MKRISTO

Kuboresha Ustadi Wetu Katika Huduma—Tumia Video Kufundisha

KWA NINI NI MUHIMU:

Wahubiri wanaonyesha video katika huduma

Video zinahusisha hisi ya kuona na kusikia na hivyo zinachochea na kugusa mioyo ya watu. Zinamsaidia mtu akaze fikira zaidi na kukumbuka mambo kwa muda mrefu. Yehova alituwekea mfano bora zaidi wa kufundisha kwa kutumia picha.—Mdo 10:9-16; Ufu 1:1.

Video Je, Mungu Ana Jina?, Ni Nani Aliyeitunga Biblia?, na Tunawezaje Kuwa na Hakika Kwamba Yale Yaliyoandikwa Katika Biblia Ni ya Kweli? zinaambatana na somo la 2 na 3 katika broshua Habari Njema. Video Kwa Nini Ujifunze Biblia?, Ni Nini Hutendeka Kwenye Funzo la Biblia?, na Ni Nini Hutendeka Katika Jumba la Ufalme zinawatia watu moyo kujifunza Biblia pamoja nasi au kuhudhuria mikutano yetu. Pia, video zetu nyingine zinaweza kutumiwa kufundisha wanafunzi wetu wa Biblia.—km 5/13 3.

JINSI YA KUFANYA HIVYO:

  • Pakua video ambayo ungependa kumwonyesha mwenye nyumba

  • Tayarisha swali moja au mawili yanayojibiwa katika video hiyo

  • Tazama video pamoja naye

  • Zungumzia mambo makuu

JARIBU DOKEZO HILI:

  • Tumia ukurasa wa nyuma wa mojawapo ya trakti zetu na umwonyeshe mtu alama inayofungua video Kwa Nini Ujifunze Biblia?

  • Onyesha video Tunawezaje Kuwa na Hakika Kwamba Yale Yaliyoandikwa Katika Biblia Ni ya Kweli? na utoe broshua Habari Njema ukikazia somo la 3

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki