Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwbr19 Aprili uku. 1
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha
  • Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
  • Vichwa vidogo
  • APRILI 22-28
Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha—2019
mwbr19 Aprili uku. 1

Marejeo ya Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha

APRILI 22-28

Kutafuta Hazina za Kiroho

it-1 1197-1198

Kutoweza Kuharibika

Wakiwa na umbo kama lile ambalo Yesu alikuwa nalo baada ya kufufuliwa, warithi washirika wa Yesu wanafufuliwa pia si ili tu wapate uzima wa milele wakiwa viumbe wa roho, bali wanapata uhai usioweza kufa na usioweza kuharibika. Baada ya kuishi, kutumikia kwa uaminifu, na kufa wakiwa na miili ya kibinadamu inayoweza kuharibika, sasa wanapokea miili ya kiroho isiyoweza kuharibika, kama Paulo anavyosema kwenye 1 Wakorintho 15:42-54. Hivyo, ni wazi kwamba uhai usioweza kufa unawakilisha ubora wa uhai wanaofurahia, yaani, uhai ulio na uwezo wa kuendelea kuwapo bila kukoma na kutoweza kuangamizwa, ilhali kutoweza kuharibika kunarejelea mwili ambao Mungu anawapa, ambao kiasili hauwezi kuoza, kudhoofika, au kuangamia. Hivyo inaonekana kwamba Mungu anawapa nguvu za kujiendeleza kuishi, hawahitaji kutegemea vyanzo vya nishati nje na mwili wao kama viumbe wengine wa kimwili na wa roho wanavyofanya. Huo ni uthibitisho mkubwa kwamba Mungu ana uhakika kabisa kuwaelekea. Hata hivyo, kwa kuwa tu wanaweza kuendelea kuwepo bila kumtegemea yeyote na bila kuangamizwa haimaanishi kwamba hawako chini ya udhibiti wa Mungu. Kama Kristo Yesu ambaye ndiye Kichwa chao, wanaendelea kujitiisha kwa mapenzi na mwongozo wa Baba yao.—1Ko 15:23-28; ona uhai usioweza kufa; nafsi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki