Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb22 Septemba uku. 3
  • Jipatie Hekima ya Kukabiliana na Changamoto za Kila Siku Kwenye JW.ORG

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jipatie Hekima ya Kukabiliana na Changamoto za Kila Siku Kwenye JW.ORG
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
  • Habari Zinazolingana
  • Dokezo la Kujifunza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Unaweza Kupata Msaada
    Amkeni!—2020
  • Dokezo la Kutumia Tovuti
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Tovuti Yetu Rasmi—Imetengenezwa ili Itunufaishe Sisi na Wengine
    Huduma Yetu ya Ufalme—2012
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2022
mwb22 Septemba uku. 3

MAISHA YA MKRISTO

Jipatie Hekima ya Kukabiliana na Changamoto za Kila Siku Kwenye JW.ORG

Neno la Mungu linatuandalia vifaa kamili vya kukabiliana na majaribu katika siku hizi ngumu za mwisho. (2Ti 3:1, 16, 17) Hata hivyo, huenda nyakati nyingine tukahitaji msaada wa kupata kanuni za Biblia zinazohusu hali hususa tunayokabili. Kwa mfano, je, wewe ni mzazi anayetafuta ushauri wa jinsi ya kuwalea watoto? Je, wewe ni kijana anayekabili majaribu ya imani? Je, unaomboleza kwa sababu ya kufiwa na mume au mke wako? Utapata habari kwenye jw.org zitakazokuonyesha kanuni hususa za Biblia ambazo zitakusaidia kukabiliana na hali hizo na hali nyingine nyingi.​—Met 2:3-6.

Tovuti ya jw.org kwenye tablet. Picha ya ndani inaonyesha tabo ya MAFUNDISHO YA BIBLIA.

Kwenye ukurasa wa mwanzo wa jw.org, bofya tabo ya MAFUNDISHO YA BIBLIA. (Ona picha ya 1.) Kisha kwenye orodha inayojitokeza, teua sehemu unayotaka. Au teua MAKTABA > MFULULIZO WA MAKALA kisha uchague sehemu ambazo ungependa kusoma. (Ona picha ya 2.) Unaweza kupata sehemu hizohizo kwenye JW Library®.a Programu hiyo pamoja na tovuti yetu zimetayarishwa kwa njia inayopendeza kutafuta habari mbalimbali. Pia, unaweza kutafuta habari hususa kwa kutumia sehemu ya tafuta kwenye jw.org.

 Tovuti ya jw.org kwenye tablet. Picha ya ndani inaonyesha tabo ya MAKTABA na ya MFULULIZO WA MAKALA.

Andika habari zifuatazo katika kisanduku cha kutafuta, na uchague makala ambazo ungependa kusoma.

  • Kulea watoto

  • Vijana walioshuka moyo

  • Kifo cha mwenzi wa ndoa

a Baadhi ya mifululizo ya makala, inapatikana tu kwenye jw.org.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki