Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 3/15 uku. 141
  • Alama za Ukristo wa Kweli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Alama za Ukristo wa Kweli
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nani Ataeneza Evanjeli Katika Uingereza?
    Amkeni!—1995
  • Alama Usoni ‘Kitambulisho’ cha Nigeria Kinachotoweka
    Amkeni!—1999
  • Uenezaji wa Evanjeli—Mahali Pao Katika Ibada ya Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
  • Kanisa La Kweli na Msingi Wake
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 3/15 uku. 141

Alama za Ukristo wa Kweli

KARIBU kila mtu atakubali kwamba kanisa kubwa au ushirika wenye kuendelea kwa muda mrefu wa kanisa haumaanishi kwamba mtu anazo alama za Ukristo wa kweli. Lakini alama hizo zimepaswa ziwe nini kwa kweli? Angalia yaliyosemwa na E. M. Green katika kitabu chake juu ya uinjilisti kati ya Wakristo wa kwanza:

“Wonyesho mmojawapo wenye kutokeza sana katika uinjilisti katika siku za kwanza ni watu waliokuwamo. Kuijulisha imani hakukuonwa kama utendaji wa wenye bidii zaidi au wa mwinjilisti aliyechaguliwa rasmi. Uinjilisti ndiyo iliyokuwa haki na wajibu wa kila mshiriki wa Kanisa. Tumewaona mitume na mitume wenye kuzunguka-zunguka, matajiri na maskini, wenye hekima nyingi na wavuvi wa samaki wote wakishiriki kwa uchangamfu katika kazi hii ya maana iliyopewa kwa Kanisa na Kristo. Watu wa vivi hivi wa Kanisa waliiona kama kazi yao: Ukristo ulikuwa kazi ya watu wasio mapadre, ukienezwa na wamisionari wa vivi hivi. . . .

“Uchangamfu huu wenye nguvu za kujieneza kwa upande wa watu hao wa namna mbalimbali na wa umri mbalimbali, hali ambazo walikuwa nazo, wa wanaume na wanawake, na wa watu wenye malezi mbalimbali ulitegemezwa na sifa ya maisha zao. Upendo wao, furaha yao, mazoea yao yaliyogeuzwa na tabia zilizogeuzwa kidogo kidogo viliyapa waliyoyasema nguvu nyingi.”

Kwa hiyo, kuenezwa kwa injili kwa bidii katika kundi, na wazee na vijana, na vile vile ushuhuda wa mageuzi ya kweli ya Mkristo​—hizi ndizo alama za Ukristo wa kweli.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki