Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 9/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1990
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1991
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 9/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Uhalifu Toleo la Januari 8, 1990 lilikuwa na ushauri ulionigutusha. Kuhusu kukabiliana na waviziaji, ilitaarifiwa hivi: “Mtazame mtu yule machoni, na ujaribu kumkazia macho bila kuwaya-waya.” Mimi niliishi kwa miaka mingi katika maeneo yenye uhalifu mwingi na nilifundishwa kutowatazama washambulizi machoni, kwa kuwa wangeweza kuhisi kwamba unajaribu kuwatambua ili wakati ujao wafanyiwe mashtaka.

R.L., United States

Sisi twaafikiana nawe kwamba, chini ya hali fulani, kumkazia macho mtu awezaye kuwa mwenye uadui kungeweza kuamsha jeuri yake. Hata hivyo, wenye mamlaka fulani huamini kwamba kudumisha uhusiano wa macho wakati wa kuviziwa ni afadhali kuliko kutazama huku na huku kwa wasiwasi mwingi au kuweka macho yakiwa yamekazwa chini—mwenendo ambao ungeweza kuonyesha hofu au babaiko.—MHARIRI.

Kitu Kibaya Kuliko UKIMWI Mimi nililelewa nikiwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova. Lakini nilitaka kupendwa na nikaingia katika uandamani mbaya. Nimesaidiwa kurudi kwenye barabara ifaayo kabla haijawa kuchelewa mno. Ile makala juu ya mhanga wa UKIMWI (Januari 8, 1990) itanisaidia kubaki katika barabara hiyo. Mwanamume huyo alikuwa shujaa kubadilika, kwa maana wengi sana wangalikata tamaa. Maono yake yaonyesha kwamba ulimwengu hauna chochote cha kututolea sisi na kwamba bila upendo na upendeleo wa Yehova, sisi ni wafu.

D.C., New Zealand

Teketezo la Umati Mke wangu na mimi twataka kutoa asante zetu na uthamini wa kina kirefu kwa usemi wa kutoboa wazi na wenye kueleweka vizuri uliotumiwa katika makala za lile Teketezo la Umati. (Novemba 8, 1989) Zile foto na ramani zilitugusa kwa kina kirefu. Zaonyesha ukatili na unyama wa mfumo wa kibinadamu. Hasa tuliionea shangwe ile makala ya ufufuo, yenye mtazamo chanya na yenye kufariji sana! Ingawa hatukupatwa na mambo hayo kibinafsi, ni jambo la maana kuyasema na kuyakumbuka.

I.L., Jamhuri ya Muungano ya Ujeremani

Ni lazima mimi niwape heko waandikaji wenu. Hakika wao walifanya utafiti. Toleo hilo litakuwa katika maktaba yangu mpaka nife! Ingawa mimi sitakuwa kamwe ‘Shahidi wa Yehova,’ ningependa kuwajulisha kwamba kuna watu ambao huwa na shukrani kwenu kwa ajili ya habari za jinsi hiyo.

A.S., United States

Chakula Salama Nilisoma kwa upendezi ile makala “Fanya Ulaji Wako Uwe Salama” katika Amkeni! ya Aprili 8, 1990. Karibu mwaka mmoja na nusu uliopita (sasa ni miwili na nusu), tulisafiri kwenye nchi ya kigeni. Nilistaajabu kujua kwamba wao wanaosha vyombo kwa maji moto yenye sabuni lakini hawasuzi kamwe yale mapovu ya sabuni kabla ya kukausha vyombo. Kwa kuwa makala yenu haikutaja kusuza, je! hii yamaanisha kwamba nyinyi hamfikiri jambo hili lahitajiwa kabisa?

S. B., United States

Kusuza vyombo vyenye sabuni ni hatua ya maana ya kanuni za afya, nasi twathamini kwamba umetaja jambo hilo.—MHARIRI.

Inashangaza ni watu wangapi huacha chakula kikiwa katika joto la kadiri ya chumbani kwa muda wa saa nyingi kwa safari moja au hawafanyi mambo sahili kama kuosha mikono kabla ya kupika. Mimi nimekuwa kwenye makao makuu yenu katika New York, na sikuzote mimi huvutiwa na usafi wao wa kupindukia. Sisi sote twahitaji kuiga kielelezo hicho katika makao yetu.

M. B., United States

Kuacha Kuvuta Sigareti Asanteni kwa ile makala “Njia Kumi za Kuacha Kuvuta Sigareti.” (Machi 8, 1990) Mimi naitumia kusaidia mtu fulani ambaye amekuwa mvuta sigareti kwa muda mrefu na amekuwa hawezi kuacha. Pia nilipiga nakala zilizokuzwa za makala hiyo nikaziweka kazini pangu, ambapo wavuta sigareti wengi hupita. Walivutiwa na habari hizo, na baadhi yao wanatumia mambo waliyosoma.

R. L. B. S., Brazili

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki